Mimi ni mvivu kweli, naombeni ushauri

Mimi ni mvivu kweli, naombeni ushauri

Duh!usiombe ukaishi na mtu mvivu utajuta mana kila kitu anakutegea ufanye wewe.
Jitahidi hata kwakujilazimisha kufanya kazi zako na kuzimaliza.
Mfano kama weekend ukiamka fanya zote uzimalize usipumzike mana hapo ndo unakaribisha uvivu.
Ila uvivu ni tabia tu ya mtu anakua nayo ila hajijui.
Nina mdogo wangu toka yupo mdogo ni mvivu hatari.Yeye ulikuwa unaweza kumpa kazi ukija kustuka unakuta mwenzio alishalala zamani na hata akiamka hataifanya tena hiyo KAZI.
Amekua lakini tabia ni ileile yaani kazi ndogo tu lakini atajivuta mpaka basi.
 
Wadau nina shida moja katika maisha yangu. Mimi ni mvivu halafu huwa natake easy kila kitu, kitu ambacho kinanisababishia hasara nyingi maishani.

Kuhusu darasani nina akili za kutosha toka primary top ten ilikuwa hainikosi hata chuo sikuwahi kupata supp, hata kuna wakati somo moja lililamba robo tatu ya darasa, tena nilikuwa nimelazwa, nikatoka hospitali asubuhi nikaingia saa tisa kwenye paper nikapata zangu B. Niliosoma nao humu wanaweza kunikumbuka.

Sasa tatizo linakuja kwenye maisha, mimi ni mvivu. Kuamka nitashtuka tu saa kumi na moja najiongeza kidogo kidogo hadi inafika saa moja najiandaa kivivuvivu hivo hivo. Mara nivae nguo hii mara nione sijapendeza nivue hadi saa mbili natoka nduki kwenda job maana sio mbali, kwahiyo hapo naacha chumba kikiwa rafu maana muda wa kupanga na kutandika kitanda unakuwa hamna hadi nirudi jioni.

Nikialikwa kwenye party najiandaa kivivu hadi wakati mwingine naacha tu maana muda unakuwa hamna tena sherehe imeisha.

Nikienda benk sihesabu hela, jana nimeibiwa elf 10 duka la kubadilishia fedha maana sikuhesabu, kwenye daladala nilipewa hela feki hivi hivi maana hata sikuangalia.

Naombeni ushauri nifanyeje maana mimi mtu mzima nahitaji kuwa na familia na kuwa mama bora. Ndio maana nilitamani kuadopt mtoto ili niwe busy nae, haya maisha ya kuishi peke yangu yananilemaza jamani nifanyeje?

Natamani kuwa active. Hapa nimeandika hivi nimechoka kweli yaani.
Sisi kikwetu huu tunaita ni uvivu wa kushindwa hata kujikuna!
 
1. Una umri gani?
2. Ulilelewa na wazazi wako au na bibi?
3. Chuo ulisoma CBE AU IFM?
 
Hero yako mm mvivu had dushelele siwez kushika kukojoa wala kulengesha kunako utamu....yan ni mvivuuuuu
 
Uvivu unaendana na uchafu na mtu akiwa mvivu lazima atakuwa mchafu
Hakuna mtu anaeweza kukubadilisha usiwe mvivu isipokuwa wewe mwenyewe kuamua mimi sitaki uvivu na sitaki uchafu
Na uvivu kwa mwanamke si kitu kidogo trust me usichukulie poa pengine ushakucost au utakucost hapo mbeleni
 
Nadhani tatizo kubwa hapo ni mtazamo wako (mindset), wanasema "you are what you think you are". Ukijiaminisha ww ni mlegevu na mvivu utakuwa hivyo, kisaikilojia matendo yataakisi.

Hebu jikubali kuwa ww ni mtu jasiri na unae_jiamini pia jali muda wako, kumbuka ukishapita haurudi nyuma. Ukijiwekea falsafa ya kwenda na muda utajikuta unafanya mambo kwa wakati. Vilevile uvivu ni sifa mbaya.
 
Anza kwenda Gym na punguza vyakula vya sukari na fastfoods. Hutaamini.
 
Back
Top Bottom