Ni kweli.
Halafu kitu kuwa mila na desturi haina maana ni kizuri, kuna mila na desturi nyingi mbaya na za kijinga.
Kwa hiyo, hata kama kitu ni mila na desturi yetu kweli, inabidi utuambie uzuri wake zaidi ya kuwa mila na desturi tu, kwa sababu kitu kuwa mila na desturi haimaanishi ni kizuri.
Inawezekana kabisa katika jambo fulani, kile kitu cha mila na desturi yetu ni cha kijinga na kimepitwa na wakati, na kitu cha kigeni ndicho kitatufaa.
Hivi mtu anaweza kukataa utamaduni wa kuweka rekodi kwa kuandika, au kutumia teknolojia mpya inayosaidia, kwa sababu tu si mila na utamaduni wetu?
Si tutadumaa kimaendeleo hapo?
Ukishaelewa hili, utajua suala la "mila na utamaduni" si hoja ya kimantiki, ni "argument from tradition" logical fallacy.