Ni muhimu sasa viongozi wa nchi hii waishi kwa kutegemea mishahara yao

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,504
2,180
Kwa maamuzi yanayofanywa na viongozi wetu Kuna haja Sasa ya kuwaondolea hizi HUDUMA za bure Kama usafiri, nyumba, chakula, malipo ya house girl, gharama za umeme na maji, matibabu na mengineyo wabaki na ULINZI tu na badala yake waishi kwa KUTEGEMEA mishahara yao Kama watumishi wengine, hii itawafanya wajue uhalisia wa maisha wanayopitia wananchi angalau kwa namna flani wanaweza kufanya maamuzi sahihi yanayohusu mustakabali wa maisha ya watu.

Nimeangalia tetesi za hoja za wagonjwa wa COVID-19 waliotoroka amana, halafu na maamuzi ya waziri wa viwanda kuhusu bei ya sukari na maamuzi mengine yanayoendelea kufanyika huko nyumbani Tanzania naona kabisa Kuna haja ya Hawa viongozi kuondolewa hizi HUDUMA.

Hebu fikiria mshahara, posho na malupulupu anayopata KIONGOZI kwa mwezi, mtumishi wa kawaida itambidi afanye kazi zaidi ya miaka 30 ili aweze kupata kiwango cha pesa anachopata yeye kwa mwezi na hapo huyo KIONGOZI kila kitu anapata bure na familia ikiwemo kutibiwa ni nje ya nchi au hospitali za hadhi ya juu hapa nchini.. na ndio maana maamuzi hayaakisi uhalisia wa maisha ya watu kabisa.

Hii nchi nilipo, ukiona KIONGOZI kafanya maamuzi lazma ni yale yanagusa maisha na uhalisia wa wananchi wake moja kwa moja na hii ndio inatakiwa iwe hivo..Gharama za sukari na bidhaa zingine mnapandisha, je hali ya wananchi wenu ikoje? Watumishi vipi mishahara yao imepanda kukabiliana na hili ongezeko la gharama za bei?

Ngozi, nyeusi siku zote mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa.

Hivi posho za COVI_19 ziko wapi mbna watu wanatoroka Amana kisa wamekosa HUDUMA muhimu na maiti kutelekezwa?

Parabora.
Geneva- Switzerland
 
Kuna ukweli hapa.. Inabidi wajihudumia wenywe.. Kwanza wanatuibia tu pesa zetu.. Wanajambajamba bure wanaona maisha ni marahisi tu.. Huku mtaani watu tunanuka jasho hadi visogoni.. Pumbaff sana hawa watu
 
Back
Top Bottom