Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Anglican haina tofauti sana na Katoliki!
Ki asili walikuwa wamoja, mfalme wa ungereza king Henry viii, alipooa mke wa pili ndo wakatengana. Nyote ni kundi la waasi. Mnafundishana uongo tu. Na warumi mliwaita ni wa Protestants, means kuna vitu walipinga toka kanisa la roma
 
Mkuu usifananishe Maaskofu wa kweli na mhuni na tapeli Gwajiboy. Huyo kawapata wajinga wake anaendelea kuwatapeli.
Kwanza wote matapeli.

Lkn ukitafta nani mwenye nafuu, bora hata Gwajima, angalau yeye kuna vitu anajitahidi kuvifuata japo hajakidhi, ndio maana namwita ni tapeli lkn wa kanisa katoliki ni matapeli zaidi yake .

Mtu kuwa askofu, soma hapa

1timothy 3:1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.
2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;

Hao wazinzinz wa roman, wamekuwa ma askofu kwa neno gani? Askofu gani wa romani hana watoto?
 
Kanisa katoliki ni kanisa makini katika nyanja zote na kwa umakini wake waumini wake wananufaika sana kwa kupata mafunzo ya kiimani kutoka kwa viongozi makini.Jambo linalosaidia sana kuiimarisha imani za waumini wakatoliki ulimwenguni pote!
Umakini katika kupofusha watu sawa.
Umakini katika kuwafunga watu na kuwapeleka kuzimu
Umakini katika mambo ya mwilu

Hapo nakubali 100%
 
Uko sahihi kanisa katoliki liko systematic na makini japo najua kuna watu watapinga kwasababu ndio kazi yao hiyo.
We unataka tukubali ujinga? Warumi ndo wapingaji wa kanisa la Kristo, warumi ndo waliuwa mitume wa Kristo, warumi ndo walipotoa mafundisho ya biblia wakatunga ya kwao, warumi ndo waliingiza sherehe za kirumi na kuzipa utukufu wa kristo ili zikubalike. Wapi umeona neno KRISMAS? Andiko gani?
 
Kuanzia uvaaji, nidhamu ya ibada hadi swala la kuzingatia muda maaskofu wa Katoliki wako vizuri.

Nimesikiliza mahubiri ya mhashamu baba askofu Ngalale Kumtwa hayakuwa na mbwembwe wala malalamishi bali yalijaa busara, hekima na upendo.

Kiukweli ipo tofauti ya kutosha kabisa baina ya maaskofu wa haya makanisa rasmi na wale wa Huduma za kiroho.

Nawatakia Dominica yenye baraka!

Mada inavutia lakini umekosa hoja madhubuti kuitetea. Kwa namna ilivyo hapo ni kuleta tu ubishani wa Yanga na Simba. Suala ambalo si busara.Ungeeleza kwa kina bila ya ushabiki , uoneshe udhaifu na ubora kwa kila eneo katika tukio kama hilo. Ukitaka mijadala hii, jifunze kujenga hoja.
 
Acha ubishi,huwezi linganisha Katoliki na hao wacheza porn kina Gwajima.
Papa aliwahi kuomba radhi kwa ajili ya watawa yaani askofu na ma padre waliokuwa wakifira na kubaka watoto. Nikupe link?
 
Lazima wawe tofauti kama walitotofautiana madhehenu lakini wote wameitwa kutumika kwenye shamba moja..Kuna vyakula vingi..vingine vina sukari vingine vichungu vingine vinawasha ila vyote vyahitajika kwa afya yako...usikomae na chakula cha aina moja....
Hakuna shamba moja, kuna mashamba mengi lkn ilitakiwa kuwa shamba moja. Soma 1kor 1:10-13
 
Ulitaka wafanane? Umeshatofautisha huduma zao sasa unataka wafanane vipi? Au umevutiwa na kanzu na lugha ya upole? Unataka hao wengine watoe pepo kwa kubembeleza? Hata Yesu hakufanya hivyo. Ni mitazamo tu.
Yesu alifanyaje?
 
