Mimi ni mwana CHADEMA nnaeishangaa CHADEMA

Mimi ni mwana CHADEMA nnaeishangaa CHADEMA

Mkuu makesy wewe ndiyo unatushangaza makamanda wenzio, M4C bolded kwenye falsafa ya mahtma ghandi ambaye aliamin kuwa CHANGE ni mimi na wewe, Kama viongozi hakuna basi hata ww unaweza kuwa kiongozi na ukatibu ukampa hata mke wako kwan si kosa maana ktk eneo hilo hakuna viongozi , baada ya hapo ndio fanya utaratibu kuwasiliana na viongozi wa chama hapo mfano kama Basil Lema.
 
Last edited by a moderator:
Ni matumizi ya akili ndogo kumshambulia mleta mada,wengine mnadai afanye initiatives kabla ya kulaumu.Je,mnadhani kila mtu aliye CHADEMA anafaa kuwa initiator,je kila mmoja anao uwezo wa kuhamasisha na kufanya political mobilization ili kuimarisha uongozi sehemu husika? Tuache kujadili mambo kwa hisia bali kwa uhalisia.Si kila mwana CHADEMA anajimudu kiuongozi mfano mleta mada yeye ni mwanachama wa kawaida tu na mpiga kura naye anachotaka awe na viongozi katika kata yake.Tujiulize kwanza uongozi wa mkoa,wilaya hadi jimbo wamefanya jitihada gani kuhakikisha unakuwepo kila kata? Ni kujidanganya kudhani kila mwanachama ni Master Planner wa kuimarisha chama.Mtu kaleta mada kuhusu tatizo,kinachotakiwa ni ushauri na maoni juu ya nini kifanywe na uongozi wa mkoa,wilaya,jimbo na mwanachama mwenyewe ili aache kushangaa badala yake atimize wajibu kama mwanachama!
 
Kumbe wewe ni mwanachama, changamka sasa ili mtu mwingine akija kuchukua nafasi usilalamike

nashukuru kwa ushauri wenu likini nimeshindwa kuelewa unapomwambia mtu kama wewe ni mwanacchama chukua nafasi inashangaza yaani wanachama wanijipa uongozi wenyewe au huchaguliwa au kuteuliwa na viongozi wa juu? halafu mtu anapokuambia wasiliana na kiongozi wa juu au wa mkoa kwa kukutajia jina unapataje mawasiliano yake au mnafikiri kila mtu anajua jinsi ya kuwasiliana na kiongozi?au tuwekeeni namba za viongozi wa mikoa yote wazi halafu muone kama kuna mtu atakuja kulalamika humu
 
Hapa mkuu ni katika mtandao maarufu wa Jamii Forums, Hapa sio mahali pa kuwasilisha malalamiko ya wanachama wa vyama vya siasa, nakushauri uwaone viongozi wa chama chako uwaeleze haya.
Hapa ni sehemu ya kuimba nyimbo za kumsifia Mbowe na Slaa tu, vinginevyto utakula ban au sio????
 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro.

Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii.

KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPA

Mkuu usisubiri kuletewa viongozi wa kata Na chama.
We na wananchi wengine wanaopenda mabadiliko ndio viongozi. Jipangeni na mtoe taarifa kwa viongozi wenu wa ngazi ya juu watawasaidia
 
nashukuru kwa mlionisapoti nawengine mlionishauru lakini bado nataka kujua unaponishauri niwasiliane na kiongozi wa mkoa halafu badala ya kunipa namba yake ya sim unanitajia jina nitampataje?au unaponishauri kuwa kama hakuna viongozi nichukue nafasi huo ndio utaratibu wa kuwapata viongozi wetu?yaani mtu anainuka na kusema kuanzia sasa mimi ni katibu wa chama na ikawahivyo?naomba muendelee kunifungua mawazo.
 
Hapa ni sehemu ya kuimba nyimbo za kumsifia Mbowe na Slaa tu, vinginevyto utakula ban au sio????
Teh, teh, teh!!, mkuu, mbona akina Ritz hawaimbi nyimbo za kumsifia mbowe na slaa hawajala ban?, Mbona kuna masalia kibao akina Shonza na wenzake wanawatukana hao akina slaa na mbowe na wanadunda mitaani?!, nikukumbushe tu kuwa hadi akina Nnape na Nchemba ​ni wanachama wa mtandao huu, unamaanisha nao huwasifia mbowe na slaa?, acha kudhalilisha watu mkuu.
 
Mim ni mwanaCHADEMA mzuri natokea Moshi Vijijini kata ya Uru Mashariki naishangaa CHADEMA kwani huwezi kuamini pamoja na umaarufu wote huo CHADEMA haina viongozi wa chama ndani ya kata nzima ukiacha mwenyekiti wa kijiji cha Mwasi Kaskazini wanamwita Dr. Maliboro.

