Mikopo Elimu ya Juu: Hatimaye Value Retention Fee 6% yaondolewa

Mifumo ya nchi yetu iko slow. Sasa kama mtu tayari alikuwa na mshahara mkopo aliuomba wa nini??

Haya kuomba mkopo siyo tatizo: Miaka yote mitatu ya chuo unachukua MKOPO ( ambao retention fee yake imeobdolewa ) +MSHAHARA unaanzaje kulialia eti unabakiwa na pesa ndogo baada ya makato kwanini pesa zote za mshahara na mkopo ulikuwa UNATUPA JALALANI???
Hawa diploma wengi wanaenda kusoma na familia. Fikiria basic ya laki 4 na take home ya laki 3. Ada ya chuo na familia ile sio rahisi
 
Serikali haija shauriwa vizuri kwenye hili.

1. Retention fee inaongeza muda wa kulipa.
2. 15% inakaza ukali wa maisha.

Hii maana yale kwenye makato hakuna unafuu, bali muda wa kulipa deni ndio utapungua.


Ni heri wangeacha 6% lakini wapunguze loan fee kutoka 15 to 9% au even lower.


Kwangu mimi sioni unafuu hapo..
Naamini we si muhanga wa hii kitu.

Ungekua muhanga usingethubutu kusema ulichosema.
 
Wajuzi wa uchumi hebu fafanueni, hiyo asilimia 6 inapunguza makato kwa kiwango gani
 
Watu wengi hawajui kukopa, ndio maana mikopo inawasumbuavsana. Mikopo ya muda mrefu inawafaa wanyabiashara na serikali tu.

Kama marejesho ya mkopo wako yanategemea mshahara, usichukue mkopo wa muda mrefu.
Hili ninalikubali kwa asilimia zote. Kwa uzoefu wako mkopo wa namna hiyo unapaswa maximum uwe miaka mingapi?
 
Hili ninalikubali kwa asilimia zote. Kwa uzoefu wako mkopo wa namna hiyo unapaswa maximum uwe miaka mingapi?
Angalia kiwango cha pesa unachoweza kuishi kwacho mwezi mzima baada ya makato, then amua kiwango utakachokopa.

Jitahidi angalau mkopo usiwe zaidi ya miaka 4.

Miaka 3 is far better.
 
Mfano nilikuwa nakatwa 250k ikitolewa hiyo 6% inabidi ukatwa sh ngap
250K unayokatwa utaendelea kukatwa kwani ni 15% ya mshahara, kumbuka deni lako halisi si hilo linaloonekana kwenye salary slip bodi wanadeni tofauti na hilo unaloliaona, ukimaliza kulipa unaloliona kwenye slip utaletewa jingine la retention. Hilo ndilo linalofutwa, lakini kama unadeni hata kama ni shilingi 700,000 na 15% ya mshahara wako ni 250K utakatwa hiyo hiyo 250K
 
250K unayokatwa utaendelea kukatwa kwani ni 15% ya mshahara, kumbuka deni lako halisi si hilo linaloonekana kwenye salary slip bodi wanadeni tofauti na hilo unaloliaona, ukimaliza kulipa unaloliona kwenye slip utaletewa jingine la retention. Hilo ndilo linalofutwa, lakini kama unadeni hata kama ni shilingi 700,000 na 15% ya mshahara wako ni 250K utakatwa hiyo hiyo 250K
Mbona sioni hata unafuuu
 
250K unayokatwa utaendelea kukatwa kwani ni 15% ya mshahara, kumbuka deni lako halisi si hilo linaloonekana kwenye salary slip bodi wanadeni tofauti na hilo unaloliaona, ukimaliza kulipa unaloliona kwenye slip utaletewa jingine la retention. Hilo ndilo linalofutwa, lakini kama unadeni hata kama ni shilingi 700,000 na 15% ya mshahara wako ni 250K utakatwa hiyo hiyo 250K
Nilijuwa makato kwenye salary slip yanapunguwa kidogo mana, hakuna kitu kinatutesa wafanyakazi kama makato ya HELSB
 
Diploma anapoenda kujiendeleza anakopa then akimaliza hawambadilishii muundo wa utumishi. Hivyo makato yakianza yanamkuta na mshahara ule ule wa Diploma aliokuwa nao.
Ni kweli kuna mtumishi aliajiriwa cheti, akaenda kujiendeleza akapata shahada utumishi wameshindwa kumfanyia promotion kwa maelezo kuwa promotion inatakiwa isiathiri mshahara lakini mtumishi huyu anatakiwa apewe mshahara wa shahada lakini imeshindikana anapewa wa cheti, na bodi wanamkata
 
Basi walikua waweke hiyo kwenye terms and condition za mkataba wa hodi sikuwahi ona hiyo mana wengine hawapendi vitu vinvohusiana na riba sio kutulaghai namna hiyo wakat wakulipa ndio wanaongeza condition sijawahi ona mimi
Hii serikali bhuana wanakumbuka kutokupandisha mishahara watumishi kwa miaka 6 lakini VRF imesimama miaka yote 6 kama imepakwa vumbi la Mkongo
 
Mama Samia miaka 9 tena. Sasa hivi tutalipa tulichokopa tu bodi ya mkopo. Hongera mama.

