MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 15,891
- 40,166
- Thread starter
- #61
Una hoja, lakini mtu akisimamishwa nafasi yake haiwezi kujazwa anayeshika nafasi hiyo anakua amekaimishwa.Mi ntatofautiana na wewe kidogo mkuu.
Nataka nikuulize: je tuhuma hizo zikithibitishwa atastahili mjadala gani mwingine ili kuendelea kumsafisha?
Kiongozi yeyote wa kijamii hatakiwi kunyooshewa kidole kwa kashifa ya namna yoyote ile.
Utamaduni wa uwajibikaji hapa Tz sasa umeanza kuonekana kama dhambi na ndiyo maana hata viongozi wa kitaifa wanapoingia kwene tuhuma za kashifa kubwa hawataki kuwajibika kwa madai mepesi kama haya ya 'ushahidi wa tuhuma'!
Unamtetea Walidi pekee, mbona sijakusikia kuwatetea wale wengine wawili waliotumbuliwa naye?
Je wao walithibitishwa tuhuma zao ndiyo wakatumbuliwa?
Tumeshaona na kusikia namna viongozi wa dini zote wakikumbwa na kashifa za kingono, ukatili pamoja na ubadhirifu wa rasilimali.
Je bashasha za kwenye mimbari na muonekano wa mtu, ndizo zinatosha kumpi maatendo yake ya sirini?
Mkuu, mbona suala hili mnalivalia sana njuga kama lile la Heche wa Cdm, kuna nini nyuma ya pazia?
Kwa jinsi taarifa zilivyo ni kwamba nafasi imejazwa maana yake hukumu imekwishapitishwa.
Kama nilivyosema hapo awali, mimi siyo Muislamu na wala sina elimu ya dini ya Kiislamu, ila misingi ya haki ni universal