We unataka tukubali ujinga? Warumi ndo wapingaji wa kanisa la Kristo, warumi ndo waliuwa mitume wa Kristo, warumi ndo walipotoa mafundisho ya biblia wakatunga ya kwao, warumi ndo waliingiza sherehe za kirumi na kuzipa utukufu wa kristo ili zikubalike. Wapi umeona neno KRISMAS? Andiko gani?
Ewe unayefahamu lakini kwa kusudi la kupotoa mafundisho ya Kristo na wewe unaamua kupotosha ili hali unajua na unaelewa. Inatakiwa uelewa huo sasa umgeukie Kristo, uache kujilisha upepo na mafundisho ya warumi yaliyo maagizo ya wanadamu.Ewe mpotevu uliyeacha mafundisho ya Kristu utatangatanga mpaka lini? Au ni dhambi ya kuasi na kujaribu kulishinda kanisa la Kristu ndiyo inakutesa? Kanisa ni Moja,Kanisa ni takatifu,Kanisa ni katoliki(limeenea ulimwenguni) Kanisa ni la mitume.
KANISA NI MOJA TU LILILOANZISHWA NA KRISTU
Kuna wakati ni vizuri tukaelezana ukweli bila kujali nani atakubaliana nao. Nataka nieleze kidogo jinsi Yesu alivyoanzisha Ukristo(kwasasa nitumie neno hili) na baadhi ya alama zinazotambua kazi hii ya Kristo na tuone kama alianzisha Kanisa au Makanisa.
1) UTEUZI WA MITUME 12
Yesu aliteua mitume 12 ambao walikuwa wakimwita Mwalimu (rabi) na kwenye maandiko mengi wakiitwa wanafunzi wake. Hawa walimfuata kote alikokwenda na kusikia kila alichofundisha. Kulikuwa na makundi makubwa ya watu kote alikokwenda lakini kwa miaka yote aliyohubiri alikuwa na wanafunzi wake.
Wakati Yesu akiteua Mitume tunaona jinsi alivyokuwa akiteua kila mmoja kwa sifa zake huku akiongozwa na Roho. Mfano uteuzi wa Petro tunaona Yesu alikwishajua huyo ndiye atakayekuja kuwa kiongozi wa Mitume yeye akiondoka duniani ndio maana alimtambua alipomwana na kumbadili jina ambalo baadae anakuja kufafanua wakati akimsimika Petro kama mkuu wa Kanisa Mathayo 1;42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, ``Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa(tafsiri yake Petro au Jiwe).''
Uteuzi wa mitume 12 ni kusimika utawala ambapo tunaona kabla ya kuondoka akiwapa maagizo ya kufanya na kuwapa mamlaka kamili ili walijenge Kanisa lake. Tunaona kwenye matendo ya Mitume kuwa mitume walipiga kura kuchagua mtu wa kuziba nafasi ya Yuda ili idadi ile iliyokusudiwa na Kristo kama msingi wa Kanisa iwe pale pale.
2) KUMTEUA PETRO KUWA KIONGOZI WA MITUME
Hapa ni moja ya sehemu tunapotofautiana wakristo wengi. Yesu alimteua Petro kuwa askofu wa kwanza wa kanisa. Tunaona toka Yesu alipomwona tu Petro alimbadili jina na kumuita Kefa yaani Jiwe alafu baadae Yesu anakuja kutamka hili kwa Petro (si Mitume wote bali specifically Petro) Mathayo 16;18-19 “Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
Lakini kabla Yesu hajampa mamlaka hayo Petro tunaona akimhoji Petro mara kadhaa kama msisitizo wa jukumu jipya analotaka kumtwisha (Yohana 21;15-17) Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu.
Maandiko yanathibitisha Yesu alimkabidhi Petro uongozi wa Kanisa baada yake yeye aliyekuwa kiongozi kuondoka, hii ni dhahiri aliona umuhimu wa kuchagua kabisa kiongozi miongoni mwao.
