Nyanya mbichi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 3,716
- 2,220
Mbeya na Iringa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Kumbuka unatuma radio yako kwangu ikidunda inakurudilia mwenyew.
Mungu hakatazi kisichokuwepo!Hakuna ukweli wowote.come on jamani amkeni.Ni mungu pekee mwenye kucontrol nature hii.asikudanganyeni mtu yoyote.uchawi upo lakini hauna nguvu hizo.tusemeni ukweli
Nawezapata ya kupiga hii mijitu iliyompiga Tindu ya mlengo mwingine? Niipige yote hadi kwenye kiti waoTanzania ina maajabu yake japo hayajaweza kuandikwa, pengine kama nchi hii ingekuwa bara la wazungu basi nchi hii ingeandikwa katika kitabu cha maajabu kwa baadhi ya Mambo.
Sanjari na kuenea kwa dini ya kikatoliki katika mikoa Miwili hii, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya 70 asilimia ni Wakatoliki ukweli ni kwamba mambo yaliyomo ndani ya jamii hii ni ya kushangaza na kuacha maswali mengi.
Kuishi katika Mikoa hiyo miwili ni changamoto kubwa hasa kwa watu wenye tabia ya ubabe, uzinzi,kujionyesha onyesha, ulafi, uongo n.k ingawa unaweza pia kuonewa bila kuwa na tabia hizo.
Wenyeji wa Mikoa hiyo ni wafipa na wabende, ama kweli mchuano wao ni mkali,si ajabu bei ya radi imeshuka kufikia shilingi 2000/=
Tanzania ina mengi,watanzania ni wataalam
TESTIMONY
Sumbawanga. Sumbawanga, kama ilivyo maeneo mengine ya mikoa ya pwani-- Tanga na Pwani (Bagamoyo) na ile ya Kanda ya Ziwa, imekuwa ikisifika sana kwa vitendo vya kishirikina.
Maeneo hayo yababeba sifa ya uchawi, ambazo huenda zikizidiana eneo kutoka eneo moja hadi jingine, huku Sumbawanga ikitajwa kuwa ndiyo ‘iko vizuri’ zaidi kwa uchawi, hasa wa ‘teknolojia’ ya asili ya radi.
Kijiji cha Chipu ndio eneo maarufu kwa sifa ya uchawi wa radi mkoani Rukwa. Chipu ni kijiji kilicho nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, umbali wa takriban kilometa 30 kutoka Sumbawanga mjini.
Radi za asili zinazodaiwa kutengenezwa katika eneo hilo la ufipa, hudaiwa kutumika kama silaha kwa watovu wa nidhamu.
Mkazi wa Kitongoji cha Katandala mjini hapa, Chela Mwanakatwe ambaye ni mtaalamu wa tiba za asili, anaeleza kuwa zipo aina nyingi za radi kulingana na utengenezaji wake.
Anasema yapo makundi matatu tu ya radi ambayo ni radi ya kuonya ambayo huwa haimdhuru mtu lakini inatokea eneo ambalo yupo mlengwa ili kujenga hisia kwa mtu aliyefanya uasi. Pindi inapotokea baadhi ya watu waliopo eneo hilo, hujiuliza “nani amefanya kosa aende kutubu”.
“Kwa mfano watu wamekaa kwenye nyumba, radi huweza kufika na kufanya uharibifu wa nyumba bila kumdhuru mtu yeyote. Au mpo chini ya mti, radi inafika na kupasua mti pasipo kudhuru mtu,” anasema Mwanakatwe.
Anasema aina ya pili ni radi inayojeruhi ambayo hutumika kumjeruhi yule aliyafanya uasi ili aende kuomba msamaha kutokana na kosa alilofanya. Alisema mara nyingi radi hiyo hutumiwa kwa wale ambao wametenda kosa bila dhamira zao kuwatuma, kushawishiwa na kudanganya.
Anasema aina ya tatu ni radi inayokusudia kuua ambayo mara nyingi mhusika anakuwa amethibitika kutenda kosa na kupewa nafasi ya kuomba radhi, lakini ameshindwa kufanya hivyo. Alisema radi ya aina hiyo haina huruma.
Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi/ www.epaper.mcl.co.tz
Kwa maelezo yako ni dhahiri wewe bado ni mvulana ambaye unahjtaji mambo mengi ya kujifunza.Hapana lakini mimi najaribu kuwaza hivi kweli uchawi una nguvu kiasi hicho.mr naona kama ni stori tu
Kigoma wakatoliki 70% si kweli hata chembeKigoma,Rukwa,Kagera.
Watu mnatisha duuuuhNenda vijiji vya mwambao ziwa Tanganyika. Mfano Kabwe, Kasanga, Kilando, Wampembe etc huko ndo watalamu wapo mkuu.