Mimba za kutegeshea zinavyoharibu maendeleo.

mbona unaniangusha teacher wangu gfsonwin?

Hivi kila vidude vinapokutana ni kwa ajili ya kutengeza watoto??

Ingekuwa hivyo wengine tungewajengea viota hewani....!!

Hata hivyo, nimependa hapo kwenye blue...mzigo wa mimba na mtoto siku zote unabebwa na mdada...ndo maana nashangaa kwa nini mtu anyejua atabeba mzigo alone halafu eti anatega mtego wa kujiingiza matatizoni!!

Kwani anazini na ng'ombe au shimo kwenye kibuyu?

Nimewatetea wapi tena amu....(najua babu mwenzangu asprin hataisoma vibaya na kuhisi ni "hamu")!!

Siyo kurudisha maendeleo kaka kwani watu wengine wanakuwa hawana hata cha kuendeleza bali ni huo msongo wa ubongo ambao unamkuta victim....

Yaani hata kama ulijiandaa kwa dinner, unapata ed ya kama siku 7 vile!

Achana na mimba bwana.... Mtu unatamani iwe gari au bajaji uweke reverse gear!!

Babu dc!!

kabisa kabisa mkuu

kwa kweli inakua inaleta kisebu sebu sana...
 
babu DC nafikiri hujanielewa niliposema wadada acheni hadi muwe tayari nilimaanisha waache kubeba mimba hadi wawe tayari sasa yampasa kutumia njia alokuwa anatumia siku nyingine ili asipate ujauzito. unajua mwisho wa siku mwenye tatizo hapa ni huyu dada manake mvulana akila kona unafikiri itakuwa nini?? na pia mwanamke ndo muhanga wa maudhi yote ya mimba zisizotarajiwa. wanawake hasa mabianti yawabidi kubadilika kumzalia mtu hakumfanyi akupende zaid ama akuoe.

Babu DC nakumbuka siku dada yangu mmoja wa ukoo mkubwa alipokuwa anaolewa ilikuwa zamani kidogo aliambiwa mwanaume ili akupende mzalie watoto wengi, maskini dada alikuwa anazaa kama kuku kila jumamosi leba baadae mama yangu akamwambia wewe zaa ukifikiri ni sifa utakuja kujizeesha umwache mwanaume akidunda kama kazaliwa jana.
 
ni kweli alimtia yeye, lakini walikubaliane watiane?
huyu naona anazungumzia zaidi ile ya kutegeshea, yaani mdada unafanya kwa makusudi kabisa kujipatia hiyo minba ili tu uolewe.
kuna zile "za kushtukiza" ambayo kwa haki ya Mungu mdada naye hakujua kama itatokea, hapo huwezi kumlaumu mdada, maana hata yeye hakupenda hayo yatokee ila ndo hivyo tena yemetokea, hapo huwezi kumlaumu binti.....ingawa kafanya kosa la kuzini.
lakini hizi "za kujitegeshea"! hata mimi naunga mkono mkaka atakayeishiwa mapenzi na huyo dada, sababu hajamtendea haki mwenzake. mimba ni ya wote kwa hiyo mnatakiwa au wote muwe na taarifa kuwa tunaitafuta, au wote msiwe na taarifa kama itatokea. kusiwe na "information asymmetry"
FP huyu kaka hajasema vyema kama binti alijua kwamba ni siku mbaya na mvulana alishiriki katika kuchukua tahadhari?? ama alimwachia binti ajijue mwenyewe?? kama nai wapenzi ni vyema mkashirikiana katika kuhalkikisha mimba szisizotarajiwa hazitokei na hili hufanywa na mkaka na mdada pia. mnakumbushana kutumia kinga ama kuwithdraw kosa ni la wote na hapaswi kumchukia.
 
Last edited by a moderator:
siosiri,,mimi nikipewaga taarifa kama hizo huwa nakua mdogo sana

coz sijajiandaa nazo,na kwanini anitegeshee sasa??

Hilo ndo swali la msingi kabisa......a million dollar question!!

damn it!! hivi alijitia mwenyewe ama ulimtia wewe?? kwanza tuanzie hapo ndipo niendelee.

Hii sasa inageuka na kuwa Teacher's talk show....twende kazi...lol!!

Hapana kbm, Huyu mdada anaupeo mkubwa tu kuhusu protection na nina hakika kanifanyia kwa makusudi kwani nimesikia kutoka kwa rafiki yake wa karibu.

Eti ulisikia kwa shoga yake?

Hapo sasa unaanza kunivunja moyo...Ulianzia wapi kuongea hayo mambo na shoga wa GF wako?