3) YESU ALIANZISHA KANISA SI MAKANISA
Tunaona Yesu alianzisha Kanisa na kuweka mitume 12 huku Petro akisimikwa kama kiongozi wao. Hii maana yake Yesu alianzisha Kanisa lenye utawala rasmi na pia kusema hata milango ya kuzimu haitalishinda, kwahiyo sifa moja muhimu ya Kanisa la Kristo lazima liwe na mtiririko wa kiutawala unaoanzia kwa Petro hadi leo maana Kristo alisema halitakufa. Lakini pia Yesu alisema atalijenga Kanisa lake na hakusema nitajenga makanisa yangu. Leo tuna makanisa mengi ingawa wote tunakiri Kristo lakini ni makanisa si Kanisa maana ili liwe Kanisa lazima liwe moja chini ya kiongozi mmoja ambaye mamlaka yake unaweza kujua jinsi alivyopata kuanzia kwa Petro hadi leo. Wengi kutafuta shortcut watasema kiongozi wao ni Kristo lakini wanasahau huyo Kristo hakuliacha Kanisa bila utawala rasmi ambao haukufa Petro alivyokufa bali upo hadi leo. Hivyo hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha Kanisa maana kazi hiyo alishaifanya Kristo miaka 2000 iliyopita, tunachopaswa kufanya ni kujua Kanisa hilo ni lipi hadi leo?
4) YESU ALITOA MAMLAKA KWA KANISA
Tunaona Yesu akiwapa maagizo mitume kwenye mambo mengi lakini ahadi kubwa juu yao ni kuachiwa msaidizi atakaye waongoza kwenye kweli yote Yohana 14;26 “Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”
Hivyo Kristo alitupa dira ya kumtegemea Roho Mtakatifu kutuongoza katika kweli. Lakini tunaona baadae Kanisa lilivyokuwa likizidi kukua changamoto za kuibuka watu na kufundisha wanayotaka na uzushi mbalimbali zikafanya Kanisa lione umuhimu wa kukusanya maandiko matakatifu na kuyaweka pamoja na kuwa sehemu ya msingi wa Imani. Hivyo Kanisa (si makanisa) ndio msingi wa ukweli maana ukweli hufunuliwa na Kanisa kwa msaada wa Roho Mtakatifu ndio maana hiyo Biblia unayotumia ni Kanisa liliamua nyaraka zipi ziwekwe, injili zipi ziwekwe, mpangilio uweje, kutoa majina ya waandishi wa injili kupitia Council of Hippo mwaka 393 ndio tunaona kazi hii ikifanywa rasmi.
HITIMISHO,
Hivyo kwa ujumla tunaona Kristo alianzisha “visible” church na hakuanzisha Makanisa ndio maana kwa mfano hatusemi makanisa ya Katoliki bali Kanisa Katoliki. Kwa neema ya Mungu na upendo wake usio na kipimo kwa watu wake, Roho Mtakatifu anatenda kazi hata nje ya Kanisa Katoliki lakini ukweli wa Kanisa kuwa MOJA tu haufutiki na wakristo wengine ni vyema mkajua hilo.
Mchungaji yeyote halali mbele za Mungu LAZIMA uzi wake, mamlaka yake tukiyafuatilia yarudi hadi kwa Mitume. Ndio maana wachungaji wa baadhi ya Makanisa mamlaka yao kichungaji yanakubalika wakiwemo Walutheri, Aglikana n.k sababu wamepokea mamlaka kutoka kwa watumishi waliokuwa wachungaji wa Kanisa Katoliki ambalo ndio pekee lenye mtiririko wa kimamlaka unaoweza kufatiliwa hadi kwa Petro na Mitume.
Si sahihi kukaa kwa mtumishi usiyejua alipakwa mafuta na nani kama sehemu ya kwanza muhimu kabla hujaangalia mengine kujua kama upo sehemu sahihi. Usifate miujiza na mafundisho yanakuvutia tu maana Yesu mwenyewe alisema watakuja walimu na manabii wa uongo na hakusema watakuja wachache alisema watakuja WENGI na kama haitoshi akasema watadanganya WENGI na si kudanganya wachache.
Alilolianzisha yeye karne ya kwanza, 33BC. Linaitwa Kanisa La Kristo.Kanisa la Mungu ndio lupi Mkuu!??
Maadam wanaendeleza mila na desturi za kirumi, hawapaswi kuitwa watumishi wa Kristo bali watumishi wa Rumi. Fahamu hiloJohn the baptist, nadhani tubaki na Utanzania ambao ni unatuunganisha kuliko kufuata misingi ya namna ya kuendesha ibaada.
