Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.

OA.
 
Kijuujuu unaweza ukafikiri tatizo la huyo dokta na mkewe ni interest tofauti.Naomba nikupe undani
wa hili tatizo lililokumba ndoa ya dokta.Hiki kisa cha dstv kilitokea mwaka 2006.
Dokta alimweleza mkewe kwamba tamthiliya za Mambo Hayo na Tausi zilishaisha zamani hazipo tena.Mkewe
hakuamini, aliona mume anamyima raha makusudi.Mke akanyamaza lakini rohoniakahifadhi cheche ya hasira iliyolipuka na kuvunja ndoa mwaka 2008 mume alipomnunulia simu.

Kwa sababu ya uelewa mdogo wa mambo, kila akimpigia mumewe simu akaambiwa na mitambo yenye sauti ya kike:"Namba unayopiga kwa sasa haipatikani kwa sasa, jaribu baadaye" mke anafikiri sauti ni ya hawara wa mumewe!
Mume akirudi nyumbani mke analianzisha, mume anamfahamisha juu ya hiyo sauti inakotoka, mke anang'ang'ania msimamo na uelewa wake.

Mwishowe waliachana oktoba 2013 baada ya vikao vyingi vya usuluhishi kushindikana.

Daktari yu mbioni anatafuta mke.
Acha ku- GENERALIZE tabia za Wanawake wengi tokana na Mwanamke m1 tu.

Fanya utafiti kisha njoo na majibu hapa uone ni asilimia ngapi ya wanawake wasio na elimu ya juu sana hawajadumu na wamedumu katika ndoa zao kwa muda mrefu tena kwa amani.
 
Kwenye mapenzi Elimu haina nafasi wewe oa tu kama unampenda kwa dhati.
 
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.


Nawasilisha.
Darasa la saba la wapi mkuu? maana darasa la saba wa mjini ni form six
 
Mkuu kama anakupenda na unampenda fungeni hizo pingu tu .
 
Mkuu mwanamke kwanza kazi yake ni kuangalia watoto nyumbani na kumtunza mumewe hakuna kumpeleka shule muhimu anajua baya na zuri hiyo inamtosha.tulia baadae umfungulie mradi wake wakumuweka busy maisha yaendelee.

Kuowa mwanamke asiyesoma sana kuna raha sana hasa ukute anajitambua,hii dunia utajiona kama wewe ndo mwanaume kushinda wote.
Kweli kabisa!
 
Hahah hatukutarajia mkuu ila tulilipokea kama Neema ya Mungu. Kwa nini hushauri kumsomesha? Matarajio yangu aje asimamie biashara mbalimbali tutakazo anzisha, sasa inatakiwa kidogo hata ooh yes yaan Kingeee na mahesabu na kutunza kumbukumbu awe anajua kwa kiasi cha kutosha.
Ngoja ujue kingereza tabu zianze! Muache ivoivo atakuheshm milele! Ukianza kumtoa tongotongo atajiona na yy Ana PhD!
 
Nina sista amemaliza shahada ya sheria pale UDSM mume wake darasa la saba A,anabanda lake anagonga nyundo na kupiga msasa.

Watu walisema weweweweeeeee,ahhhg wapi wanalisongesha life lao toka kitambo.
 
Nina sista amemaliza shahada ya sheria pale UDSM mume wake darasa la saba A,anabanda lake anagonga nyundo na kupiga msasa.

Watu walisema weweweweeeeee,ahhhg wapi wanalisongesha life lao toka kitambo.

hatari sana. Huyo jamaa mpiga msasa atakua analishwa sana matango pori
 
Mkuu, Uzi wako umenipa nguvu ya kuoa form 4 wangu maskini, maana nilikuwa najiuliza sana juu ya chaguo langu."hivi ni kweli ndo naenda kuoa huyu mwanamke, mbona kama hatufanani?" nikimaanisha kielimu..! mie nna kadigrii kangu yeye form 4 leaver...hata kazi hana ukiondoa kumsaidia mama ake kuuza duka la vipodozi....na kinachoniumiza kichwa zaidi kuona rafiki zangu wengi wa karibu wameoa wake ambao ni wasomi wenzao..wengine tayr hao wake zao wakiwa na kazi zao na wengine bado wanapambana kutafuta ajira...but wana degree zao mkononi.

Nikimfikiria huyu wangu wakati mwengine nachoka kabisa..maana mawazo wakati mwngine yanafika mbali kbs,najiuliza kwa mfano akikutana na wake wa marafiki zangu hatojisikia vibaya? kuona wenzake wana elimu ya kutosha hlf yeye ndo hivo tena...najiuliza hata stori zao zitaendana kweli?

Ila nimeamua kuoa tu maana nishamtia tamaa sana na sio yeye tu hadi mama yake na baadhi ya ndugu zake wa karibu..nikimuacha kwa kigezo cha elimu nahisi si sababu madhubuti na Mungu anaweza hata kunipa mtihani katika maisha yangu ya ndoa kwa hao wengine.coz huyu mtoto hana shida she is cool, heshima,mapenzi na hana tamaa...sio omba omba wa hela,mpk wakati.mwengine najisikiaga aibu naamua kumgaia hata kama hajaomba...na tena anashukuru hata ukimpa buku 5 anaona nyingi...cjui huko mbele itakuaje naomba Mungu asibadilishe tabia na fikra zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Elimu na IQ kwanza tuanze na hilo, Ukiwa kama msomi mwenye Elimu ya kiwango cha Masters haukupaswa kujiuliza hili swali. nadhani kuna kitu Watanzania tunatakiwa kukitambua kuwa akili ya kawaida ndio huvumbua mambo mengi duniani na sio ya kufundishwa darasani. Mfano Genius wote duniani wamevumbua vitu ambavyo havimukuwepo duniani na kwa maana hiyo ili ugundue kitu ni lazima kisiwepo duniani wewe ule wa kwanza kukitambulisha ndio maana halisi ya ugunduzi. "Note" Kuwa na mwanamke ambaye amesoma au hajasoma kabisa sio kipimo mahusiano na maendeleo ya maisha au malezi ya familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom