Mishahara juu

Mishahara juu

Mimi wa ajira mpya April 2014 sijaona mshahara vp kuna wa ajira mpya aliyeingiziwa kwa kua inasemekana mishahara imeingizwa toka hazina haijapitia halmashauri

ajira mpya huku wamelipwa take home 320000... Ongezeko kama 30000 hv.
 
Mimi wa ajira mpya April 2014 sijaona mshahara vp kuna wa ajira mpya aliyeingiziwa kwa kua inasemekana mishahara imeingizwa toka hazina haijapitia halmashauri

mimi ajira mpya nimepata mshahara wameniongezea tsh 16000 (elfu kumi na sita)
 
Hakika inakera na inaudhi sana tuu,yaani tangu wapate mishahara yao ya mwezi huu julai wamekuwa wakilalamika sana juu ya utapeli waliofanyiwa,na haya ndiyo wanayoyasema nanukuu:-

-"kodi ya nyumba imepanda,umeme bei juu,nauli ya kwendea kazi imepanda,mkaa gunia moja tsh:30000,watoto wanataka ada shuleni,vyakula bei juu,madeni nadaiwa kila kiduka kilichopo mtaani kwetu,saccos nako nadaiwa na bado hisa sijapeleka,dharula ndogondogo kama ugonjwa na wageni hizo hazielezeki.

Mshahara hautoshi nyongeza yenyewe kiduchu,aaah! Sijui nani atanisaidia maana kama ni kudanganywa ilikuwa mei mosi mkuu alipo tuonyesha usanii wake kwakutudanganya hadharani,tucta nao wanatumika.

Sasa najiuliza nimlilie nani maana kufa sifi,maisha magumu,hii serikali hii ya CCM ngoja tutakuna 2015".

-Hayo ndiyo malalamiko yao na siyo yangu mimi willafrica.

Hivyo naomba kuwasilisha jamvini.

umevurugwa wewe. Ulevi wa gongo ni mbaya sana

mkuu elewa kuwa hunitukani mimi bali unatukana wafanyakazi wote tanzania ambao ndio wenye kilio kikali kwa hayo niliyoyaeleza!
-wamekula kiapo dhidi ya serikali ya c.c.m kwa kuinyima kura kwani wanasema imeishia kuwa danganya kwa zaidi ya miaka 50 juu ya maisha bora.
 
mtasubiri sana. Ccm ni nambari one. Labda wafanyakazi wenu hapo Kinondoni ndo wanalalamika
 
Waambie hayo ndo maisha bora waliyohaidiwa, na wao wengi ndo wanaiwezesha ccm wakati wa uchaguzi mkuu, hasa walimu!
 
Back
Top Bottom