Kwangu mimi huyu ndio mzamiaji mwenye roho ngumu kinoma, wengine wanangoja

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu zangu mwaka 2005 mwishoni, mimi na madogo fulani wawili wa mtaani tulikuwa safarini tukielekea Kaburu. Mimi nikiwa kiongozi wa safari, tuliamua kupitia njia ya Malawi ambayo ndio nilikuwa na uzoefu nayo. Safari yetu ilianza vizuri, kila mmoja akiwa na chake mfukoni.

Tulipofika katika border ya Malawi na Msumbiji "dedza", mmoja wetu aligundua kwamba amepoteza pesa njiani (hatujui alipotezaje potezaje), kwahiyo ikawa ngumu kuruhusiwa kupita pale mpakani maana hakuwa na hela za kuonesha kama "Pocket Money". Kutokana na uzoefu wang wa safari hasa kwa njia ile ikabidi nimfanyie mandingo kwa upande wa Msumbiji. Nilimtafuta kijana mwenye baiskeli ambao wengi wao hufanya kazi ya kuwavusha watu kwa njia za panya, nikampanga fresh akakubali na kwenda kumvusha yule dogo. Mpaka hapo tayari ilikuwa ishakuwa jioni na border zote zilikuwa zimefungwa. Yule jamaa wa baiskeli akatupeleka kwao tukaoga tukala, ilipofika saa 1:30 ya usiku akatupeleka sehemu fulani ambapo kuna mabasi yanapita hapo kuelekea katika mji fulani mdogo ambao nimeusahau jina lake.

Tulipofika katika ule mji mdogo hapo tayari ilikuwa ishafika saa 5.30 usiku, ikatubidi tutafute nyumba ya kulala wageni tukalala.

Asubuhi na mapema tukaelekea katika stand kuu ya hapo mjini, ambapo kuna vi aisi mbali mbali vya kuelekea maeneo mbali mbali ya nchi. Sisi tukapanda ya kuelekea "Tete" (kwa wale waliowahi kupitia njia hii bila shaka wanaufahamu huu mji ambao ukiutazamana ni kama mwambasa vile) Basi safari ikaanza nikiwa na wale madogo wawili, kwa pamoja hatukumtupa mwenzetu, bali tulishirikiana kumsaidia, ilimradi na yeye afike salama. Baada ya kutembea kwa muda mrefu ndani ya gari, hatimae tulifika katika lile daraja linalogawa upande wa tete na huku tulipotoka. Ni daraja refu kweli kweli, na kabla ya kuvuka daraja lile huwa kuna migration wanaikagua watu ndani ya magari. Wakijua kwamba wewe sio raia na hauna vibali vya kukuruhusu kuwa nchini kwao, basi unabaki, at least utoe chochote ili wakuachie.

Dogo kuona vile akaanza kuchachawa akijua sasa ana baki pale darajani ( ikumbukwe dogo hakuwa na visa ya kuingia msumbiji, aliingia tu kwa njia za panya kupitia baiskeli) Mimi nikamtuliza nikamwambia dogo kaza roho usiogope sana, maana itakuwa rahisi kukugundua na ikitokea wamekuotea mimi nitaongea na dereva amalizane nao. Kweli bwana kama zali yule migration kachungulia chungulia akasema nendeni, tukavuka hadi upande wa pili wa Tete.

Kufika tete tukajielekeza hadi kunako kituo cha mabasi yanayotoka tete kuelekea maeneno mengine pia ya nchi kama vile Maputo nk. Kwa bahati mbaya sisi kufika pale tukakuta gari iliyokuwepo imeshajaa, kwahiyo tusubiri gari nyingine. Na pale gari ili ijae ilikuwa inachukua siku 5 hadi wiki ( kwa waliopitia njia ile miaka ile nafikiri wanafahamu) Kwa vile lengo letu ni kufika tunapoelekea basi hatukuwa na jinsi zaidi ya kusubiri. Bahati nzuri maeneo yale kuna msikiti ambao ulikuwa unasaidia watu wenye matatizo mbali mbali. Ukijua kuongea unapewa hata sehem ya kulala katika vyumba vya nje ambavyo vilitumiwa kama madrasa.

Sisi tukaomba msaada wa kulala, ila kula mara nyingi tulikuwa tunajinunulia chakula chetu wenyewe. Siku ya kwanza ikapita, ya pili, ya tatu, ya nne tukiwa tunakwenda pale stand kuangalia ujazo wa lile basi, ghafla tukakumbana na mbongo mmoja pale stand. Jamaa kutuona akatufuata na kujitambulisha kwetu huku akiongea kwa lafudhi ya kimtwara mtwara. Mara ya kwanza nilitaka kumpuuza, kwa sababu mimi nawajua ndugu zetu wakiwa safarini, wengine wanakuwa hawana mioyo kabisa. Unaweza kujipa muda wa kumsikiliza, na nyinyi mkaongea ya kwenu, kumbe mwenzenu "mchoraji wa ramani za watu", mwisho wa siku anawaletea polisi mnakamatwa.