Ndani ya kata nzima hakuna kiongozi yeyote na ukizingatia mwaka kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa ni nani anayefanya maandalizi ya viongozi hao au mnasubiri muje na zile kampeni za zimamoto yeyote atakae jitokeza kugombea nafasi yoyote mnampa hata kama hafai halafu akishindwa mnakuja na kauli za kuibiwa kura kumbe mlisimamisha watu wasiofaa mbele ya jamii.

KAMA NIMEDANGANYA ANAEMJUA KIONGOZI YEYOTE WA CHADEMA NDANI YA KATA HII ANITAJIE HAPA

yaweza kuta lumumba imebadilishwa jina kuwa m vijijini.
 
Mpaka sasa tatizo ni wewe na si CDM na tena nawezasema wewe si mwana CHADEMA wa dhati maana kama wewe umeweza kuwa mwana CDM katika eneo lisilo na kiongozi hata mmoja wa CDM nadhani utakuwa unajua sababu na unatakiwa utumie fursa hiyo kuleta mabadiliko katika eneo lako kama kweli wewe ni CDM na sio unabaki unashangaa humu JF wakati CDM ni wewe na viongozi wako (au umekuwa mwanachama pambo
 
CHADEMA mnahitaji wanachama kama huyu aliyeanzisha hii thread, siyo hawa wachumia tumbo tuliowazoea hapa jamvini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ndugu nakuunga mkono, huyo Bwana kweli anaipenda CDMm ameona losa la chama chake na amelitakia marekebisho. Hao viongozi mkoani kwake ndio sababu ya upotofu na uzembe, kwa hivyo akiwapelelkea maoni yake si watamfukuza. WAna CDM pelekeni hili jambo kwa viongozi wenu wa taifa lifanyiwe kazi. Tanzania inahitaji chama pinzani chene nguvu
 
Ukimaliza Kushangaa hamasisha wanachama wenzako muanzishe uongozi maana hata wewe ni kiongozi, CHADEMA ni open source bwana siyo chama ch ukiritimba. kila mwanachama ni kiongozi.
tengenezeni jambo hapo ili kama usemavyo muwagalagaze hapo kama mnaangusha mlevi vile
 
Hii ni dictatorial persona kufikiria kila mtu ana fikra kama za mwingine.

Hapa ni sehemu ya kuelimishana na kusaidiana.

Kwa viongozi waandamizi wa CHADEMA ambao wanakesha hapa JF, Msaidieni na kama ikihitajika, muelimisheni kwa sababu wazo lake ni zuri mbeleni kwa uhai wa chama. Mbona zikitolewa shutuma kwa chama kuna viongozi wandamizi huwa wanakuja hapa JF kwa haraka kuzijibu au kuzitolea ufafanuzi.

Mimi nilikuwa nafikiria Kilimanjaro ni ngome ya CHADEMA kwa maana kuwa hata uongozi umejipanga sawa sawa.
 
Mkuu CHADEMA KILIMANJARO IMELALA

sasa ndugu zangu,hv mmefikia hatua ya kumlaumu kiasi ichoo mtu ambaye hajitambui?nazan mngempa ushauri tu ulikuwa unamtosha.asanteni
 
Hapa ni sehemu ya kuimba nyimbo za kumsifia Mbowe na Slaa tu, vinginevyto utakula ban au sio????

hapana,jifunze upya namna ya kufikiri kabla hujatoa majibu yakoo,uchama weka kushooto ndugu ndo mana hujitambui kama shonza na mtera.
 
Sasa kwa nini nyie msijipange mchaguene? Au mnasubiri makao makuu?
 
Mkuu Kitila,

Huyu mwanachama wenu anatakiwa kuelemishwa kama ulivofanya hapa chini na sio kubezwa kama wanavyofanya wengine hapa.

Mwanachama amefanya la maana kuwakilisha tatizo walilo nalo huko kwao. Inawezekana tatizo ni matokeo ya wao wenyewe kutokuelewa mifumo ya uongozi. Lakini kwasababu ameamua kulisema tatizo lao; mimi ningetegemea CHADEMA wenye uelewo wamwelemishe huyu jamaa kwa lugha isiyo na kubeza au vijembe. Kwamba hata yeye kama ameweza kufikisha ujumbe hapa tayari ni kiongozi na awakusanye wenzake wote ili waunde uongozi hapo hapo walipo.

Uelewo wa watu wetu bado mdogo sana, sio kwenye masuala ya siasa tu bali hata kwenye masuala ya uchumi wao. Kuna fursa zingine wanazo lakini wanashindwa kuzitumia. Ni vizuri tuwe wapole na kuwaelemisha na sio kuwabeza au kuwatumia maneno makali.

Ni ushauri kwa mzee mwenzangu maana sisi wa zamani tulikuwa na hamu ya kuelemishnaa na kufundishana hapa JF.

Sasa kwa nini nyie msijipange mchaguene? Au mnasubiri makao makuu?
 
Back
Top Bottom