Ewe mu roman-katoliki, pole sana kwa kudanganywa na kuwa sehemu ya mafundisho ya uongo ya kanisa lenu la kirumi.

1. Kanisa rasmi kwa kutumia maneno yako, haliwezi kuwa kanisa lenu la kirumi, wala la kiingereza~Anglican wala la wajerumani~Lutheran, wala lolote unalolifaham lililoundwa kwa vikao vya wanadam waliokaa na kuamua namna gani wamwabudu Mungu, bali kanisa rasmi ni KANISA LA KRISTO alilolianzisha kwa neno lake mwenyewe. Soma

Math 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

2. Imeandikwa, pia Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Kuheshimu kwa midomo ni ile hali ya kusema hbr za Kristo. Fine. Lkn huamini chochote/ au unaamini kwa sehemu kuhusu habari za Kristo. Mfano, unaamini hbr za ubatizo, lkn ubatizo gani? Hapo kwa sehemu inakutesa.

Kuabudu bure na kufundisha maagizo ya wanadamu, ni pale mnapofanya ambayo hayajaelekezwa kwenye biblia. Mmetunga taratibu zenu wenyewe za ibada na kuagiza watu wazifuate. Mfano, ubatizo wa watoto, ubatizo wa kunyunyiza, sala za maria, matumizi ya rozari, na meeengi mnayofundishana, kwenye biblia hutayaona, mmetunga wenyewe.

3. Mmiliki wa kanisa, ni Kristo mwenyewe. Alisema kanisa langu, ni moja hajawahi kusema makanisa yangu.

Kuwa mrumi, mwa anglican, mruther, mu full gospel, mu ufufuo na uzima, mu tag, fpct, batist n.k, maana yake umekubali kufuata mafundisho ya waanzilishi wa madhehebu hayo. Ndiyo maana pamoja na yote kumtaja Kristo, lkn mafundisho na aina ya ibada zao wanatofautiana. Yote hayo Mungu ameyakataza.

Soma 1kor 1:10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Hayo maswali yanawahusu ninyi na madhebu yenu. Ni sawa na kuuliza, ulibatizwa kwa jina la RC? Au Anglican alikufa kwa ajili yako? Au FPCT alikufa kwa ajili yako? Nk.

Ndugu yangu, neno linasema "...na milango ya kuzimu haitalishinda...". Pamoja na fitina za kila namna zilizofanywa na warumi-RC, kuua, kutesa, kubagua, kutweza WAKRISTO waliopokea injili kwa Kristo na waliokuwa kwenye utume kama walivyoagizwa, "... enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa, ataokoka". Fitina hizo hazikumaliza wakristo, hazikuua kanisa la Kristo, liliendelea, linaendelea na litaendelea. Hakuna milango/madhehebu yatakayo lishinda kanisa la Bwana. Yesu na kanisa lake watabaki hata kama wamezungwa na wapingaji kama nyie.

Nakualika uje ujifunze hbr za Kristo, uanze kuabudu unachokijua tena kilicho sahihi, uachane na hizo misa zilizotungwa na wanadamu. Siyo vitu vya kujivujia.
Ewe mpotevu uliyeacha mafundisho ya Kristu utatangatanga mpaka lini? Au ni dhambi ya kuasi na kujaribu kulishinda kanisa la Kristu ndiyo inakutesa? Kanisa ni Moja,Kanisa ni takatifu,Kanisa ni katoliki(limeenea ulimwenguni) Kanisa ni la mitume.

KANISA NI MOJA TU LILILOANZISHWA NA KRISTU

Kuna wakati ni vizuri tukaelezana ukweli bila kujali nani atakubaliana nao. Nataka nieleze kidogo jinsi Yesu alivyoanzisha Ukristo(kwasasa nitumie neno hili) na baadhi ya alama zinazotambua kazi hii ya Kristo na tuone kama alianzisha Kanisa au Makanisa.

1) UTEUZI WA MITUME 12

Yesu aliteua mitume 12 ambao walikuwa wakimwita Mwalimu (rabi) na kwenye maandiko mengi wakiitwa wanafunzi wake. Hawa walimfuata kote alikokwenda na kusikia kila alichofundisha. Kulikuwa na makundi makubwa ya watu kote alikokwenda lakini kwa miaka yote aliyohubiri alikuwa na wanafunzi wake.

