Milestone Record: Uingereza alitawala 90% ya dunia.

Milestone Record: Uingereza alitawala 90% ya dunia.

Tofauti ya USA na UK ni eneo lakini walioitawala hiyo USA wengi wana asili ya UK kuanzia kwa George Washington na wengin wengi waliokuja nyuma yake. Kumbuka USA pia ilitawaliwa na Britan ambayo ndio Uingereza
Generally misingi karibia yote ya Marekani ya leo iliwekwa na Uk. Kwa mantiki hiyo USA na UK ni baba na mtoto.
 
Mwingireza hakutawala eneo lote la usa Kama ilivyo Leo kina majimbo yalikaliwa na wahispaniola
Yah ni kweli lkn utawala uliokuwa na nguvu zaidi ni wa waingereza, ndio maana hata wakat wa kupigania uhuru kina Washington ilibidi wapate support nyingine kutoka kwa wafaransa, waholanzi nao hao hao wahispaniola ili kumng'oa muingereza. Bila hivyo wasingeweza na ukizingatia hizo nchi tajwa hapo juu zilikuwa zimeshakung'utwa vibaya na muingereza na kunyanganywa baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyatawala, sana sana ufaransa ndo ilikuwa kibonde kbs mbele ya muingereza alinyang'anywa eneo kubwa la Canada walilokuwa wakilitawala bila kusahau Cameroon ambayo ilikuwa chini ya ufaransa walichapwa mpk wakaacha baadhi ya ngome zao ambazo baada ya kipigo zilikaliwa na waingereza mpk uhuru. Eneo ndo sasa hivi wanataka kujitenga na lile linalozungumza kifaransa. Pia waholanzi walipokea kipigo kizito kule Afrika Kusini wakati wa kupigania koloni. Ikumbukwe waholanzi ndio waliotangulia kufika Africa Kusini ila muingereza alikuja nyuma akamchapa na kuchukua eneo lote ambapo baadae waholanzi wakakubali kuwa chini ya utawala wa waingereza mpk walipodai uhuru wao wenyewe. So tunapozungumzia mtawala wa Marekani hapa tunamzungumzia UK maana ndio alikuwa mbabe wa eneo na waliodai uhuru ni vizazi vyao wenyewe ndio maana hata US yenyewe huwa inasherekea uhuru mmoja tu kutoka kwa waingereza na sio wahispaniola wala wafaransa. Trump alisema juzi "wamarekani lugha yetu ni kingereza, so ikitokea mtu anazungumza lugha tofauti na kingereza mfano kihispaniola, kireno, kifaransa nk basi huyo sio mmarekan ni mgeni kwahiyo inabidi idara inayohusika na uhamiaji wamuulize vibali huyo mtu.
 
Generally misingi karibia yote ya Marekani ya leo iliwekwa na Uk. Kwa mantiki hiyo USA na UK ni baba na mtoto.
Baba ni baba tu. Leo hii UK ikivamiwa kijeshi nina imani US ndio itakuwa nchi ya kwanza kumsaidia kwa gharama yoyote ile ikisaidiwa na Canada, Australia na New Zealand, hivyo hivyo na kwa UK endapo US au any country kati ya hizo mlizotaja hapo juu itavamiwa.
 
Ndicho anachokifanya Mchina bro.
Yan anampumulia USA mgongoni ktk rank ya uchumi.
Na watafiti wanasema 20 to 30 years China will be the universal greatest economy.
Na ashaanza kuwa na ushawishi mkubwa kibiashara pande zote ulimwenguni.
Yeah bado hajafika ila kupitia mpango wake wa ONE BELT SILK ROAD anaweza kuja kuwa namba 1.
Kwa ninavyouona uelekeo Next super power hatahitaji ushawishi mkubwa wa kijeshi itabidi awe na nguvu za kiuchumi!. Nchi nyingi zinajiweka vizuri kijeshi zikijisahau kiuchumi!.
 
China ilikuwa koloni la Japan.
China haijawahi kuwa koloni la Japan ni baadhi ya visiwa vya china, ila China alikuwa anakaliwa kimabavu na UK mpaka hivi majuzi ndo China karudishiwa Hong Kong na Macau!..
Ukifatiria vita ya Opium utaona jinsi China alivyopigwa mara 2 na muingereza!.
 
Baba ni baba tu. Leo hii UK ikivamiwa kijeshi nina imani US ndio itakuwa nchi ya kwanza kumsaidia kwa gharama yoyote ile ikisaidiwa na Canada, Australia na New Zealand, hivyo hivyo na kwa UK endapo US au any country kati ya hizo mlizotaja hapo juu itavamiwa.
Hao wote ni ndugu wa damu.
 
90% ya dunia....napata wasiwasi na hizi data...walitawala eneo kubwa lkn hawakufikia asilimia 90...kipindi chao palikua na mataifa makubwa pia ambayo yalikua yanascramble kujitanua zaidi....wafaransa, wajerumani, spanish,russia empire etc.....ni kweli yeye ndo aliibuka kinara lkn sio kwa asilimia zote hizo
Mimi mwenyewe napata mashaka na huu utafiti
Kuwasaidia tu kujua kwanini UK aliweza kuwa na eneo kubwa la utawala wake ingieni humu.
Au ukitaka compare empire zote zilizowahi tokea duniani kwa ukubwa wake unaweza anzia hapa
"the land where the sun never settle".
 