Uaskofu ni wito wa kumhubiri Yesu Kristo ambae ni Bwana na mwokozi wa wanadamu. Namna ya kuendesha ibaada in mapokeo toka Vatcana au kwingineko. Kama umewahi kumsikia Martin Luther King mchungaji na activist, hakuna na mfumo wa kuzungumza kwa culture ya Vatcana, yet content yake kwenye injili ya Yesu au utetezi wa haki za binadamu haukuwa na "ustaarabu wa Vatcana". Kama umskikiza Jesse Jackson, huwezi kumlinganisha na Ruachi au Pengo.
Yet, wote ni watumishi na tuwaheshimu kwa mwito wao wa kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
Tuwaacheni watumishi watumikie mwito wa Mungu maishani mwao, maadamu wapo kwenye muktadha wa kuhubiri upendo wa Kristo kwenye maisha ya watu.
Nani kakudanganya kuwa Petro alikuwa papa wakwanza? Huo ni uongo na hakuna andiko linalosema hivyo.Hapana.Mafundisho yanafundisha kuwa papa si mwakilishi wa Mungu duniani bali ni Khaifa wa mtume Petro.
Mathayo 8:13
Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Petro ndiye aliyekabidhiwa mamlaka hayo kutoka kwa Kristu Yesu mwenyewe ili kuliongoza kanisa lake.Petro amekabidhiwa funguo za mamlaka anaweza kufunga na kufungua jambo duniani na mbinguni ikawa hivyo.Baada ya Petro ambaye ndiye papa wa kwanza kabisa na kiongozi wa kanisa la Yesu kanisa limeendeleza utaratibu wa kiti cha Petro ili kuchunga na kulinda kondoo wa bwana.
Yn 21:15-25
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
Sote tu mashahidi juu ya kazi kubwa ya kitume inayofanywa na papa dunia nzima katika kumtangaza Kristu na kuhubiri ujumbe wake.Mfano Papa Yohane Paulo II alizunguka nchi nyingi sana duniani na kote alipofika alitangaza na kuhubiri ujumbe wa Yesu kuhusu amani.Papa ni mpatanishi na msuluhishi wa migogoro mingi iliyo na inayotokea duniani.Kazi hizi ni ishara wazi kuwa yeye amekabidhiwa mamlaka na msalaba kama alivyokabidhiwa Petro katika kuendelea kuchunga kondoo wa Bwana.
Na wewe nionyeshe andiko lisilosema hivyoNani kakudanganya kuwa Petro alikuwa papa wakwanza? Huo ni uongo na hakuna andiko linalosema hivyo.
Sina la kusema mkuu. Anaewaita ni Mungu alie juu, kwa kumtumikia kwa kufuata desturi za Vatcana au kwingineko,sina la kusema kabisa.Maadam wanaendeleza mila na desturi za kirumi, hawapaswi kuitwa watumishi wa Kristo bali watumishi wa Rumi. Fahamu hilo
Juu wapi mkuu? Vatcan ni juu? Asilimia 90 ya wanaylyafanya ni maagizo ya Vatican siyo juu. Hebu sona 1Timo 3, uone sifa za wanaoyafanya ya aliye juuSina la kusema mkuu. Anaewaita ni Mungu alie juu, kwa kumtumikia kwa kufuata desturi za Vatcana au kwingineko,sina la kusema kabisa.
Ila itoshe tu kuwaheshimu kwa wao kuitikia wito wa "Alie juu"
Andiko linalosemaje? Wewe ndo ulete andiko la Petro kuitwa papa. Halipo, ila lipo linalokataza ujinga huo wa kuitana baba mtakatifu.Na wewe nionyeshe andiko lisilosema hivyo
Ndivyo mnavyojidanya mdogo wangu nilimwachia ziwa alitolewa pepo na padri bila hayo makelele yenu,kamshika kichwa kamwombea,kamwagia maji na alikuwa peke yake sisi tukiwa pembeni.Imani ya makanisa ya Kikatoliki, na makanisa yote ya kiprotestanti k.v Lutheran, Anglikana, Moravian, Menonite, nk ni makanisa yanayomwabudu Mungu kwa kuishia kwenye nafsi. Nafsi ya mwanadamu imeundwa na components kuu tatu UTASHI, AKILI, na HISIA. Ibada zao zote huwa hazivuki hapa na kuingia rohoni.