So nilipuuza puuza ila baadae nikaja kugundua kuwa jamaa ni msafiri kweli, sio mchora ramani kama nilivyofikiria. Afu pia na yeye ashaishi Kaburu kabla ya kurudishwa bongo kutokana na biashara ya mazabe. Jamaa akawa anatuomba msaada, dah tukijicheki mfukoni sisi wenyewe hatujui hatima yetu huko mbele, maana tayari mmoja wetu hana chochote mfukoni kwake, sisi ndio tegemezi wake. So tukisema tuanze kuongeza mungine wa kumsaidia huenda tukafika sehem tuka stuck wote kwa pamoja bila wa kumsaidia mwenzake. Ikabidi tumueleze jamaa kuwa sisi wenyew tunaunga unga tu safarini. Ila nikamwambia jamaa kuhusu swala la misosi tunaweza kuwa tunakula pamoja, akakubali.

Sasa siku ya 5 yake asubuhi na mapema ndio ilikuwa tuondoke, jamaa akanifata akanambia mwamba mimi ni lazima niondoke na basi hili, nikamwambia utaondokaje na ww hauna nauli, akasema yeye ataenda chini ya lile basi kuna tairi la rizevu limewekwa, kwahiyo atajichimbia chini ya lile tairi hadi Maputo. Fikiria wakati ule gari ilikuwa inatumia siku mbili njiani ili kufika huko Maputo, na barabara maeneo mengi ilikuwa mbovu kweli kweli plus na mvua zilikuwa zinanyesha sana kipindi hicho. Kwangu nilijua utani, lkn siku na saa ilipofika jamaa akajichimbia chini ya tairi, safari ikaanza huku mimi tu na wale madogo ndo tuliokuwa tunajua kinachoendelea huko chini ya basi. Yani ilikuwa mnaanza safari kama vile leo j'mosi saa kumi asubuhi na mnafika keshokutwa j'3 saa 4 au 5 asubuhi.

Safari ikaanza tukawa tukifika sehem ya watu kuchimba dawa, naangalia noma afu naenda kwa nyuma ya basi nachungulia na kumpenyezea jamaa msosi kiaina. Na kama ni mida ya usiku namshtua jamaa anatoka kwa nje kidogo maeneo ya giza giza anapata hewa. Cha kushangaza sisi tuliokuwa ndani ya gari kwa kutwa moja tu tayari tulikuwa tumeshachoka balaa, sasa yeye alie chini ya tairi si ndo ilikuwa balaa. Jiulize zile siku mbili njiani wakati gari ikichanja mbuge usiku alikuwa analalaje? Mvua inanyesha, barabara madimbwi kibao, gari inalala upande wa kushoto, inarudi tena upande wa kulia mithili ya gari iliyojaza magunia ya mkaa. Mpaka tumekuja kufika katika kijiji fulani ambacho ni kilometers kadhaa tu kufika Maputo, nakumbuka ilikuwa asubuhi hiyo, ikabidi nimpelekee jamaa kidumu cha maji safi ili anawe uso na kusukutua, jamaa akafanya hivyo na baadae akachomoka. Nilikuwa na nguo kadhaa nikampa suruali 1 na tshirt ili hata akiwa anazunguka zunguka pale watu wasimhisi chochote. Mpaka hapo jamaa alikuwa ashatabanika sana, nguo zake utafikiri alimezwa na mamba afu akacheuliwa. Tulikaa pale kwa muda wa saa 1, ilikuwa ni kwenye sheli, baada ya hapo safari ikaanza tena ya kuelekea Maputo, msela akajitupa tena chimbo.

Baada ya masaa kadhaa tukawa tumefika Maputo, yeye akasema kwamba kwa pale tayari ashafika maana ana wana wengi sana maeneo yale. Sisi hatukutaka kuuweka usiku, nikachukua gari hadi kwa wale wazee wa kuvusha watu. Kufika pale tukaungana na wengine waliokuwepo pale. Mida ya usiku safari ikaanza ya mguu kwa mguu, ilituchukua kama masaa 9 hivi kwa mguu ili kuingia Kaburu. Yule mwamba tukawa tumepoteana nae pale Maputo. Sasa siku moja nikiwa Pretoria maeneo ya Marabastad nikamuona msela, sema nilikuwa kwenye gari afu nina haraka, so sikuweza kushuka kumfata niongee nae. Ila ki ukweli nilitaka kwenda nimpongeze jamaa kwa ujasiri wake wa safari. Maana ile ilikuwa haina tofauti na mbinu ya kijeshi anapoingia eneo la adui kupitia gari ya kambi. Dah hivi ni nani aliwahi kupitia changamoto hizi safarini? Kama ni wewe au una mtu unaemfahamu karibu utupe ushuhuda wako.

Asanteni.
 
Wangekuwa wengine wangeweka vituo vingi na kusema itaendelea
 
Tete nilipita 2017 dah aisee watu wanasafiri maana nilikuta nyomi ya watu pale stand mpk nikajiuliza hii nchi ina tatizo gani watu wanaondoka hv dah kumbe ni mkusanyiko watu kota sehem tofaut wengi wamalawi wanaenda kufanya kazi mashambani South, ntarudi tena South kupitia boda ya Namibia maana hiyo ya malawi to Maputo hapana aiseee
 
Nilienda kijiji kimoja hivi kwa ajili ya kilimo, basi bana mwenyeji wangu akanambia kuna jamaa ameachiwa nyumba usiku nitalala akirudi. Nilivotoka shamba ile najitambulisha jamaa akanikataa. Kulalek, nilienda kulalala kwenye kibanda flani iv kilichowah kutumiwa na wakulima kama miaka miwili nyuma. Humo ndani sijui kuna nyoka, nge au fisi.

Jaman maisha haya ni achaneni nayo kabisa.
 
Back
Top Bottom