Milipuko yatikisa Zanzibar

Milipuko yatikisa Zanzibar

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,842
Reaction score
10,765
Nimeisikia live redioni sasa hivi Faruq Karim akiripoti kuwa imetokea milipuko kwanza hoteli ya Forodhani kisha muda mfupi tena kwenye lango la kanisa la anglikani mkunazini huko Zanzibar. Walioko huko watatujuza zaidi

Source: Radio one zilizotufikia

====

Hakuna Majeruhi
Dear Friends, before any innacurate information starts floating around: two bombs went off this afternoon at the entrance to the Anglican Church compound in Mkunazini.

The bombs were placed near the entrance on the street. There were no injuries to pedestrians and no damage to the property. We are most grateful that no one was hurt.

Rev. Jerry
Anglican Diocese of Zanzibar
 
Sera mbaya za ccm. wameuza viwanda vijana hawana kazi ndio maana wanarubuniwa na washenzi al kaeda kirahisi
 
Wakuu wenye updates zozote watuletee hapa habar nmeisikia hapa radio 5.


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Milipuko miwili imetokea huko Zanzibar mchana huu..moja ikiwa ni kanisa la Anglican Mkunanzini na mwingine kwenye hotel huko Forodhani..Polisi bado wanafanya uchunguzi.

source: Radio one
 
Magaidi wamepiga hodi tanzania nasi tukawaruhusu waingie? Sasa tujiandae kuzikana tu.
 
Duh!! Kanisani tena kumbe ndio maana katika wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar kati ya 67 Wakristo ni 2 na wote wametoka katika kipengere cha vikundi vya Kidini. inamaanisha kama kungekuwa hakuna kipengere cha dini Kutoka Zanzibar kusingekuwepo na Mkristo.
 
serikali imezidi kulea hawa wahuni,sijui huo uchunguzi unafanyiwaga wapi. ndo maana hayaaachagi haya magaidi
 
ujumbe umefika dodoma na ni saa moja tu kabla ya rais kuhutubia bunge la katiba
 
tunaitaji majibu ya kina,maana haiwezekani nchi ni moja ila kila siku ni milipuko huko visiwani,hawa watu wanapitisha wapi hizi silahaa ama vilipuzi?mtu anashuka bandarini dar anaingia navyo mpaka visiwani,IGP na AMIRI JESHI MKUU JK tunaitaji majibu ya kina kama usalama umewashinda mtuambie mapema
 
Kusiwe kumetokea maafa..poleni watanzania wenzangu huko nyumbani
 
tunaitaji majibu IGP MWEMA na waziri wa mambo ya ndani ya nchi CHIKAWE,
Waziri kivuli tunataka ili jambo ulivalie njuga sana tupate majibu na hadidu a rejea ziwepo.kuna matukio mengi sana yametokea zanzibar hakuna majibu
 
Back
Top Bottom