Mimi ni mwana CHADEMA nnaeishangaa CHADEMA

Mimi ni mwana CHADEMA nnaeishangaa CHADEMA

Let's be honest. Hivi unafikiri ni wangapi wana katiba ya chama au tayari wameishaisoma.
Hawa hawa wanaobeza na kubwabwaja kama sikosei wengi wao hawajui hata katiba ya chama ikoje achilia mbali kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki za chama.
Mkuu Kitila,

Huyu mwanachama wenu anatakiwa kuelemishwa kama ulivofanya hapa chini na sio kubezwa kama wanavyofanya wengine hapa.

Mwanachama amefanya la maana kuwakilisha tatizo walilo nalo huko kwao. Inawezekana tatizo ni matokeo ya wao wenyewe kutokuelewa mifumo ya uongozi. Lakini kwasababu ameamua kulisema tatizo lao; mimi ningetegemea CHADEMA wenye uelewo wamwelemishe huyu jamaa kwa lugha isiyo na kubeza au vijembe. Kwamba hata yeye kama ameweza kufikisha ujumbe hapa tayari ni kiongozi na awakusanye wenzake wote ili waunde uongozi hapo hapo walipo.

Uelewo wa watu wetu bado mdogo sana, sio kwenye masuala ya siasa tu bali hata kwenye masuala ya uchumi wao. Kuna fursa zingine wanazo lakini wanashindwa kuzitumia. Ni vizuri tuwe wapole na kuwaelemisha na sio kuwabeza au kuwatumia maneno makali.

Ni ushauri kwa mzee mwenzangu maana sisi wa zamani tulikuwa na hamu ya kuelemishnaa na kufundishana hapa JF.
 
CHADEMA mnahitaji wanachama kama huyu aliyeanzisha hii thread, siyo hawa wachumia tumbo tuliowazoea hapa jamvini.Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Wewe kweli ni Sumu.
 
Huu ni ushamba wa hali ya juu! Unashangaa nini kutokuwepo kiongozi wakati wewe upo na si kiongozi? Anza wewe halafu ndio ushangae wengine!!?

Si busara kumbeza huyu jamaa aliyeileta hii hoja. He has a valid point, hatuwezi kuwa na chama kinachoelea, kuna haja ya kuelekeza nguvu vijijini ili kujenga msingi imara. Huyu mtu ni mdau mzuri kwani ametoa dukuduku lake, mnapoana kum-task atafute viongoz wa ngazi za juu wakat yeye keshadeliver ujumbe hapa na wadau wengi wenye access na hao viongoz wa juu mmeuona itakuwa si vyema.

Wewe uliyeona huu ujumbe kama una nafasi ya kuwasiliana na mmoja wa viongoz wa eneo hilo au hata ngazi za juu wafahamisheni juu ya mapungufu haya, Ni kwa namna hiyo ndio tutajenga chama chetu.
 
Lakini atasemaje hawafahamu viôngozi na hajui aanzie wapi wakati amesema anamfahamu mwenyekiti wa chadema anayeitwa malboro? Ndugu, kama basil lema kumpata ni ngumu mfate huyo mwenyekiti anaweza akawa na wazo, acha kushangaa..huu ni muda wa kazi
 
Unajua ukizoea spoonfeending matatizo yake ndio haya. Sasa kama mwanachadema unakaa pembeni na kuanzakunyooshea vidole wwengine na ww kujiondoa basi haufai kuwa mwanachadema. Wanchadema siku zote ni wachapa kazi na wabunifu. Hapo ndipo pa kuthibitisha kuwa ww ni kamanda wa cdm. Komaaa mkuu.
 
Jipange wewe mwenyewe - anzisha tawi, panga safu ya uongozi, zishughulikie kero za wananchi. wewe ndio chadema. Na chadema inawategemea watu kama wewe kuweza kuwa suluhisho la matatizo ya jamii inayokuzunguka.
 
Kwa ushauri ilikuwa unatakiwa kufanya mambo yafuatayo
1. kupitia huyo mwenyekiti Dr Maliboro ambae ni mwanachama wa CDM ungekaa nae mkajaribu kupanga ni jins gan mnaweza kuanzisha tawi la CDM katka kjj chenu
2. Baada ya hapo mgeitisha mkutano wa wanachama na wale wenye nia ya kujiunga na CDM wenye agenda kuu ya kuunda tawi
3. kupitia mkutano huo mgepanga tarehe ya kikao cha chama ili kupata uongozi wa mda ambao utashughulia mikakati ya uzinduzi wa tawi lenu.
4. Baada ya kupanga mipango yenu na ikikamilika mnawaandikia barua viongozi wenu wa CDM wa ngazi ya juu yenu mkiwapa taarifa juu ya tawi lenu na kuwapa mwaliko wa uzinduzi wa tawi, kama wasipowapa hushirikiano ndo ungewatupia lawama. kumbuka kuwa kabla ya kutoa lawama juu ya tatizo fulani, lazima ujiangalie wewe umeplay part gani katka kusolve hilo tatizo maana unaweza kuwa wewe ni source ya hilo tatzo na ukaishia kulaumu
 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro.

Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii.

KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPA

Umetoa malalamiko yenye maana na ya msingi,pole sana kwani naona Miprochadema inakushambulia kama vilempira wa kona,ukiona maji yapo shingoni fanya kama walivyofanya kina shonza na Mwampamba..
 
Last edited by a moderator:
Umetoa malalamiko yenye maana na ya msingi,pole sana kwani naona Miprochadema inakushambulia kama vilempira wa kona,ukiona maji yapo shingoni fanya kama walivyofanya kina shonza na Mwampamba..

Huo ushauri ni sumu kabisa huna haja ya kuwafuata hao walotajwa hapo juu ila tuu chukua hatua na kwa uelewa wangu wanachadema mtakuwa wengi tuu kwenye hiyo kata.Tambuaneni,jiungeni na huo utakuwa mwanzo wa kuwapata viongozi mnaowahitaji.Hata kama wewe unafaa ila huwezi kujitangazia uongozi ukiwa pekeyako.

Kwa wengine hebu tutafakari ni nani viongozi wetu kwenye kata zetu? Hapa nahisi tatizo la uru lipo sehemu nyingi.Shime wana CDM!!
 
siyo moshi ...tunazungumzia kata...halafu kuna aibu gani hapa, je kunachama kilichojengwa kwa muda mfupi tu kikawa na mwakilishi kila mahali, hata Obama pamoja na mamilioni ya fedha ya kampeni kuna baadhi ya vitongoji hakufikia...lakini kwa hili la mezani, km yupo mwanachama mmoja basi ndio chama kimefika katani humo
 
CHADEMA mnahitaji wanachama
kama huyu aliyeanzisha hii thread, siyo hawa wachumia tumbo tuliowazoea
hapa jamvini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

wamemstahi kweli mana angeoga mvua ya matusi, hawatakagi kuambiwa ukweli hao..
 
Huu ni ushamba wa hali ya juu! Unashangaa nini kutokuwepo kiongozi wakati wewe upo na si kiongozi? Anza wewe halafu ndio ushangae wengine!!?
Sio kila mtu mwanasiasa bana, kuna wengine ni bora kubaki wanachama kwa sababu wanajijua kuwa siasa hawaziwezi, na sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi, tunaona matokeo ya kupewa yeyote kwasababu alikuwepo peke yake. CDM lazima mbadilike, tunaona vyeo vinavyo gaiwa kwa vingozi wale wale sasa hata viongozi wa kata mnataka kufanya hayo hayo. Mwisho mnabaki kufukuza watu hovyo.
 
siyo moshi ...tunazungumzia kata...halafu kuna aibu gani hapa, je kunachama kilichojengwa kwa muda mfupi tu kikawa na mwakilishi kila mahali, hata Obama pamoja na mamilioni ya fedha ya kampeni kuna baadhi ya vitongoji hakufikia...lakini kwa hili la mezani, km yupo mwanachama mmoja basi ndio chama kimefika katani humo
Mliweza kufika UK na kufungua tawi na kuweka vingozi wa kila aina,kilimanjaro imeshindikana, hii ni kali.
 
Siasa mtandao hizi,hujui wajibu wako kama mwanachama wa CDM? chukua kadi yako geuza upande wa pili soma kilichoandikwa kisha tekeleza.
 
CHADEMA mnahitaji wanachama kama huyu aliyeanzisha hii thread, siyo hawa wachumia tumbo tuliowazoea hapa jamvini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Huyu mwana Chadema ajiunge na magamba kwa sababu Chadema watu wanajituma; magamba zidume fikra za dhaifu
 
Teh, teh, teh!!, mkuu,
mbona akina Ritz hawaimbi nyimbo za kumsifia mbowe na slaa
hawajala ban?, Mbona kuna masalia kibao akina Shonza na wenzake
wanawatukana hao akina slaa na mbowe na wanadunda mitaani?!,
nikukumbushe tu kuwa hadi akina Nnape na Nchemba ​ni
wanachama wa mtandao huu, unamaanisha nao huwasifia mbowe na slaa?, acha
kudhalilisha watu mkuu.

mkuu Ritz kala ban tayari, MODs wangepaswa kutupa sababu
 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro.

Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii.

KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPA

Ruzuku kajikopesha Dr Silaa.... unategemea nini kitatokea !
 
Back
Top Bottom