Mikoa miwili ambayo radi huuzwa

Mikoa miwili ambayo radi huuzwa

Hakuna ukweli wowote.come on jamani amkeni.Ni mungu pekee mwenye kucontrol nature hii.asikudanganyeni mtu yoyote.uchawi upo lakini hauna nguvu hizo.tusemeni ukweli
Usibishe bwana haya mambo yapo mbona radi inatumwa mchana kweupe jua linawaka hata bila uwepo wa mvua hapana chezea sumbawanga
 
Hakuna ukweli wowote.come on jamani amkeni.Ni mungu pekee mwenye kucontrol nature hii.asikudanganyeni mtu yoyote.uchawi upo lakini hauna nguvu hizo.tusemeni ukweli
Usibishe bwana haya mambo yapo mbona radi inatumwa mchana kweupe jua linawaka hata bila uwepo wa mvua hapana chezea sumbawanga
 
Yupo dogo 18 yrs ni moto wa kuotea mbali anatengeneza Radi hatari .
Kwann wasitumie huo uchawi kutengeneza pesa?
Hapa ndipo naamini Mtoaji wa ridhiki na uhai ni Mungu tu.
Utakuta mtu anafanya yote hayo hata pesa hana, anaishi kwa tabu, chakula shida pamoja na mavazi.
 
Tanzania ina maajabu yake japo hayajaweza kuandikwa, pengine kama nchi hii ingekuwa bara la wazungu basi nchi hii ingeandikwa katika kitabu cha maajabu kwa baadhi ya Mambo.

Sanjari na kuenea kwa dini ya kikatoliki katika mikoa Miwili hii, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya 70 asilimia ni Wakatoliki ukweli ni kwamba mambo yaliyomo ndani ya jamii hii ni ya kushangaza na kuacha maswali mengi.

Kuishi katika Mikoa hiyo miwili ni changamoto kubwa hasa kwa watu wenye tabia ya ubabe, uzinzi,kujionyesha onyesha, ulafi, uongo n.k ingawa unaweza pia kuonewa bila kuwa na tabia hizo.

Wenyeji wa Mikoa hiyo ni wafipa na wabende, ama kweli mchuano wao ni mkali,si ajabu bei ya radi imeshuka kufikia shilingi 2000/=

Tanzania ina mengi,watanzania ni wataalam

TESTIMONY
Sumbawanga.
Sumbawanga, kama ilivyo maeneo mengine ya mikoa ya pwani-- Tanga na Pwani (Bagamoyo) na ile ya Kanda ya Ziwa, imekuwa ikisifika sana kwa vitendo vya kishirikina.

Maeneo hayo yababeba sifa ya uchawi, ambazo huenda zikizidiana eneo kutoka eneo moja hadi jingine, huku Sumbawanga ikitajwa kuwa ndiyo ‘iko vizuri’ zaidi kwa uchawi, hasa wa ‘teknolojia’ ya asili ya radi.

Kijiji cha Chipu ndio eneo maarufu kwa sifa ya uchawi wa radi mkoani Rukwa. Chipu ni kijiji kilicho nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, umbali wa takriban kilometa 30 kutoka Sumbawanga mjini.

Radi za asili zinazodaiwa kutengenezwa katika eneo hilo la ufipa, hudaiwa kutumika kama silaha kwa watovu wa nidhamu.

Mkazi wa Kitongoji cha Katandala mjini hapa, Chela Mwanakatwe ambaye ni mtaalamu wa tiba za asili, anaeleza kuwa zipo aina nyingi za radi kulingana na utengenezaji wake.

Anasema yapo makundi matatu tu ya radi ambayo ni radi ya kuonya ambayo huwa haimdhuru mtu lakini inatokea eneo ambalo yupo mlengwa ili kujenga hisia kwa mtu aliyefanya uasi. Pindi inapotokea baadhi ya watu waliopo eneo hilo, hujiuliza “nani amefanya kosa aende kutubu”.

“Kwa mfano watu wamekaa kwenye nyumba, radi huweza kufika na kufanya uharibifu wa nyumba bila kumdhuru mtu yeyote. Au mpo chini ya mti, radi inafika na kupasua mti pasipo kudhuru mtu,” anasema Mwanakatwe.

Anasema aina ya pili ni radi inayojeruhi ambayo hutumika kumjeruhi yule aliyafanya uasi ili aende kuomba msamaha kutokana na kosa alilofanya. Alisema mara nyingi radi hiyo hutumiwa kwa wale ambao wametenda kosa bila dhamira zao kuwatuma, kushawishiwa na kudanganya.

Anasema aina ya tatu ni radi inayokusudia kuua ambayo mara nyingi mhusika anakuwa amethibitika kutenda kosa na kupewa nafasi ya kuomba radhi, lakini ameshindwa kufanya hivyo. Alisema radi ya aina hiyo haina huruma.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi/ www.epaper.mcl.co.tz
wacha habari zako za kizamani na zisizo na mashiko!

wewe unaijua radi?
radi ni uchawi kama ulivyo uchawi mwingine, uchawi wa kuua mtu ni ghali sio kiivo mnavyodanganyana huko

sisi ndio wenye sumbawanga, ukiitaji zaidi kujua uliza sio uongouongo tu
 
Nilinunua radi kimzahamzaha aaaahh INA masharti sana kuitunza niliirudisha unaihifadhi sehemu ya majimaji
 
wacha habari zako za kizamani na zisizo na mashiko!

wewe unaijua radi?
radi ni uchawi kama ulivyo uchawi mwingine, uchawi wa kuua mtu ni ghali sio kiivo mnavyodanganyana huko

sisi ndio wenye sumbawanga, ukiitaji zaidi kujua uliza sio uongouongo tu
Kanywe chai kwanza ndo urudi, unabisha nini bwana?
 
Watz bwana, hizi ndoto za kuwa kwenye nchi ya kipato cha kati kufikia 2025 mtazisikia tu redioni. Wenzetu wanakwenda sayari nyingine kwa teknolojia sisi tunafikiria kununua radi!!!! Wakati hata ubunifu kwenye kilimo bado tunatumia jembe la mkono!!!
 
Yaani wazee mnataka sema huku na huku mara oyaaaa naomba radi ya buku mbili bila chenchi huku..!?
 
Watz bwana, hizi ndoto za kuwa kwenye nchi ya kipato cha kati kufikia 2025 mtazisikia tu redioni. Wenzetu wanakwenda sayari nyingine kwa teknolojia sisi tunafikiria kununua radi!!!! Wakati hata ubunifu kwenye kilimo bado tunatumia jembe la mkono!!!
Hao wataalam wa kutufikisha kwenye uchumi wa kati tunawaazima nchi gani? wataalam wa kilimo waliopo wamesaidia nini mpaka sekunde hii katika nchi..unaweza kuungana nami kwamba hata hawa waliopo humu ni wataalam wa fani mbalimbali?tuache kujadili tamaduni tusubiri uchumi wa kati?
 
Dah,mwanangu haolewi huko kwa wafipa aise,bora apate mchagga mtaftaji
 
Back
Top Bottom