Misaada: To hell with it!!

Misaada: To hell with it!!

Ni aibu kubwa sana kunyimwa misaada kwa sababu za uhalifu dhidi ya ubinadamu , hii maana yake ni kwamba mnanyimwa misaada kwa vile viongozi wenu ni wakatiri mithili ya wanyama wa mwituni , ni fedheha kubwa sana kwa nchi
Kwahiyo wewe kupewa misaada kwako ni jambo la heshima sana kuliko nchi kujitegemea yenyewe.
 
Bandiko lako lina nia nzuri sana, lakini haliwezekani kamwe kwa tanzania kwani serikali zote awamu ya 1-5 hawataki kuona tanzania inajitegemea maana wanaamini hilo likiwezekana na wao hawatakuwa madarakani. Halaf nchi kujitegemea ni mchakato pevu na wa miaka mingi sana na consistency inahitajika na akili kubwa pia zinahitajika. Sasa ccm kila wakileta rais mpya anakuja na yake, nchi haina mipango bali kuna mipango ya marais wa ccm, hivi hapo kuna kujitegemea kutatoka wapi?? Hiyo china ambayo ccm hupenda kujinasibu nayo kwa zaidi ya miaka 50 kumekuwa na strict consistency kwenye ujenzi wa uchumi wao.

Ushahidi upo alituambia majiri wataishi kama mashetani akasahau kwamba you cannot help the poor by destroying the rich
 
Libya iliendelea sana wakati ilipo pigwa sanction
Kilicho muharibia huyu jamaa ni udini
SA nayo pia hivyo hivyo!
Hawa nao ni ubaguzi
Well, kila kitu kina makusudi yake mazuri hapa duniani ni kuwa na hekima na busara mathubuti wakati wa mabadiliko!
Na majitu ambayo haya wezi kufikiri na kazi yao ni kucheza singeli mitaani katika kila tukio wao ni automatically deceased!
 
Kumekuwepo na taarifa kuwa eti tumenyimwa misaada na nchi za jumuiya ya Ulaya, Marekani, na sehemu zingine.

Sababu kuu inayotajwa ni kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini chini ya huu utawala wa Rais John Pombe Joseph ‘Jiwe’ Magufuli [huyu ngosha ana majina mengi kweli...mara Tingatinga...sijui Sizonje....but I digress].

Nachotaka kuzungumzia hapa si hayo madai ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu. Hiyo ni hoja ya siku ingine.

Hapa nataka kuzungumzia huu upumbavu wa misaada.

Kwa tunaofahamiana humu tokea 2004/2005/ 2006/ na 2007, watakuwa wanakumbuka msimamo wangu kuhusu hii misaada ya maendeleo ambayo taifa letu limekuwa likipewa tokea nianze kupata/ kupatwa na fahamu.

Kwa maneno mengine, ni muda mrefu mno sasa tumekuwa tukipewa hii misaada ya maendeleo.

Kilicho cha ajabu kwangu ni: mbona bado tu hatuendelei? Hiyo si inaitwa misaada ya maendeleo? Miongo na miongo tunapokea hiyo misaada lakini ukiangalia maendeleo yenyewe hakuna.

Mbaya zaidi, tuna idadi kubwa tu ya watu [kwa makadirio yangu] ambao wanaipenda sana hii misaada ya maendeleo. Yaani wanapenda sana sisi kupewa hii misaada na hizo nchi.

Sasa ngoja nirudie ambacho nimekuwa nikikisema miaka yote hii ya uwepo wangu hapa JF na huko kwingineko.

Siipendi hii misaada. Siitaki kabisa. Naamini imetulemaza sana hadi kufikia hatua ya kudhani bila kupewa hiyo misaada basi hatutoweza kuendelea.

Naamini kabisa tunaweza kuendelea kiuchumi bila hata hiyo misaada isiyo na msaada wowote. Ni kiasi cha kuamua tu na kubadili mindset yetu kutoka kwenye ‘can’t do’ kwenda kwenye ‘can do’.

Tuna hali ya kujiona hatuwezi kufanya mambo flani flani bila ya kusaidiwa na flani. Mara zote huwa najiuliza, hivi hao wanaotupa hiyo misaada, wao nani aliwasaidia?

Na sizungumzii misaada ya hapa na pale wakati wa majanga ya kiasili, vita, au mazingira fanani. Kwa kawaida binadamu huwa tunapitia changamoto na hatuna budi kusaidiana saidiana pale inapobidi.

Hapa nazungumzia hii misaada isiyoisha ambayo huitwa misaada ya maendeleo.

Siitaki. Siipendi. Naichukia kwa hisia kali sana. Na nasema watunyime tu hiyo misaada ili tuamke toka kwenye huu utegemezi wa kipumbavu tulionao.

Bila hiyo misaada yao tutaangamia au?

Gonga ‘Like’ kama unakubaliana nami.
We menyewe ni mkimbizi ughaibuni, unaishi kwa kubeba mabox, au umeoa bibi kizee ili upate uhali,

sisi tuko huku tandahimba tubangua korosho,

alafu eti unatushauri tususie misaada
 
Kwahiyo wewe kupewa misaada kwako ni jambo la heshima sana kuliko nchi kujitegemea yenyewe.
Huyo Erythrocyte ni wa kuonea huruma. Kutwa anaombea mabaya yawakute watanzania ili tu ionekane uongozi wa rais Magufuli umeshindwa. This is very low. Anafanya hata wenye hoja za msingi waonekane wajinga.
 
Hiyo misaada tukipewa tunaitumia tofauti na malengo, ndio hatuendelei na hatutaendelea kwa misaada!
 