Wakati Yesu akiteua Mitume tunaona jinsi alivyokuwa akiteua kila mmoja kwa sifa zake huku akiongozwa na Roho. Mfano uteuzi wa Petro tunaona Yesu alikwishajua huyo ndiye atakayekuja kuwa kiongozi wa Mitume yeye akiondoka duniani ndio maana alimtambua alipomwana na kumbadili jina ambalo baadae anakuja kufafanua wakati akimsimika Petro kama mkuu wa Kanisa Mathayo 1;42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, ``Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa(tafsiri yake Petro au Jiwe).''

Uteuzi wa mitume 12 ni kusimika utawala ambapo tunaona kabla ya kuondoka akiwapa maagizo ya kufanya na kuwapa mamlaka kamili ili walijenge Kanisa lake. Tunaona kwenye matendo ya Mitume kuwa mitume walipiga kura kuchagua mtu wa kuziba nafasi ya Yuda ili idadi ile iliyokusudiwa na Kristo kama msingi wa Kanisa iwe pale pale.

2) KUMTEUA PETRO KUWA KIONGOZI WA MITUME

Hapa ni moja ya sehemu tunapotofautiana wakristo wengi. Yesu alimteua Petro kuwa askofu wa kwanza wa kanisa. Tunaona toka Yesu alipomwona tu Petro alimbadili jina na kumuita Kefa yaani Jiwe alafu baadae Yesu anakuja kutamka hili kwa Petro (si Mitume wote bali specifically Petro) Mathayo 16;18-19 “Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

Lakini kabla Yesu hajampa mamlaka hayo Petro tunaona akimhoji Petro mara kadhaa kama msisitizo wa jukumu jipya analotaka kumtwisha (Yohana 21;15-17) Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu.

Maandiko yanathibitisha Yesu alimkabidhi Petro uongozi wa Kanisa baada yake yeye aliyekuwa kiongozi kuondoka, hii ni dhahiri aliona umuhimu wa kuchagua kabisa kiongozi miongoni mwao.

3) YESU ALIANZISHA KANISA SI MAKANISA

Tunaona Yesu alianzisha Kanisa na kuweka mitume 12 huku Petro akisimikwa kama kiongozi wao. Hii maana yake Yesu alianzisha Kanisa lenye utawala rasmi na pia kusema hata milango ya kuzimu haitalishinda, kwahiyo sifa moja muhimu ya Kanisa la Kristo lazima liwe na mtiririko wa kiutawala unaoanzia kwa Petro hadi leo maana Kristo alisema halitakufa. Lakini pia Yesu alisema atalijenga Kanisa lake na hakusema nitajenga makanisa yangu. Leo tuna makanisa mengi ingawa wote tunakiri Kristo lakini ni makanisa si Kanisa maana ili liwe Kanisa lazima liwe moja chini ya kiongozi mmoja ambaye mamlaka yake unaweza kujua jinsi alivyopata kuanzia kwa Petro hadi leo. Wengi kutafuta shortcut watasema kiongozi wao ni Kristo lakini wanasahau huyo Kristo hakuliacha Kanisa bila utawala rasmi ambao haukufa Petro alivyokufa bali upo hadi leo. Hivyo hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha Kanisa maana kazi hiyo alishaifanya Kristo miaka 2000 iliyopita, tunachopaswa kufanya ni kujua Kanisa hilo ni lipi hadi leo?