Usipokuwa mwangalifu utazalisha wote wawili....shauri lako!!

the shoo kubwa unanishangaza sana na leo ngoja niwape mchambo kidogo wakaka wadogo wa jf.
hivi mmesahau kwamba mwanamke ndo chanzo cha dhambi ulimwenguni?? je unasahau kwamba ananguvu hata ya kumuangusha kifua chuma kama SAMSONI na hata kuua kabisa?? kama mnalijua hilo kwanini mnajilengesha wenyewe?? kwani hao wanawake wenu wana shikaga yoyoyo zenu na kujitia ama huwa mnaziingiza wenyewe??

acheni visingizio bana, mnjua kabisa kwamba wanawake wanawatega yet manajilengesha what do you expect?

Teacher please, suala siyo kupiga games, suala ni kutegesheana mzigo...

Ni vitu viwili tofauti kabisa!!

No. Nimtashi juu ya prena protection na hilo lililonitokea nililisikia kutoka kwa rafiki ake wa karibu baada ya kunionea huruma navyohuzunika.

Hadi hapo umeshaharibu,

Hata kama umetegeshewa,....nenda kalee mwanao!!

Babu, inawezekana hata sio kama dada wa watu anafanya makusudi. Inaweza kuwa bahati mbaya. Ila kiukweli uchumba sugu umeshindikana mjini, mnajipanga hadi wapi? Jitu lina kazi, lina kibaby walker japo vitz, lina kiwanja mpigi magoe, afu linajipanga nini? Kama ikitokea unplanned pregnancy mnapaswa kuhandle pamoja. Sasa mambo ya kugoma kuhusika inahuu? Kumbe kila siku ukiwekeza ulijua pipa la mahindi hilo unamiminia nafaka?

tena sio mapacha, triplets, dadeki!

Hizo accidents zinaeleweka ila kwa ujumla wake, lazima dada atoe maelezo ya kujitosheleza kuonesha kuwa ilikuwa ajali na siyo calculated move!

Suala la uchumba sugu mnalitaka wenyewe...kwa nini uende kukaa kwa mwanamume asiyekuwa mumeo?

If you can get free milk, why keep a cow...by Rev Rwakatale!!

Babu DC!!
 
Kitu na box, kwanini ulimwaga ndani? Mnavyofahamiana si hata mzunguko wake uko familiar au?. kama unampenda muoane. Maendeleo gani unayoyawaza kipindi chote? kujenga nyumba angani?

BJ,

Wanaume wanaotunza hizo kumbukumbu ni wachache sana kama wapo......At least nilikuwa najaribu enzi zangu!!

Kitu gani kimfanye mtu ahangaike ni mizunguko ya mwenzake....??

Ndo maana kitu kikinasa, dada anatakiwa aandika maelezo kama page 10 hivi kabla hukumu haijatolewa!!

Babu DC!!
 
babu DC unless kama tunadress jambo moja kwa njia tofauti, huyu mkaka anajua kabisa kwamba nguvu ya mwanamke sas kwann hakujilinda yeye?? kama angekuwa mwangalifu angevaa kondom istoshe kijana hajitambui huyu manake mpasha habari wake ni rafiki wa gf wake jambo ambalo naona ni tatizo zaid kama je gf wake anamawazo hali hii atatokaje na hajampa nafasi ya kudiscuss naye ila anasikiliza watu baki. to me huyu ni mvulana asiyejua wajibu wake. babu mark my words atakuja hapa hapa jamvini kabla mwaka haujaisha akisimulia rafiki wa gf wake kamuharibia uhusianao wake kama hatakuja na uzi nimempa ujauzito rafiki wa gf wangu.
 
sasa huyo rafiki wa deu wako ndo anayekutakia mabaya na maisha ya tabu. let me tell you hakunaga watoto ambao wanakuwaga na roho wa Mungu kama watoto wa kwanza, na haijalish amepatikana wapi mzaliwa wako wa kwanza ni lango lako la baraka ama laana and believe me ukimtesa huyo mtoto utakuja juta.

kuna msemo usemao mwisho wa uwezo wako wa kufikiri ndio mwanzo wa matatizo yako, usifike mwisho wa kufikiri badala ya kujadili mimba ya kutegeshewa ungatuambia tujadili jinsi gani ya wewe kuweza kuvuka hapo ulipo bila kuchoka wala kukata tamaa.

Naona hapa unamtetea mwanamke mwenzio kwa kasi zaidi, ari zaidi na......!!

Babu DC!!
 