Huyo Erythrocyte ni wa kuonea huruma. Kutwa anaombea mabaya yawakute watanzania ili tu ionekane uongozi wa rais Magufuli umeshindwa. This is very low. Anafanya hata wenye hoja za msingi waonekane wajinga.
ni aibu sana kwa demu kuwa muongo , badala ya kunishutumu mimi kwanini usimshutumu aliyesema akiwa Rais wananchi watalimia meno ?
 
Jambo moja huyu magu aache kubana wapinzani na Uhuru tu baaasi...sisi hayo mengine ni kelele wanalia vyuma vikaza hadi kwa wazungu teh! Teh! ....
 
Yaweza kuwa ni baraka iliyojificha.

Ndo tuanze kujitegemea sasa.

Halafu, hata hao watoa misaada rekodi zao za haki za binadamu zina mushkeli vilevile...
Ili tuwe tunaminya zaidi haki za watu/binadamu yaani unajua ni sawa na nini uwe unakaa kwa baba ako alafu mkienda kupalilia shamba wewe ukakata maharage akakuchapa wewe ususe kula ndo mnachokitaka.

Kulima kwenye shamba la baba ako wakati wewe ni mtu mzima ni aibu tena kubwa sana lakini kama hujifunzi kulima ukiwa hapo utaweza kulima kweli kwenye shamba lako je shamba lako utalitoa wapi wakati wewe ni mtoto mkaidi hutii desturi za maisha wala hutaki kujifunza?
 
Tena misaada yenye mashart ki ukweli haina msaada wowote kwetu bora ikiwezekana tufunge mkanda tu na ndio akili itakuja,hiv wew mtu gani kila siku unaomba unga kwa jirani kwani kipindi cha kulima ulikuwa wapi?
 
Mkuu umenena ,JPM na serikali yake wakomae hadi kieleweke .Kwa kuanzia nashauri aanze kupunguza matumizi ya serikali yasiokuwa na tija mfano matumizi ya magari aina ya V8 ,matumizi ya bunge kwa kufuta wabunge waote wa viti maalum na pua kupungiza allowance zao ,Mikopo ya elimu ya juu utolewe kwa wanafunzi wanasoma masomo yq sayansi tu na si vinginevyo,zoezi la kurasimisha ardhi lifanyike hadi vijijini.
Apunguze na misafara ya viongozi wa kiserikali itangazwe na marufuku ya kuhama vyama tuna incur costs kubwa kweli kwenye chaguzi ndogo, toa wabunge wa viti maalumu wote.
 
Kumekuwepo na taarifa kuwa eti tumenyimwa misaada na nchi za jumuiya ya Ulaya, Marekani, na sehemu zingine.

Sababu kuu inayotajwa ni kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini chini ya huu utawala wa Rais John Pombe Joseph ‘Jiwe’ Magufuli [huyu ngosha ana majina mengi kweli...mara Tingatinga...sijui Sizonje....but I digress].

Nachotaka kuzungumzia hapa si hayo madai ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu. Hiyo ni hoja ya siku ingine.

Hapa nataka kuzungumzia huu upumbavu wa misaada.

Kwa tunaofahamiana humu tokea 2004/2005/ 2006/ na 2007, watakuwa wanakumbuka msimamo wangu kuhusu hii misaada ya maendeleo ambayo taifa letu limekuwa likipewa tokea nianze kupata/ kupatwa na fahamu.

Kwa maneno mengine, ni muda mrefu mno sasa tumekuwa tukipewa hii misaada ya maendeleo.

Kilicho cha ajabu kwangu ni: mbona bado tu hatuendelei? Hiyo si inaitwa misaada ya maendeleo? Miongo na miongo tunapokea hiyo misaada lakini ukiangalia maendeleo yenyewe hakuna.

Mbaya zaidi, tuna idadi kubwa tu ya watu [kwa makadirio yangu] ambao wanaipenda sana hii misaada ya maendeleo. Yaani wanapenda sana sisi kupewa hii misaada na hizo nchi.

Sasa ngoja nirudie ambacho nimekuwa nikikisema miaka yote hii ya uwepo wangu hapa JF na huko kwingineko.

Siipendi hii misaada. Siitaki kabisa. Naamini imetulemaza sana hadi kufikia hatua ya kudhani bila kupewa hiyo misaada basi hatutoweza kuendelea.

Naamini kabisa tunaweza kuendelea kiuchumi bila hata hiyo misaada isiyo na msaada wowote. Ni kiasi cha kuamua tu na kubadili mindset yetu kutoka kwenye ‘can’t do’ kwenda kwenye ‘can do’.

Tuna hali ya kujiona hatuwezi kufanya mambo flani flani bila ya kusaidiwa na flani. Mara zote huwa najiuliza, hivi hao wanaotupa hiyo misaada, wao nani aliwasaidia?

Na sizungumzii misaada ya hapa na pale wakati wa majanga ya kiasili, vita, au mazingira fanani. Kwa kawaida binadamu huwa tunapitia changamoto na hatuna budi kusaidiana saidiana pale inapobidi.

Hapa nazungumzia hii misaada isiyoisha ambayo huitwa misaada ya maendeleo.

Siitaki. Siipendi. Naichukia kwa hisia kali sana. Na nasema watunyime tu hiyo misaada ili tuamke toka kwenye huu utegemezi wa kipumbavu tulionao.

Bila hiyo misaada yao tutaangamia au?

Gonga ‘Like’ kama unakubaliana nami.
Ngabu usikate tawi ulilokalia hau wazungu ndio wamekupakata huko uliko!
 
Back
Top Bottom