4) YESU ALITOA MAMLAKA KWA KANISA

Tunaona Yesu akiwapa maagizo mitume kwenye mambo mengi lakini ahadi kubwa juu yao ni kuachiwa msaidizi atakaye waongoza kwenye kweli yote Yohana 14;26 “Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Hivyo Kristo alitupa dira ya kumtegemea Roho Mtakatifu kutuongoza katika kweli. Lakini tunaona baadae Kanisa lilivyokuwa likizidi kukua changamoto za kuibuka watu na kufundisha wanayotaka na uzushi mbalimbali zikafanya Kanisa lione umuhimu wa kukusanya maandiko matakatifu na kuyaweka pamoja na kuwa sehemu ya msingi wa Imani. Hivyo Kanisa (si makanisa) ndio msingi wa ukweli maana ukweli hufunuliwa na Kanisa kwa msaada wa Roho Mtakatifu ndio maana hiyo Biblia unayotumia ni Kanisa liliamua nyaraka zipi ziwekwe, injili zipi ziwekwe, mpangilio uweje, kutoa majina ya waandishi wa injili kupitia Council of Hippo mwaka 393 ndio tunaona kazi hii ikifanywa rasmi.

HITIMISHO,

Hivyo kwa ujumla tunaona Kristo alianzisha “visible” church na hakuanzisha Makanisa ndio maana kwa mfano hatusemi makanisa ya Katoliki bali Kanisa Katoliki. Kwa neema ya Mungu na upendo wake usio na kipimo kwa watu wake, Roho Mtakatifu anatenda kazi hata nje ya Kanisa Katoliki lakini ukweli wa Kanisa kuwa MOJA tu haufutiki na wakristo wengine ni vyema mkajua hilo.

Mchungaji yeyote halali mbele za Mungu LAZIMA uzi wake, mamlaka yake tukiyafuatilia yarudi hadi kwa Mitume. Ndio maana wachungaji wa baadhi ya Makanisa mamlaka yao kichungaji yanakubalika wakiwemo Walutheri, Aglikana n.k sababu wamepokea mamlaka kutoka kwa watumishi waliokuwa wachungaji wa Kanisa Katoliki ambalo ndio pekee lenye mtiririko wa kimamlaka unaoweza kufatiliwa hadi kwa Petro na Mitume.

Si sahihi kukaa kwa mtumishi usiyejua alipakwa mafuta na nani kama sehemu ya kwanza muhimu kabla hujaangalia mengine kujua kama upo sehemu sahihi. Usifate miujiza na mafundisho yanakuvutia tu maana Yesu mwenyewe alisema watakuja walimu na manabii wa uongo na hakusema watakuja wachache alisema watakuja WENGI na kama haitoshi akasema watadanganya WENGI na si kudanganya wachache.
 
Kasome biblia uimalize yote ukianza kuhubiri hutohubiri kwa kuwabembeleza watu, utahubiri kwa nguvu zote tena kwa sauti kubwa. usije ukadhani wanapenda kuhubiri vile yule ni Roho mtakatifu akisha jaa unajikuta unahubiri kwa nguvu.
Jaribu kutofautisha Mihemuko na uwepo wa Roho Mtakatifu. Kwa Roho Mtakatifu hakuna mihemuko. Usiukoee heshima utatu Mtakatifu kwa kuufananisha na mihemuko ya akina Gwajima na wenzie
 
Papa aliwahi kuomba radhi kwa ajili ya watawa yaani askofu na ma padre waliokuwa wakifira na kubaka watoto. Nikupe link?
Yesu alisema ukipigwa kofi upande mmoja,geuza upande wa pili.Inasikitisha kuona mtu ujiitaye mkristu hujui maana ya kuomba msamaha.Hii ni ishara ya unyenyekevu na kujishusha.Kanisa halitojali kama ni kweli au si kweli juu ya matukio hayo na wala halikuhoji bali liliiga mfano wa Yesu wa kujishusha na kujinyenyekeza kwa kuomba msamaha.
 
Mimi ni muislam niliye mfuasi mzuri wa DINI yangu, Ila kiukweli huwa nasuuzika sana kila jumapili ninapofuatilia misa za kanisa katoliki kupitia televisheni.Leo nilifarijika Sana kumuona askofu Ngalalekumtwa akitutuliza na kutujaza hisia za ukweli kabisa.
Nisieleweke vibaya kuwa hao waliotajwa hawana maana laa laa Ila nimeacha tu kuwafuatilia kwenye televisheni km nilivyoacha kabisa kuwafuatilia ndugu zetu Answaar Sunna a.k.a Wahabi na pia Sina maana nawadharau Answaar Sunna hapana.