Attachments

Umesahau Ethiopia
View attachment 1046002Mwandishi Stuart Laycock alifanya utafiti katika historia nzima ya dunia na kuja na kitabu kinachoitwa ‘All the Countries We've Ever Invaded: And the Few We Never Got Round To’.
Hiki kitabu kimeangalia maeneo yote duniani ambayo Utawala wa Muingereza uliweza vamia na kupatawala au kuweka majeshi yake na katika tafiti yake imeoneka kati ya nchi 200 zilizopo duniani ni nchi 22 pekee kati ambazo utawala wa muingereza hakuweza zitawala!, hii ni sawa na kusema Muingereza aliweza tawala 90% ya dunia kwa wakati wake!.
Nchi 22 zilizopona mabavu ya Muingereza ni:
  1. Andorra
  2. Belarus
  3. Bolivia
  4. Burundi
  5. Central African Republic
  6. Chad
  7. Congo, Republic of
  8. Guatemala
  9. Ivory Coast
  10. Kyrgyzstan
  11. Liechtenstein
  12. Luxembourg
  13. Mali
  14. Marshall Islands
  15. Monaco
  16. Mongolia
  17. Paraguay
  18. Sao Tome and Principe
  19. Sweden
  20. Tajikistan
  21. Uzbekistan
  22. Vatican City
source: RT
 
Umesahau Ethiopia
Kaangalie nani aliingia kumsaidia watoa waitaly Ethiopia!, unajua kuwa kwenye ww2 mussolini aliwapiga waethiopia mpaka Haille Sellasie akaenda kaa mafichoni uingereza!.
Achana na hiyo waethiopia waliwateka wamissionary wa UK kikatumwa kikosi wakomboa na kikawapiga mpaka mfalme wa ethiopia akaamua kujiua (Battle of Magdala).
 
China haijawahi kuwa koloni la Japan ni baadhi ya visiwa vya china, ila China alikuwa anakaliwa kimabavu na UK mpaka hivi majuzi ndo China karudishiwa Hong Kong na Macau!..
Ukifatiria vita ya Opium utaona jinsi China alivyopigwa mara 2 na muingereza!.
Bro zile Opium wars zilikua vita za biashara sio utawala.
Zilikua ni trade wars.
Hazihusiani na kutawaliwa kwa China.
Na British navy ilisaidiwa na France la sivyo wasingefua dafu.Na hata hizo Hong Kong na Macau zilichukuliwa na UK baada ya Japan kupigwa vita ya pili ya dunia maana yeye Japan ndio alikua anazishikilia.
Na kwa hii contemporary world UK hana nguvu ya kumpiga China tena.
 
1. Opium wars zilikuwa 2 moja ya mwaka 1839–1842 ambayo British Empire alipigana yeye mwenyewe na China halafu na nyingine ya mwaka 1856-1860 ambayo ndio alisaidiwa na France Empire.
2. China alitawaliwa sababu alitakiwa fata matakwa ya UK, imagine leo Tz ije pigwa na Kenya ili tuwaruhusu wauze bangi yao nchini kwetu utasema huko sio kutawaliwa?.
3. Vita ya pili (opium war) ndio China alitakiwa aachie Bandari zake 5 zitumiwe na UK pamoja na kuwaachia visiwa vya Hong Kong.
4. Japan hakuwahi chukua Hong Kong yeye aliichukua Manchuria ambayo ilikuwa protectorate ya warusi.
5. UK alikuwa ashinde hata bila msaada ila France alimsaidia tu baada ya mmoja wa mwananchi wake kuuliwa na wachina!.
6. Kipindi hicho bado china haikuwa na nguvu kuweza pigana na Europeans yeyote na ikamshinda!.
Ni kweli mara baada ya ww2 ndio china akajitambua na kujipanga, sasa hivi haingiliki kizembe.
Hebu rudia zisoma vizuri Opium Wars 1&2!.
 
Ila mwaka 1912 si walimpindua Yule Qing alokuwa anashirikiana na UK na wakaunda taifa huru ambalo lilichukua asilimia 90 ya eneo la China.Mwaka 1949 ndio China nzima ikavuta maeneo yake na kuitwa People's republic of China ikabakia Macau na Hong Kong tu.
Ambazo 1977 km sikosei ndio walizirudisha UK.

HUKO JUU NIMEKUELEWA NA NITAENDA KUISOMA VEMA.
 
Kweli dunia ni duara, aliyetawala karibia dunia yote Leo hana ushawishi mkubwa kama aliokuwa nao, USA nae ajiangalie sana, unaweza shangaa Burundi baadae akaja kuwa mtawala wa dunia.
😂😂😂
 
Kweli dunia ni duara, aliyetawala karibia dunia yote Leo hana ushawishi mkubwa kama aliokuwa nao, USA nae ajiangalie sana, unaweza shangaa Burundi baadae akaja kuwa mtawala wa dunia.
Well said. The IQ of Tanzanians is among the lowest in the world.
 
Back
Top Bottom