FP huyu kaka hajasema vyema kama binti alijua kwamba ni siku mbaya na mvulana alishiriki katika kuchukua tahadhari?? ama alimwachia binti ajijue mwenyewe?? kama nai wapenzi ni vyema mkashirikiana katika kuhalkikisha mimba szisizotarajiwa hazitokei na hili hufanywa na mkaka na mdada pia. mnakumbushana kutumia kinga ama kuwithdraw kosa ni la wote na hapaswi kumchukia.
kama nimemsoma vizuri kasema kategeshewa, kwa maana hiyo mdada alikuwa anajua anachokifanya, na kafanya hivyo makusudi kabisa ili aolewe.
nakubaliana na wewe kabisa kuwa kama kweli mnapendana na hamtaki hayo yatokee ni juhudi za wote wawili kuhakikisha kuwa mnalindana kwa mambo kama hayo. tena kuna wakaka nawajua wapo vizuri sana na kalenda na kufwatilia siku za wapenzi wao. utakuta hata mdada unaweza upoteze step lakini kaka akakukumbusha, lakini ni wakaka wangapi wenye kufanya hivi? wengi huwa wanaona ni jukumu la mdada kujichunga, na wengine wanaona "isiwe tabu" tutakuwa tunakula pipi yetu kwenye makaratasi kila wakati
 
ni kweli alimtia yeye, lakini walikubaliane watiane?
huyu naona anazungumzia zaidi ile ya kutegeshea, yaani mdada unafanya kwa makusudi kabisa kujipatia hiyo minba ili tu uolewe.
kuna zile "za kushtukiza" ambayo kwa haki ya Mungu mdada naye hakujua kama itatokea, hapo huwezi kumlaumu mdada, maana hata yeye hakupenda hayo yatokee ila ndo hivyo tena yemetokea, hapo huwezi kumlaumu binti.....ingawa kafanya kosa la kuzini.
lakini hizi "za kujitegeshea"! hata mimi naunga mkono mkaka atakayeishiwa mapenzi na huyo dada, sababu hajamtendea haki mwenzake. mimba ni ya wote kwa hiyo mnatakiwa au wote muwe na taarifa kuwa tunaitafuta, au wote msiwe na taarifa kama itatokea. kusiwe na "information asymmetry"

Ngoja sasa nikapumzike,

Hebu endeleza hii shule mzee mwenzangu........

Haki ya nani wewe ni rare member wa the 1947 club...

Babu DC!!
 
Naona hapa unamtetea mwanamke mwenzio kwa kasi zaidi, ari zaidi na......!!

Babu DC!!
babu mimi si kwamba namtetea ila namtete huyu mtarajiwa. nimelea mtoto wa aina hii, ninaye hadi leo na naweza kukuambia ndiye mtoto ninayemtegemea kwa akili na busara, imagine mtoto wa kiume anayeweza kubajeti house hold expenditures siyo mchezo. sometimes huwa nawaza baba yake angemkataa ileo hii ningepata wapi mwl wa wadogo zake?? na je ningekuwa nimewanyima wanangu bahati kiasi gani?? damu ya mtu ni damu tu babu iwe umeipata kwa kupangilia ama kwa kutopangilia.
 
kama nimemsoma vizuri kasema kategeshewa, kwa maana hiyo mdada alikuwa anajua anachokifanya, na kafanya hivyo makusudi kabisa ili aolewe.
nakubaliana na wewe kabisa kuwa kama kweli mnapendana na hamtaki hayo yatokee ni juhudi za wote wawili kuhakikisha kuwa mnalindana kwa mambo kama hayo. tena kuna wakaka nawajua wapo vizuri sana na kalenda na kufwatilia siku za wapenzi wao. utakuta hata mdada unaweza upoteze step lakini kaka akakukumbusha, lakini ni wakaka wangapi wenye kufanya hivi? wengi huwa wanaona ni jukumu la mdada kujichunga, na wengine wanaona "isiwe tabu" tutakuwa tunakula pipi yetu kwenye makaratasi kila wakati
FP umemsoma huyu kijana?? hajampa gf wake muda wa kumsikiliza amekimbilia kuhukumu kwa maneno ya rafilki wa gf wake mark ma words huyu kijana atamlala huyu rafiki wa gf wake.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja sasa nikapumzike,

Hebu endeleza hii shule mzee mwenzangu........

Haki ya nani wewe ni rare member wa the 1947 club...

