MIMI WEWE NDIO MIMI(shairi)

MIMI WEWE NDIO MIMI(shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1)hakuna tena umimi,kwenye dunia ya sasa.
Umoja ndio ukumi,kwa kizazi cha kisasa.
Kila wa roho ya ami,atajaliwa na kasa.
Ataponzwa na ulimi,kwa kutamani lumbesa.
Kama wewe ndio mimi,basi mimi ndio wewe.

2)kama mimi siyo mimi,katu swezi kujijua.
Akili kwangu uchumi,nitaulinda na jua.
Lenye muale wa ndimi,kwako sije kuungua.
Kwa kuwa wewe ni mimi,mimi nae twakujua.
Kama wewe ndio mimi,basi mimi ndie wewe.

3)mili yetu tofauti,ila twa roho mmoja.
U kama shingo na uti,vilo ungana pamoja.
Kwa jambo la tofauti,na kuepusha viroja.
Jali kupiga saluti,roho nafsi kwa pamoja.
Kama mimi ndie wewe,basi wewe ndie mimi.
4)kama wajijua wewe,utanijua na mimi.
Kama u wewe kiwewe,unahitaji alimu.
Elimu iso ka jiwe,fupa la kunyonya sumu.
Hata liwe la nguruwe,binafsi usilaumu.
Kama mimi ndie wewe,basi wewe ndie mimi..
5)babu yako a mzawa,uliwahi muuliza.
Kama sisi tu u ziwa,au ujawahi waza.
Kama ungelitunziwa,vipi ungejikereza.
Haya uliuliziwa,japo wewe makengeza.
Kama wewe ndie mimi,basi mimi ndie wewe.
6)nahisi kama nalewa,vile nikikutazama.
Ila kweli najelewa,kama naona twazama.
Naona hujaelewa,mboni nikikutazama.
Nani wa kukulelea,umekufa ku mzima.
Kama wewe ndio mimi,basi mimi ndio wewe.
Shairi:WEWE MIMI NDIO MIMI.
Mtunzu:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.
 
Back
Top Bottom