Misemo hii kiboko...weka ya kwako...!

Misemo hii kiboko...weka ya kwako...!

mi mbona nina pesa lkn tabia yangu ni ileile kama ya kabla sijazikamata?
 
1-sio kila shimo lakuingiza mguu
2-mwanamke asingiziwi mtoto
3-ukimpnda mtoto wa kambo ..............malizieni
 
chezea mshahara....usichezee kazi
hodi ya chooni haikaribishwi......
 
Kumpiga chura teke ni kumuongezea mwendo.
 
Unaturingia na nyumba ya self contained kumbe choo cha shimo!!!!!!!
 
Kichungu huonjwa

Kipya kinyemi ingawa kidonda

Hata 6 ilikuwa 9

utamu wa pipi mate yako

mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio

kukopa harusi kulipa matanga by Dr. Remy

Tajiri na gari yake masikini na watoto By Dr Remy

Anahusu!!!!!!!!
 
1. Maskini haishiwi ndoto.

2. Heri karipio la rafiki, kuliko busu la mnafiki.

3. Wakijifanya mapaka, sisi paka tupo.

4. Heri mego kavu pamoja na utulivu kuliko nyumba ya karamu pamoja na kelele/masimango. Hiyo ni Bible
5. Heri mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa!
6. nitaleta nyingine, nimepata mgeni.......
 
Back
Top Bottom