Milestone Record: Uingereza alitawala 90% ya dunia.

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,125
rt-20190314-0002.jpg
Mwandishi Stuart Laycock alifanya utafiti katika historia nzima ya dunia na kuja na kitabu kinachoitwa ‘All the Countries We've Ever Invaded: And the Few We Never Got Round To’.
Hiki kitabu kimeangalia maeneo yote duniani ambayo Utawala wa Muingereza uliweza vamia na kupatawala au kuweka majeshi yake na katika tafiti yake imeoneka kati ya nchi 200 zilizopo duniani ni nchi 22 pekee kati ambazo utawala wa muingereza hakuweza zitawala!, hii ni sawa na kusema Muingereza aliweza tawala 90% ya dunia kwa wakati wake!.
Nchi 22 zilizopona mabavu ya Muingereza ni:
 1. Andorra
 2. Belarus
 3. Bolivia
 4. Burundi
 5. Central African Republic
 6. Chad
 7. Congo, Republic of
 8. Guatemala
 9. Ivory Coast
 10. Kyrgyzstan
 11. Liechtenstein
 12. Luxembourg
 13. Mali
 14. Marshall Islands
 15. Monaco
 16. Mongolia
 17. Paraguay
 18. Sao Tome and Principe
 19. Sweden
 20. Tajikistan
 21. Uzbekistan
 22. Vatican City
source: RT
 
Kweli dunia ni duara, aliyetawala karibia dunia yote Leo hana ushawishi mkubwa kama aliokuwa nao, USA nae ajiangalie sana, unaweza shangaa Burundi baadae akaja kuwa mtawala wa dunia.
Tofauti ya USA na UK ni eneo lakini walioitawala hiyo USA wengi wana asili ya UK kuanzia kwa George Washington na wengin wengi waliokuja nyuma yake. Kumbuka USA pia ilitawaliwa na Britan ambayo ndio Uingereza
 
HII INADHIHIRISHA KUWA DUNIA LAZMA IWE NA MBABE ILI ITULIE. HISTORIA INAONYESHA DUNIA HAIJAWAHI KUKAA BILA SUPER POWER NATION. ZIMETAWAKA DUNIA: BABYLON, RUMI, UK NK. SASA NI ZAMU YA US, JAPO WATU HUMU HAWAKUBALI HILO. KAMA US ITAANGUKA LITAIBUKA TAIFA LINGINE NA LINAWEZA KUWA TISHIO ZAIDI.
 
US zama zake zinapita mbona kuna Dragon anaamka on the Eastern sea board!..
 
Huyo Mchina bado ana safari tumpe muda! Japo huenda ikawa kweli
Yeah bado hajafika ila kupitia mpango wake wa ONE BELT SILK ROAD anaweza kuja kuwa namba 1.
Kwa ninavyouona uelekeo Next super power hatahitaji ushawishi mkubwa wa kijeshi itabidi awe na nguvu za kiuchumi!. Nchi nyingi zinajiweka vizuri kijeshi zikijisahau kiuchumi!.
 
90% ya dunia....napata wasiwasi na hizi data...walitawala eneo kubwa lkn hawakufikia asilimia 90...kipindi chao palikua na mataifa makubwa pia ambayo yalikua yanascramble kujitanua zaidi....wafaransa, wajerumani, spanish,russia empire etc.....ni kweli yeye ndo aliibuka kinara lkn sio kwa asilimia zote hizo
 
Mimi mwenyewe napata mashaka na huu utafiti
 
Tofauti ya USA na UK ni eneo lakini walioitawala hiyo USA wengi wana asili ya UK kuanzia kwa George Washington na wengin wengi waliokuja nyuma yake. Kumbuka USA pia ilitawaliwa na Britan ambayo ndio Uingereza
Mwingireza hakutawala eneo lote la usa Kama ilivyo Leo kina majimbo yalikaliwa na wahispaniola
 
Hata leo Uingereza bado inatawala Dunia, kwanini? Lugha yake ndiyo imekuwa yenye ushawishi mkubwa duniani kote na ndio ya kibiashara. Kufanikisha hilo tu si haba mkuu
 
90% ya dunia....napata wasiwasi na hizi data...walitawala eneo kubwa lkn hawakufikia asilimia 90...kipindi chao palikua na mataifa makubwa pia ambayo yalikua yanascramble kujitanua zaidi....wafaransa, wajerumani, spanish,russia empire etc.....ni kweli yeye ndo aliibuka kinara lkn sio kwa asilimia zote hizo
Mimi mwenyewe napata mashaka na huu utafiti
Hebu pinga kwa facts, ilitawala asilimia ngapi kama sio 90%
 
Back
Top Bottom