=====

SERIKALI imefuta tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni la wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) iliyokuwa ikitozwa zaidi.

Agizo la kufutwa kwa tozo hiyo imetolewa leo na Rais Samia Saluhu katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mwanza.

Akitoa agizo hilo Rais Samia alisema “Serikali imeamua kufuta asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa zaidi, lakini hata hivyo tumeamua riba ya asilimia 15 itabaki kama ilivyo.

Awali Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) liliwasilisha kilio cha wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) kwa Rais Samia Suluhu, na kutaka ongezeko la makato ya mkopo huo ipunguzwe na tuzo nyingine ziondolewe.

Akisoma risala Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Said Wamba alisema mikopo ya elimu ya juu imegeuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza dhana halisi ya serikali kuwa wanaopewa mikopo hiyo ni watoto wa maskini.

Alisema tozo ya kutunza thamani ya mkopo ya asilimia 6 (Value retention fee -VRF), tozo ya asilimia moja ya shughuli za kiutalawa (Loan Administration Fee) na adhabu ya asilimia 15 ya deni linalodaiwa kwa anayechelewa kulipa deni baada ya miaka miwili tangu kuhitimu chuo ni kaa la moto kwa wanufaika.

“Tozo ya asilimia 6 ya thamani ya deni inakuwa kubwa, kila mwaka inaongezeka tofauti na kiasi alichokopeshwa mnufaika, tunataka ipungue, mkopo unageuka kiama kikubwa kwa wafanyakazi na inapoteza uhalisia kuwa ni watoto wa maskini.” alisema Wamba na kuongeza

“Viwango au makato haya yanafanya vijana kutopiga hatua yeyote. Pia ni kinyume na katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 23(1) inayohitaji mtu kupata ujira kulingana na kazi yake,” alisema Wamba

Kwa mujibu wa Sheria Bodi ya Mikopo ya 2016, Kifungu 7.2.1.1 cha Mwongozo wa HESLB wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa Wanafunzi kinabainisha kuwa mnufaika wa mkopo wa bodi hiyo atalipa tozo ya kulinda thamani ya fedha ambayo itakatwa asilimia sita kwa mwaka tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.

Pia, katika kifungu 7.2.1.2 cha mwongozo wake huo, HESLB inaeleza kuwa itakata asilimia moja ya ada ya uendeshaji kwa mwanafunzi mnufaika.
View attachment 1770644
Kwa hili nampongeza ila kwa lile lingine sitaki kabisa nimechukia
 
Wale waliokatwa retention fee kabla ya tamko la Mh Rais itakuwa busara wakarejeshewa pia au zitumike kulipia deni husika kwa wale ambao bado hawajakamilisha bado
Mkuu. Umeongea point sana. Hivi waliokua wameisha katwa wanajisikiaje
 
Serikali haija shauriwa vizuri kwenye hili.

1. Retention fee inaongeza muda wa kulipa.
2. 15% inakaza ukali wa maisha.

Hii maana yale kwenye makato hakuna unafuu, bali muda wa kulipa deni ndio utapungua.


Ni heri wangeacha 6% lakini wapunguze loan fee kutoka 15 to 9% au even lower.


Kwangu mimi sioni unafuu hapo..
Kwani mkuu unalipwa mshahara mdogo? Mimi naona afadhali ya hii maana mwezi wa 9 namaliza aisee tangu 2017 wananikata ila walivyoondoa hio 6% nimeona ahueni...kubwa tu
 
Maana Yangu ni kwamba both retention fee na hyo 15% ni majanga kwa waTanzania wa hali ya chini hebu fikiri mtu analipwa 400k au 500k ,aje akatwe paye,mfuko wa afya,nssf, plus na hyo 15% ya HESLB unafikiri atabakiwa na kiasi gani??

km amendoa 6% ya retention it was right lakini kuna mzigo wa kukatwa tena 15%..
kifupi nilitaka ashughulikie vyote kwa pamoja.

Mkaruka soma pia uelewe nn nimelenga.
Anaelipwa 400,000 anakua anakatwa 60,000 na HESLB na take home yake inakua 291,900 tsh na anaelipwa 500,000 anakatwa na HESLB 75,000 kwaio take home yake inakua ni 358,800 tshs hapo nimeshatoa NSSF na kodi husika kwaio ukisema ilipwe 8% bodi ya mikopo inakua nusu hivyo badala ya kupata 291,900 + 30,000 = 321,900 tshs na hio ingine ni 358,800 + 37500 = 396,300 sasa hapo unakua unalala mika kitu gani mkuu
 
Back
Top Bottom