BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Utafiti wa Hali ya UKIMWI nchini (Tanzania HIV Impact Survey - THIS 2022/23) umeonyesha kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) kuwa kimepungua kutoka asilimia 4.9 mwaka 2016/17 hadi asilimia 4.4 mwaka 2022/23. Mikoa mitatu yenye kiwango cha juu cha maambukizi katika Utafiti huu ni Njombe (12.7%), Iringa (11.1%) na Mbeya (9.6%), na.
Mikoa yenye maambukizi ya chini ni Kigoma (1.7%), Manyara (1.8%) na Lindi (2.6%).
Kwa Utafiti wa mwaka 2016/17, mikoa iliyoongoza kwa kiwango kikubwa kwa maambukizi ilikuwa ni Njombe (11.4%), Iringa (11.1%) na Mbeya (9.3%). Mikoa iliyokuwa na maambukizi ya chini ilikuwa ni Kigoma (2.9%), Manyara (2.3% na Lindi (0.3%).
Katika kufikia malengo ya 95-95-95 ifikapo Mwaka 2025, Kiwango cha watu wanaofahamu hali yao ya maambukizi kuhusu VVU ni asilimia 82.7 kwa 2022/23 kulinganisha na asilimia 60.6 kwa mwaka 2016/17,
Kiwango cha Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na wanatumia dawa za Kufubaza VVU (ARV) ni asilimia 97.9 kulinganisha na asilimia 93.6 mwaka 2016/17
Aidha, kiwango cha wanaotumia dawa na wamefubaza VVU ni asilimia 94.3 mwaka 2022/23 kulinganisha na asilimia 87 mwaka 2016/17.