Peace

Rip BWM
hao sunna ndo wale wanaovaa surali fupi?
 
Mmemwacha Kristo na kufundishana mambo mnayoyajua. Tubuni mkaiamini injili
Injili hiyo mnayoiamini iliandikwa kwa mikono ya watu wakiongozwa na roho mtakatifu.Kanisa ndilo lina vitabu vyote original vya biblia na hata hivyo mnavyovitumia vimeandikwa na kanisa kwa muongozo wa roho mtakatifu.
Kanisa lina sehemu mbili
1: Maandiko matakatifu
2:Mapokeo matakatifu

Yote hufanyika kwa uongozi wa roho mtakatifu
 
Kuanzia uvaaji, nidhamu ya ibada hadi swala la kuzingatia muda maaskofu wa Katoliki wako vizuri.

Nimesikiliza mahubiri ya mhashamu baba askofu Ngalale Kumtwa hayakuwa na mbwembwe wala malalamishi bali yalijaa busara, hekima na upendo.

Kiukweli ipo tofauti ya kutosha kabisa baina ya maaskofu wa haya makanisa rasmi na wale wa Huduma za kiroho.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Ndio umejua leo kwani na hao wengine huwa unawaita maaskofu pia! Ha ha ha kuhusu muda ndio hawana kabisa kwani ibada yao kuisha ni mpaka mate yaishe mdomoni inabidi mtu unaenda kanisani umekula ugali kabisa kwani hujui mtarudi saa ngapi
 
Haijalishi wewe sijui dhehebu gani umetoka wapi kikubwa kinachoitajika ni kuishi katika neno LA Mungu kuchukua mafundisho na kuyaishi Yale mafundisho dhehebu halikupeleki mbinguni "unaweza kuta njia zipo nyingi sana lakini wote tunaelekea sehemu mmoja " kikubwa kuishi katika neno LA Mungu tu hayo mengine ni mbwembwe tu
 
Injili hiyo mnayoiamini iliandikwa kwa mikono ya watu wakiongozwa na roho mtakatifu.Kanisa ndilo lina vitabu vyote original vya biblia na hata hivyo mnavyovitumia vimeandikwa na kanisa kwa muongozo wa roho mtakatifu.
Kanisa lina sehemu mbili
1: Maandiko matakatifu
2:Mapokeo matakatifu

Yote hufanyika kwa uongozi wa roho mtakatifu
Mapokeo ni maagizo ya wanadam, jidanganye eti kuna kanisa katoliki, hilo ni dhehebu wapingaji wa kanisa la Mungu
 
Kuanzia uvaaji, nidhamu ya ibada hadi swala la kuzingatia muda maaskofu wa Katoliki wako vizuri.

Nimesikiliza mahubiri ya mhashamu baba askofu Ngalale Kumtwa hayakuwa na mbwembwe wala malalamishi bali yalijaa busara, hekima na upendo.

Kiukweli ipo tofauti ya kutosha kabisa baina ya maaskofu wa haya makanisa rasmi na wale wa Huduma za kiroho.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
John the baptist, nadhani tubaki na Utanzania ambao ni unatuunganisha kuliko kufuata misingi ya namna ya kuendesha ibaada.

Uaskofu ni wito wa kumhubiri Yesu Kristo ambae ni Bwana na mwokozi wa wanadamu. Namna ya kuendesha ibaada in mapokeo toka Vatcana au kwingineko. Kama umewahi kumsikia Martin Luther King mchungaji na activist, hakuna na mfumo wa kuzungumza kwa culture ya Vatcana, yet content yake kwenye injili ya Yesu au utetezi wa haki za binadamu haukuwa na "ustaarabu wa Vatcana". Kama umskikiza Jesse Jackson, huwezi kumlinganisha na Ruachi au Pengo.

Yet, wote ni watumishi na tuwaheshimu kwa mwito wao wa kuhubiri injili ya Yesu Kristo.

Tuwaacheni watumishi watumikie mwito wa Mungu maishani mwao, maadamu wapo kwenye muktadha wa kuhubiri upendo wa Kristo kwenye maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom