Waziri Mhagama: Maambukizi ya VVU na UKIMWI Yaendelea Kupungua Tanzania kwa Utafiti wa Mwaka 2022/2023

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
Imeelezwa kuwa Tanzania imepata Matokeo chanya katika Mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kwamba idadi ya maambukizi mapya inaendelea kupungua ikilinganishwa na matokeo ya Utafiti wa mwaka 2016/17.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Utafiti wa viashiria na matokeo ya VVU na UKIMWI ambao umekamilika. Waziri Mhagama alizungumza na waandishi hao Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2023.

Mhe. Jenista amesema lengo la utafiti huo ni kupima matokeo ya juhudi za mapambano dhidi ya UKIMWI ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya VVU na UKIMWI (Tanzania AIDS Impact Survey - THIS) kila baada ya miaka mitano ambapo Uchakataji wa takwimu zilizokusanywa unaendelea.

“Haya ni mafanikio mazuri ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeyafikia kuelekea kufikia Malengo ya kitaifa ya kufikia SIFURI TATU – yaani Kutokuwa na Maambukizi Mapya, Kutokuwa na Unyanyapaa na Ubaguzi, na Kutokuwa na Vifo Vitokanavyo na UKIMWI. Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya VVU na UKIMWI ya mwaka 2022/23 itazinduliwa rasmi tarehe 1 Disemba, 2023,” Amesema Mhe. Jenista.

Pia ameeleza kwamba utafiti wa aina hiyo hufanyika kupima mwenendo wa VVU na UKIMWI Duniani, kwa kupima kiwango cha maambukizi mapya na Kufubaa kwa VVU katika ngazi ya jamii. Kupitia utafiti huu, tutapata taarifa kuhusu viashiria na matokeo ya VVU/UKIMWI katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2022/23 ambazo ni takwimu muhimu kuhusu hali ya UKIMWI nchini.

“Utafiti wa mwaka 2022/23 ni wa Tano kufanyika nchini Tanzania, na wa pili wa aina ya Population Based HIV Impact Assessment - PHIA kufanyika katika ngazi ya Jamii na utafiti wa PHIA kwa mara ya kwanza ulifanyika nchini Tanzania mwaka 2016/17,” Ameeleza.

Aidha Mhe. Jenista amebainisha kuwa Utafiti huo umefanywa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Kudhibiti UKIMWI Zanzibar (Zanzibar AIDS Commission- ZAC), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar.

WhatsApp Image 2023-10-31 at 20.09.28.jpeg
F9xsXhHWEAAlqA2.jpg
WhatsApp Image 2023-10-31 at 20.09.29.jpeg
 
Back
Top Bottom