Babu DC!!
Noted with thanx, lol!
usiondoke babu tusaidiane kuwaweka hawa wajukuu katika mstari.
hicho kitendo siyo haki kabisa kufanyika, itokee bahati mbaya, wote hamkujua sawa lakini kama umejua na unataka tu kumfunga mtu ili akuoe hiyo si busara kabisa. Tena mimi naona kama mtu anazugazuga kukuoa ni vizuri ukajibakia zako bila mimba, huwezi jua labda hakuwa wako, na ukaja pata mwingine. sasa vipi inavyotokea umejilengesha na jamaa kala kona vile vile? maana kukupa mimba si lazima akuoe
 
FP umemsoma huyu kijana?? hajampa gf wake muda wa kumsikiliza amekimbilia kuhukumu kwa maneno ya rafilki wa gf wake mark ma words huyu kijana atamlala huyu rafiki wa gf wake.
ha haaaaaa, gfsonwin, samahani sijasoma post zake zote, nilivyosoma hapo juu nikaona kama amelengeshewa, lol!
kama ni hivyo basi ana matatizo yake.
ila rafiki yangu haya mambo ya kulengeshewa pia yapo. ndo hayo niliyokuwa nayazungumzia mimi kuwa hayafai
 
Last edited by a moderator:
babu DC unless kama tunadress jambo moja kwa njia tofauti, huyu mkaka anajua kabisa kwamba nguvu ya mwanamke sas kwann hakujilinda yeye?? kama angekuwa mwangalifu angevaa kondom istoshe kijana hajitambui huyu manake mpasha habari wake ni rafiki wa gf wake jambo ambalo naona ni tatizo zaid kama je gf wake anamawazo hali hii atatokaje na hajampa nafasi ya kudiscuss naye ila anasikiliza watu baki. to me huyu ni mvulana asiyejua wajibu wake. babu mark my words atakuja hapa hapa jamvini kabla mwaka haujaisha akisimulia rafiki wa gf wake kamuharibia uhusianao wake kama hatakuja na uzi nimempa ujauzito rafiki wa gf wangu.

Hapa kuna issues mbili teacher...

Moja ni suala la kutegeshewa mimba ambalo hata wajanja huwa mara nyingine wananaswa....Sex inatawaliwa na mwanamke na anaweza kukufanyia lolote kama kweli anajitambua....Chance ya kutegeshewa ipo na wahanga wapo wengi!

Jingine ni lile la kwenda kutafuta information kwa shoga wa GF wake....hapo kwa kweli hata mie nimekereka sana. Mwanamume anayejitambua hawezi kufanya blunder kama hiyo!

Babu DC!!
 
ha haaaaaa, gfsonwin, samahani sijasoma post zake zote, nilivyosoma hapo juu nikaona kama amelengeshewa, lol!
kama ni hivyo basi ana matatizo yake.
ila rafiki yangu haya mambo ya kulengeshewa pia yapo. ndo hayo niliyokuwa nayazungumzia mimi kuwa hayafai

ni kweli haya yapao ila binti anyefanya haya ilihali yeye ndo muhanga wa mimba isotarajiwa bado ni mjina na mwisho wa siku kidume lazima kimshinde tu
 
kama nimemsoma vizuri kasema kategeshewa, kwa maana hiyo mdada alikuwa anajua anachokifanya, na kafanya hivyo makusudi kabisa ili aolewe.
nakubaliana na wewe kabisa kuwa kama kweli mnapendana na hamtaki hayo yatokee ni juhudi za wote wawili kuhakikisha kuwa mnalindana kwa mambo kama hayo. tena kuna wakaka nawajua wapo vizuri sana na kalenda na kufwatilia siku za wapenzi wao. utakuta hata mdada unaweza upoteze step lakini kaka akakukumbusha, lakini ni wakaka wangapi wenye kufanya hivi? wengi huwa wanaona ni jukumu la mdada kujichunga, na wengine wanaona "isiwe tabu" tutakuwa tunakula pipi yetu kwenye makaratasi kila wakati

Kutegeshewa kunaumiza sana @FP,

Unaweza ghafla ukaanza kumchukia mtu ambaye ulimpenda sana katika hii dunia....

Babu DC!!
 
Unapenda kavu halafu unalalamika mimba za kutegesha

Kwani akiamua kusababisha pancha kwenye mpira utamzuia?

Kwani zinahitajika risasi ngapi kuua mtu?

Hakuna mtu anaweza kumshida mwanamke aliyeamua kufanya kitu kama hiki...

Babu DC!!
 
babu mimi si kwamba namtetea ila namtete huyu mtarajiwa. nimelea mtoto wa aina hii, ninaye hadi leo na naweza kukuambia ndiye mtoto ninayemtegemea kwa akili na busara, imagine mtoto wa kiume anayeweza kubajeti house hold expenditures siyo mchezo. sometimes huwa nawaza baba yake angemkataa ileo hii ningepata wapi mwl wa wadogo zake?? na je ningekuwa nimewanyima wanangu bahati kiasi gani?? damu ya mtu ni damu tu babu iwe umeipata kwa kupangilia ama kwa kutopangilia.

Sina ugomvi na hilo kwani watoto wa namna hiyo tunao wengi..

Suala ni kumpa maelezo ya kutosha baba kwamba kweli hujamwekea mtego...

Ila hapa jamaa analalamika kwamba kategeshewa. Unadhani katendewa haki??

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom