Misamiati maarufu vyuo vikuu

kuwasha blue tooth - kuruhusu wenzako waangalizie
network(protocal) kukaa kimjuano ili msaidiane kwenye mtihani
contena - first year
 
1.'Boom'(fedha za kujikimu zitolewazo na Bodi ya Mikopo ya Elimu Ya Juu kwa wanachuo/wanafunzi)
2. 'Kuuza chai'(Kupiga stori hasa za kuchekesha/au sizizo za kweli)
3.'Nyanga'(Supplementary exams)
4.Kutiwa nyavuni/kukamatwa(kufeli somo hivyo kutakiwa kulirudia)
5.Nondo(vitu visivyoruhusiwa mtihanini lakini vinavyoingizwa kimagendo)
6.Exile(kumpisha mwanachumba mwenzako 'atumie' chumba pekeyake kwa muda fulani
7.'Kupiga Dash'(kushinda bila kula kwasababu ya kuishiwa fedha za kujikimu)
8.Kipanga(mwanafunzi anayejiweza darasani kwa kuelewa haraka au kutosahau haraka)
9.Kilaza(mwanafunzi ambaye uelewa wake ni wa mashaka/haelewi mapema na hachelewi kusahau)
10.'Ungwini'(Masomo ambayo hayaambatani na mahesabu)
11.'Kudesa'(kuiga kwa mwanafunzi mwingine au kuandika kitu kama kilivyokutwa mahali fulani au kwa mtu fulani)
12.'Desa'/'Madesa'(Kitabu/Vitabu visivyo rasmi

Wana JF tuendelee...
Hapo kwenye nyekundu, umechapia, Nyanga, ni masomo magumu, na ni neno ambalo lilikuwa linatumika sana kwa masomo ya engineering, hasa pale COET & ARDHI
 
September conference hii kama una supp...
Exile-ukiwa first year especially au mkiwa wachache room hii itakuhusu kwa wingi
 
Back
Top Bottom