Mimi ni kijana wa miaka 20 nahitaji ushauri wa wa kazi nayoweza kufanya kulingana na elimu yangu

Luteni Mkuu

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
328
297
Wakuu nawasilisha kama kichwa kinavyojieleza nahitaji mnipe ushauri kama mdau wenu. Nilifeli kidato cha nne mwaka 2018 mpaka sasa hivi nipo nipo tu sina cha kufanya naishi na wazazi wangu wote bila kumsahau dada na kaka yangu ambae anasoma chuo hapo UDOM.

Mara zote nimekuwa nikiisaidia familia yetu chochote nitakachokipata kutokana na mzee hana kazi ya uhakika nimeona nije kwenu kama kuna anaeweza kuniorodheshea kazi zote ninazoweza fanya bila kuhitaji mtaji wowote.

Wakuu msaada tafadhali maana hali inazidi kuwa ngumu kwa upande wangu nipo njia panda sijui nifanye kipi niache kipi.
 
Wakuu nawasilisha kama kichwa kinavyojieleza nahitaji mnipe ushauri kama mdau wenu.nilifeli kidato cha nne mwaka 2018 mpaka sasahivi nipo nipo tu sina cha kufanya naishi na wazazi wangu wote bila kumsahau dada na kaka yangu ambae anasoma chuo hapo UDOM...
Ndoto na kiu yako ndiyo itakufikisha unakotaka kwenda, Kuna kijana nimekuwa nikiwasiliana Naye toka mwaka jana mwezi wa Saba sijawahi kukutana Naye ila nimehandle miamala yake Sana, Ana trade forex, Bitcoin anauza vitu Shopify Yuko mwanza, Mimi akili yangu ilikuwa inanituma kuwa atakuwa 30+ kwanza ukizingatia kaoa ndoa ya mkeka mwaka huu.

Jana ndiyo kwa Mara ya kwanza tumepiga story za maisha nikashangaa dogo Ana miaka 22, mkewe Ana miaka 18 na Wana mtoto.
Dogo hakumaliza advance alikosa karo akiwa form 5, Sasa ndiye anawasomesha wadogo zake na kuwatunza wazazi wake, ni trader mzuri Sana wa FX Ana vitu bingo anafanya mpaka nlishangaa kwa umri wake na ambitions zake haviendani maana kipindi Nina umri huo nilikuwa Sina mawazo ya maana.

Anampenda Sana Ontario eti anasema anamtazama yeye. Dogo kwa week hakosi kupiga transaction za 500$ kwa issue anazofanya.
Yani nachotaka kusema kila mtu haijalishi kaishia wapi ametokea wapi akiwa una kiu na utayari wa kujifunza chochote na kufanya lolote unaweza japo Safari uwa siyo rahisi.

Huyo dogo toka Jana nimeanza kumzingatia kwa picha nyngne akija fika 30s atakuwa mbali nadhani.
 
Wakuu nawasilisha kama kichwa kinavyojieleza nahitaji mnipe ushauri kama mdau wenu.nilifeli kidato cha nne mwaka 2018 mpaka sasahivi nipo nipo tu sina cha kufanya naishi na wazazi wangu wote bila kumsahau dada na kaka yangu ambae anasoma chuo hapo UDOM.mara zote nimekuwa nikiisaidia familia yetu chochote nitakachokipata kutokana na mzee hana kazi ya uhakika nimeona nije kwenu kama kuna anaeweza kuniorodheshea kazi zote ninazoweza fanya bila kuhitaji mtaji wowote wakuu msaada tafadhali maana hali inazidi kuwa ngumu kwa upande wangu nipo njia panda sijui nifanye kipi niache kipi.

Pole sana kwa changamoto unayopitia.

Kazi ambazo hazihitaji mtaji ni kutumia nguvu zako mf Saidia fundi,kwenye viwanda etc
 
Ndoto na kiu yako ndiyo itakufikisha unakotaka kwenda, Kuna kijana nimekuwa nikiwasiliana Naye toka mwaka jana mwezi wa Saba sijawahi kukutana Naye ila nimehandle muamala yake Sana, Ana trade forex, Bitcoin anauza vitu Shopify Yuko mwanza, Mimi akili yangu ulikuwa inanituma kuwa atakuwa 30+ kwanza ukizingatia kaoa ndoa ya mkeka mwaka huu.....
Shukran na asante kwa somo mr nina imani wengi wenye shida kama yangu watajifunza kupitia hiki 🙏
 
Ndiyo na kiu yako ndiyo itakufikisha unakotaka kwenda, Kuna kijana nimekuwa nikiwasiliana Naye toka mwaka jana mwezi wa Saba sijawahi kukutana Naye ila nimehandle muamala yake Sana, Ana trade forex, Bitcoin anauza vitu Shopify Yuko mwanza, Mimi akili yangu ulikuwa inanituma kuwa atakuwa 30+ kwanza ukizingatia kaoa ndoa ya mkeka mwaka huu...
You Inspired me alot Boss, kuna rafiki yangu mmoja anapenda Online Business hasa Forex, yani sana nafikiri angeona hili andiko angefurahi sana kuona things are possible, previous years nilikuwa mweupe kabisa kwenye Forex kwasasa ninaijua japo Price Action tumekubaliana hakuna kitu kingine cha kufanya kuanzia tar 1/2021 zaidi ya FX kujenga Consistency nzuri.

Rafiki yangu anakuja Dsm tukomae wote siku moja tutapenda tuonane utupe miongozo yako maana sie bado tunachangamoto nyingi sana na tuna picha kubwa sana.
 
Back
Top Bottom