Mimi ni mwanahisa wa CRDB, sijapata gawio hadi leo

Huwa sina hulka ya kubishana, nachofanya ni kuonesha faida iliyopo kwa crdb tofauti na nmb ila kwa kuwa umeamua kuset mind yako kwamba nakushawishi ununue crdb basi nunua nmb ili uwe against na mimi then utakua umeshinda.
Hesabu ziko wazi kwa wanaotaka kuelewa! Ahsante kwa ufafanuzi!
 
Mkuu samahani unasema kama mtu akiweka 1M gawio anaweza pata 50000 au 93000 hii ni kwa mwaka au mwezi?

Kama ni kwa mwaka acha tu niendelee kuuza vocha maana kwa mwaka nitakuwa na faida kubwa kuliko 50000 au 93000.
Hiyo 1M inatosha kabisa kununua baiskeli 10. Ikikodisha watu, hiyo 50,000 no ndani ya siku tatu mpaka tano afu mtu anaisubilia mwaka
 
Tatizo mjadala umevamiwa na wabangaizaji na sio wawekezaji.

Msinielewe vibaya.

Kuwekeza mtaji ni uwezo. Sasa una mtaji wa vitumbua unataka kuwekeza kwenye vipande vya benki wapi na wapi? Utakufa njaa.

Kuza mtaji kisha sasa sogea kwenye hii mada.
 
Kiutendaji CRDB ipo vizuri zaidi ya NMB by FAR!!

Usipende namba bila kupenda hesabu
Hisa moja ya NMB ni Tsh 2,400 kwa gawio la tsh 127 ni sawa na 5% (ROI) Ungekua umewekeza 1M faida ni 50k
Hisa moja ya CRDB ni Tsh 235 kwa gawio la tsh 22 ni sawa na 9.3% (ROI) Ungekua umewekeza 1M faida ni 93k

Nadhani nimeeleweka vizuri hapo. ikiwa unahitaji kuwekeza kimbia CRDB, NMB userekali mwingi bila hivyo hata faida wanayoipata isingekuepo.
Upo vizuri kweli Mc Ras Paroko nilikuwa natafuta mda mrefu jinsi ya kupiga hesabu za kutafuta Gawio kutokana na thaman ya Hisa ulizonazo
 
Hesabu ziko wazi kwa wanaotaka kuelewa! Ahsante kwa ufafanuzi!
Kwa hiyo apa Kiongozi kwa hesabu izi kwa Mwanahisa atakae wekeza let's say milioni Kumi (10M) bank ya crdb atapa Gawio la sh. 930,000/= ?? Na Kama akiwekeza milioni Mia (100M) atapata Gawio la sh.9,300,000/= si ndio ivyo au ??
 
Kwa hiyo apa Kiongozi kwa hesabu izi kwa Mwanahisa atakae wekeza let's say milioni Kumi (10M) bank ya crdb atapa Gawio la sh. 930,000/= ?? Na Kama akiwekeza milioni Mia (100M) atapata Gawio la sh.9,300,000/= si ndio ivyo au ??
Ili kujua gawio gawanya mtaji kwa bei ya hisa zidisha kwa gawio kwa hisa: 10,000,000/430x36=837,209
Less .05 kodi!!
 
Na pia kuna faida ya capital gain,na ndio msingi hasa wa Ku trade stocks. Mf CRDB mwaka Jana hisa moja ilisoma 230 sasa ivi ni 430 ..
Angalia capital gain ni ngap,zidisha mara idadi ya hisa zako

Hisa inaweza kupanda au kushuka thamani.
Capital gain ni pale tu hisa inapoongezeka thamani per share..
Iwapo hisa itashuka thamani per share, kutakuwa na Capital Loss.
 
Kama akili zako zimefika mwisho kabisa wa kufikiri ndio usumbuane na mambo ya hisa za mabank
 
Back
Top Bottom