Ibada zao zimekaa kiakili-akili, na kihekima-hekima tu,,. Ndio maana utakuta mtu anaitwa askofu mkuu ila hawezi kukemea viumbe vya rohoni kama mapepo/majini, ... kwa sababu roho hizi chafu hukemewa kwa namna ya rohoni.
Ninapoyasema haya sio kwamba ninamsapoti Gwajima, ila lipo Kanisa la kweli (sio Gwajima, na sio Katoliki). Ukitaka kulijua nitafute.
Jesus is Lord .
Uache utapeli wako mkuu. Wapi imeandikwa Peter ni Papa wa Kwanza? Wapi Petro alikabidhi huduma mtu mmoja na kumpa uongozi? Hivi nyie mnasoma biblia kweli?Hapana.Mafundisho yanafundisha kuwa papa si mwakilishi wa Mungu duniani bali ni Khaifa wa mtume Petro.
Mathayo 8:13
Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Petro ndiye aliyekabidhiwa mamlaka hayo kutoka kwa Kristu Yesu mwenyewe ili kuliongoza kanisa lake.Petro amekabidhiwa funguo za mamlaka anaweza kufunga na kufungua jambo duniani na mbinguni ikawa hivyo.Baada ya Petro ambaye ndiye papa wa kwanza kabisa na kiongozi wa kanisa la Yesu kanisa limeendeleza utaratibu wa kiti cha Petro ili kuchunga na kulinda kondoo wa bwana.
Yn 21:15-25
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
Sote tu mashahidi juu ya kazi kubwa ya kitume inayofanywa na papa dunia nzima katika kumtangaza Kristu na kuhubiri ujumbe wake.Mfano Papa Yohane Paulo II alizunguka nchi nyingi sana duniani na kote alipofika alitangaza na kuhubiri ujumbe wa Yesu kuhusu amani.Papa ni mpatanishi na msuluhishi wa migogoro mingi iliyo na inayotokea duniani.Kazi hizi ni ishara wazi kuwa yeye amekabidhiwa mamlaka na msalaba kama alivyokabidhiwa Petro katika kuendelea kuchunga kondoo wa Bwana.
Kwa misingi ya biblia, kuna mengi mazuri wanayofanya japo kwa kupungukiwa sifa ya kuwa wanandoa naomba nisitie neno hapa.Juu wapi mkuu? Vatcan ni juu? Asilimia 90 ya wanaylyafanya ni maagizo ya Vatican siyo juu. Hebu sona 1Timo 3, uone sifa za wanaoyafanya ya aliye juu
Logic ipo ila hakupaswa kuleta wakati huu..No logic.
Waliohoji maamuzi ya Vatican, siyo watawa tena. Mfanl Fr Nkwera hata huyu mwandishi Privatus Karugendo. Alihoji anakuwaje Padre ilo hali hana ndoa, leo anaendelea na ndoa yake japo ukatoliki bado umemzingira. Askofu Slaa aligundua hilo akajisalimisha kwa Mshumbusi lkn ukatoliki wa kufuata maagizo ya Vatican bado umemzinga.Kwa misingi ya biblia, kuna mengi mazuri wanayofanya japo kwa kupungukiwa sifa ya kuwa wanandoa naomba nisitie neno hapa.
Ila itoshe kusema, "Yule mama aliekamatwa na mafarisayo akizini wakitaka apigwe mawe, Yesu hakumtia hukumuni japo alijua ametenda dhambi.
Principle aliyoitoa ni nenda usitende dhambi tena.
Kwa kuwa wajua wana nakisi ya kukidhi utimilifu wa maandiko, nikushauri uwatafute na kuwasaidie waijue kweli yote kibiblia na sio kufuata maelekezo ya Vatcana pekee.
NonsenseNa wewe nionyeshe andiko lisilosema hivyo
,,,najaribu kufikilia paroko anavyokemea pepo kwa upole
"Toka pepoooo uende zakooo"