Mishahara serikalini!!

Dec 26, 2011
28
9
nimeikuta hii kwenye post ya jamaa yangu fb! wanajamvi nisaidieni nini sababu ya hizi tofauti?
Tofauti ya mishahara miongoni mwa wafanyakazi wa umma wenye kiwango kimoja cha elimu?
CHETI
mwalimu 244,400
afya 472,000
kilimo/mifugo 959,400
... sheria 630,000

DIPLOMA
mwalimu 325,700
afya 682,000
kilimo/mifugo 1,133,600
sheria 871,500

DEGREE
mwalimu 469,200
afya 802,200
kilimo na mifugo 1,354,000

Utagundua kwamba aliyesema 'balaa kubwa si kifo bali ni maisha yasiyo na matarjio' yuko sahihi! Walimu hatuna matarajio! change what you see by changing how you see.! Hizi ni dharau tena naweza kuita ni 'ACADEMIC ABUSE'. Tushikamane walimu kuondoa matusi haya
 
Usilolijua litakusumbua, hizo takwimu ulizotoa hapo juu haziko sahihi na pili ujue ukiajiriwa serikalini ajira yako inaongoza na kuratibiwa na mwongozo wa ajira yaani circular ambapo kwa sasa iliyo current ni ya mwaka 2007 nakushauri uitafute uisome utaelewa tofauti ya mishahara inatokana na nini
 
Zinaweza kutokuwa figure sahihi, lamsingi ni kuwa utofauti wa mishahara ktk sekta mbalimbali kwa viwango sawa vya elimu upo! Na chanzo chake ni selikali dhaifu, isiyo kusanya kodi, inayofisadi hata kale kadogo kalikokusanywa, inayogawa rasilimali ktk jina ka uwekezaji huku ikisamehe kodi kwenye vitendea kazi vyao, yenye matumizi ya anasa, yenye makao makuu sehemu mbili tofauti,....nadhani nimejibu sehemu ya swali lako.
 
Angalia hizo data zisije zikachochea mgomo wawafanyakazi kada zote.
 
hakuna kitu hicho,serikali haina pesa ya kuongeza mishahara kiasi hicho,na huwa kikawaida hakuna mpishano mkubwa kiasi hicho,kati ya kilimo na udaktari na kama kweli umefuatilia vyema huwa madaktari mishahara yao ipo juu kuliko kilimo na wanasheria pia,sasa huo uongo sijui umeutoa wapi,huo ni ujumbe ulitumwa na CWT ili kuhamasisha mgomo na ulikuwepo hapa JF wiki moja iliyopita.
 
Usilolijua litakusumbua, hizo takwimu ulizotoa hapo juu haziko sahihi na pili ujue ukiajiriwa serikalini ajira yako inaongoza na kuratibiwa na mwongozo wa ajira yaani circular ambapo kwa sasa iliyo current ni ya mwaka 2007 nakushauri uitafute uisome utaelewa tofauti ya mishahara inatokana na nini

Kama wewe ni great thinker tuletee huo waraka wa 2007 sio kutoa povu tu hapa
 
kama huo ndio ukweli kuna sababu ya hao watu kugoma na wewe uwaunge mkono! kuna sababu gani ya watumishi wenye kiwango sawa cha elimu kulipwa mishahara tofauti? kama baadhi ya kada ni bora kuliko zingne ni vyema watu waambiwe wazi wasisomeshe watoto wao kada kama za elimu, hii inauma sana kwani bei ya sukari ni ileile, pango la nyumba, kodi ya umeme na maji halikadhalika.
 
Walimu kazi zao ni nyepesi kuliko kada zingine ndo maana hata mishahara yao iko chini kuliko watumishi wengine wa umma. Jianzishieni miradi mingine kuongeza kipato!
 
Sikatai kuboreshewa maslahi, lakini siyo sahihi kujilinganisha na fani nyingine. Jaribu kufuatilia hata nchi nyingine, mishahara haiko uniform. Huwezi kukuta mwalimu wa history akalipwa sawa na daktari, eti kisa wote wana degree.
 
Walimu kazi zao ni nyepesi kuliko kada zingine ndo maana hata mishahara yao iko chini kuliko watumishi wengine wa umma. Jianzishieni miradi mingine kuongeza kipato!
Inaonesha una matatizo ya akili wewe,wewe unachokipata kwa sasa hata huu utumbo unaoandika bila mwalimu ungeweza wewe?
 
Back
Top Bottom