Nyongeza ya mshahara mpya ni sh ngapi?
====================================
====================================
Hakika inakera na inaudhi sana tuu,yaani tangu wapate mishahara yao ya mwezi huu julai wamekuwa wakilalamika sana juu ya utapeli waliofanyiwa,na haya ndiyo wanayoyasema nanukuu:-
-"kodi ya nyumba imepanda,umeme bei juu,nauli ya kwendea kazi imepanda,mkaa gunia moja tsh:30000,watoto wanataka ada shuleni,vyakula bei juu,madeni nadaiwa kila kiduka kilichopo mtaani kwetu,saccos nako nadaiwa na bado hisa sijapeleka,dharula ndogondogo kama ugonjwa na wageni hizo hazielezeki.
Mshahara hautoshi nyongeza yenyewe kiduchu,aaah! Sijui nani atanisaidia maana kama ni kudanganywa ilikuwa mei mosi mkuu alipo tuonyesha usanii wake kwakutudanganya hadharani,tucta nao wanatumika.
Sasa najiuliza nimlilie nani maana kufa sifi,maisha magumu,hii serikali hii ya CCM ngoja tutakuna 2015".
-Hayo ndiyo malalamiko yao na siyo yangu mimi willafrica.
Hivyo naomba kuwasilisha jamvini.