Mimi ni mwana CHADEMA nnaeishangaa CHADEMA

kaka changamka hyo nafasi chukuwa na toa mwanga kwa wenzio .sio lazma msubiri m2 atoke dodoma kwenye ccm awapangie.nyie iteni kikao then mchague uongoz wenu,
 
Unajua ukizoea spoonfeending matatizo yake ndio haya. Sasa kama mwanachadema unakaa pembeni na kuanzakunyooshea vidole wwengine na ww kujiondoa basi haufai kuwa mwanachadema. Wanchadema siku zote ni wachapa kazi na wabunifu. Hapo ndipo pa kuthibitisha kuwa ww ni kamanda wa cdm. Komaaa mkuu.

sasa ulitaka afanye nini? Si ndio mchango wake huo tayari na ndio maana ameamua kuja humu na kusema, badala ya kukaa kimya? Na wahusika kama ni wakusikia watasikia na kuchukua hatua, kwa nini unamshambulia kosa lake nini?

 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro.

Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii.

KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPA

Fanya mawasiliano ya haraka na Antony Komu (diwani) ama umcheki John Mrema anaweza kukusaidia. Kama uko tayari nikuPM namba za hao makamanda.
Aluta Continua!
 
Si wakati wa kushangaa. Chukua hatua "Mabadiliko yanaanza na wewe kama ukitimiza wajibu wako" Acha kulalamika.
 
nashukuru kwa ushauri wenu likini nimeshindwa kuelewa unapomwambia mtu kama wewe ni mwanacchama chukua nafasi inashangaza yaani wanachama wanijipa uongozi wenyewe au huchaguliwa au kuteuliwa na viongozi wa juu? halafu mtu anapokuambia wasiliana na kiongozi wa juu au wa mkoa kwa kukutajia jina unapataje mawasiliano yake au mnafikiri kila mtu anajua jinsi ya kuwasiliana na kiongozi?au tuwekeeni namba za viongozi wa mikoa yote wazi halafu muone kama kuna mtu atakuja kulalamika humu


Mkuu wazo lako ni zuri na unastahili kupongezwa kwa kuliweka wazi. Wanaokulazimisha kuwa wewe ndio uwe kiongozi hawajui kuwa leaders are born and not made. Wanaopewaelimu elekzi na ikawafaa ni wale tu amabo talant ya uongozi wanayo tayari. Kinyume chake ni kulazimish na matokeo yake ni kuwa na wanaojifanya viongozi lakini muda wote wanaongea matusi, utumbo, mipasho na mambo mengine. Wana CDM kina Shonza, Mwambambwa, Shibuda watufunze mengi na tusiwe tayari kuendelea kuwa na watawala ambao tutawaita majina ya wasaliti au masalia. Tufanye usahili mapemana yule anayetwambia kuwa tu uchi tumsikilize.Hongera kwa kuwa muwazi na viongozi mtafute mtu wa aina hii ili tuweke mizizi huko ngazi za chini na tuweke facilities za kueneza falsafa ya mabadiliko
 
Hapa mkuu ni katika mtandao maarufu wa Jamii Forums, Hapa sio mahali pa kuwasilisha malalamiko ya wanachama wa vyama vya siasa, nakushauri uwaone viongozi wa chama chako uwaeleze haya.

Hivi nyie wanachadema mkoje? Kila Siku mnapost threads za kuilalamikia CCM humu ndani ya jamvi, au CCM sio chama cha. Siasa? Achani unafiki. Kwanza mngemshukuru mtoa mada kwamba kawaamusha ktk baadhi ya maeneo hamjafika. Pumbafu sana
 
Huu ni ushamba wa hali ya juu! Unashangaa nini kutokuwepo kiongozi wakati wewe upo na si kiongozi? Anza wewe halafu ndio ushangae wengine!!?

Acha Jazba na kumdhihaki mkuu, Muelimishe kistaarabu akuelewe. Si wote wanafikiri kwa haraka kama wewe!!!
 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro. Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii. KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPAUmeanza lini kuwa mwanachadema? Unafiki mtupu! Kama wewe ni mwanachadema na kuna mambo hayakufurahishi tumia uhuru wako wa kikatiba hamia chama kingine unachoona kinafaa.
 
Hivi nyie wanachadema mkoje? Kila Siku mnapost threads za kuilalamikia CCM humu ndani ya jamvi, au CCM sio chama cha. Siasa? Achani unafiki. Kwanza mngemshukuru mtoa mada kwamba kawaamusha ktk baadhi ya maeneo hamjafika. Pumbafu sana
Mkuu una hasira!, hadi umemalizia na "pumbafu sana" .

Hata hivyo mkuu kuna utofauti kidogo hapa, hao wanachadema(mimi sio mmoja wao)huwa wanaikosoa CCM kwa kuanika mabaya yake na wala huwa hawaombi ushauri wa nini cha kufanya juu ya udhaifu huo(kumbuka ni wana CDM kuianika CCM). Huyu yeye ni mwana CDM anaomba ushauri ni nini afanye ili kupata viongozi katika eneo lake. Nikamweleza kuwa hapa sio mahala pake unless kama yeye ni salia.
 
CHADEMA mnahitaji wanachama kama huyu aliyeanzisha hii thread, siyo hawa wachumia tumbo tuliowazoea hapa jamvini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mwanachama kama huyu asiyeweza kujenga chama kwenye eneo lake anasubiri Dr. Slaa au Mbowe afike hapo hatufai ningekuwa na uwezo ningemnyang'anya kadi ya chadema!
 
Back
Top Bottom