Mimi nimechagua kuwa mtoto wa mama

Mimi nimechagua kuwa mtoto wa mama

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,333
Reaction score
20,763
Kuwa mtoto wa mama kuna raha sana,

Hivi unajua mama anavyodekeza eeh hasa kwa watoto wake sasa imagine unakuwa mtoto wa mama yaani ni full kudeka, ukiwa mtoto wa mama mtoto wa jirani akikufinya tu ukiita ma... hata ujamaliza kupiga kelele mama huyu hapa kashafika,

Ukiwa mtoto wa mama hata ukiwa mwizi, kibaka mzoefu mama atakutetea bwana na atakusema kimyakimya nyumbani tena chumbani, kuwa mtoto wa mama ni raha sana.

Baba nilikupenda ila ukauzu wako hapana.. ona sasa haupo umeshageuka nyota upo juu mawinguni sisi huku tunatumbua ulivyochuma ingawa ukauzu wako ulinifunza nikomae na maisha kwenye mazigira yoyote yale na nitafute vya halali nisipende vya bure sitakusahau

Baba ulitulisha maharage na mlenda ili tujenge jumba la ghorofa na kweli ulilijenga ingawa hukulipaka rangi ila tunajisifu na sisi mtaani tuna jumba la ghorofa,

Wasiwasi wangu kwa mama ni kuwa je zikiisha pesa alizotafuta baba itakuwaje maana mama yeye umwambii kitu kuhusu sisi watoto wake yupo teyari kutupa chochote tutakacho hata kama gharama zake ni kubwaaa.

Mimi ni hayo tu kwa leo acha niende mama ameshaniita acha nikadeke mie.🤓
 
No
kuwa mtoto wa mama kuna raha sana,
hivi unajua mama anavyodekeza eeh hasa kwa watoto wake sasa imagine unakuwa mtoto wa mama yaani ni full kudeka, ukiwa mtoto wa mama mtoto wa jirani akikufinya tu ukiita ma... hata ujamaliza kupiga kelele mama huyu hapa kashafika,

ukiwa mtoto wa mama hata ukiwa mwizi, kibaka mzoefu mama atakutetea bwana na atakusema kimyakimya nyumbani tena chumbani, kuwa mtoto wa mama ni raha sana.
baba nilikupenda ila ukauzu wako hapana.. ona sasa haupo umeshageuka nyota upo juu mawinguni sisi huku tunatumbua ulivyochuma ingawa ukauzu wako ulinifunza nikomae na maisha kwenye mazigira yoyote yale na nitafute vya halali nisipende vya bure sitakusahau,
baba ulitulisha maharage na mlenda ili tujenge jumba la ghorofa na kweli ulilijenga ingawa hukulipaka rangi ila tunajisifu na sisi mtaani tuna jumba la ghorofa,

wasiwasi wangu kwa mama ni kuwa je zikiisha pesa alizotafuta baba itakuwaje maana mama yeye umwambii kitu kuhusu sisi watoto wake yupo teyari kutupa chochote tutakacho hata kama gharama zake ni kubwaaa.

mimi ni hayo tu kwa leo acha niende mama ameshaniita acha nikadeke mie.🤓
Not chawa wa mama kweli? 🤣🤣🤣
 
Dekeni Sana ila rasilimali za Tanganyika ni kwa ajili ya watanganyika.
 
Msimchanye Mother, Mother yuko kwenye mstari sahihi. Mama mtu wa haki, acha agawe ugali kwa kipimo sawa sawa ili sote tuonje hata finyango mojamoja inatosha. Mama wewe ndiyo mlezi wa familia. Komaa hivyohivyo usisikilize maneno ya watu. Hii nyumba yetu sote kila mtu apate sawa. Uchungu wa mwana aujuae mama.
 
Back
Top Bottom