Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

FREEDOM OF INFORMATION

Nafikiri umefika wakati tuwe na 'freedom of information' kwenye masuala yote ya mikataba hata kama sio kwa watanzania wote at least tukaanzia kwa wabunge.

Vile vile tume na kamati ya bunge ambayo kazi yake itakuwa kuchunguza mikataba kabla haijaizinishwa vinginevyo tutaendelea kuliwa.

Au tuanzishe fungu la pesa kwa 'Whistle blowers' na wawe protected.

______________________________
Dua la kuku halimpati mwewe
 
Dua,
Hapo umenena. Kwa kufanya hiyo mikataba iwe siri ni nani anayelindwa? Inawezekanaje kampuni moja tu ihodhi prospecting licenses za madini kama ilivyo Tanzania Royalty Exploration Corporation ambayo ni tawi la Barrick. Hii ina maana kwamba kama kuna kampuni mpya inakuja Tanzania kufanya prospecting lazima wawalipe TREC badala ya kuilipa serikali ya Tanzania. Ndiyo mirija hii aliyokuwa anaisema Mwalimu enzi zile za Ujamaa.
 
RAIS WA ZAMANI

IMETOLEWA NA THISDAY

Ex-president implicated in govt house sale ’scam’

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE administration of former president Benjamin Mkapa has been put on the spot over revelations that it sanctioned the controversial sale of government houses to high ranking officials at grossly deflated prices, THISDAY can reveal.

Investigations by this paper have found that ex-president Mkapa personally expedited the sale of house No. 474 along Mindu Street in Upanga, Dar es Salaam to the then Minister of State in the President’s Office responsible for Planning and Privatization , Dr Abdalah Kigoda, a transaction in which the government suffered a 123m/- loss.

The house, which previously belonged to the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), was acquired by the government at a cost of 190m/-. However, it has emerged that Dr Kigoda bought it for just 66.4m/-. This was after the government, through notice No. 7/201, ordered that the house be sold to a civil servant at ’book value.’

A letter signed by former State House Chief Secretary Matern Lumbanga then directed that the house be sold to Dr Kigoda, apparently on direct orders from Mr Mkapa.

’’I am bringing you instructions from President Mkapa regarding house No. 474 Mindu Street, Dar es Salaam. The instructions are that this house should be sold to Dr Abdallah Omar Kigoda, Minister of State, President’s Office,’’ said part of the chief secretary’s letter, which was addressed to the Treasury.

Documents show that in 2003, the house was valued at 93m/-, and a year later the government bought the same house for 190m/- before selling it for 66.4m/-. The explanation for the depreciation in price was a government ’directive’ that the house be sold at ’depreciated replacement value’, that is, excluding the value of the plot.

The validity of the transaction has been questioned by the Controller and Audit General’s office and the issue is currently being investigated by the Parliamentary Public Accounts Committee (PAC), under the chairmanship of Bariadi East Member of Parliament, John Cheyo (UDP).

Contacted by THISDAY in the city yesterday, Cheyo confirmed that the committee was indeed investigating the sale of government houses. He however, declined to discuss details, claiming that the Kigoda house issue is still under scrutiny and further submissions are to be made in parliament early next year.

’’We are investigating this issue but it is not yet ready for public consumption. It’s true that we have discussed that and other houses, but wait until we (committee) present our report to the National Assembly next year,’’ said Cheyo.

During a recent parliamentary session in Dodoma, the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, John Magufuli, defended the government’s decision to sell its houses, strongly asserting that there were no plans to form a commission of inquiry into the controversial sales which continue to generate heated public debate.

Explained Magufuli: ’’The sale of government houses started in 1963. It was repeated in 1973 and 1975. The need to sell government quarters usually arises when the costs of maintenance of the houses become unbearable.’’ He was responding to a question raised by Bariadi East legislator , John Cheyo.

Nonetheless, current President Jakaya Kikwete has said the fourth phase government intends to review the government houses sale exercise with the aim of clearing shortcomings that have arisen during the implementation of the exercise todate.

He conceded that the exercise was not foolproof, and needed to be revised to plug existing loopholes.
 
Kichuguu,

Huyu Mwanyika naye anakuja eti "...........leteni evidence......", hiyo mikataba inter alia IPTL, RADAR, SONGAS, RDC anataka tumpe evidence gani, hapo kuna yafuatayo
1.Negotiation skills = Zero
2.Kusoma mikataba na kuielewa = Zero
3.10% and/or 29% kickbacks = mia kwa mia
4.UZALENDO = Zero

i can go on and on and on. Hivyo nilivyotaja hapo juu vingekuwa ni kinyume chake, wala tusingekuwa tunazungumza hivi sasa

Inaelekea naye ni Chenge style!!!

Huyu Johnson Mwanyika alijipatia umaarufu sana wakati wa kesi ya uhaini ya akina McGhee mwanzoni mwa miaka ya themanini. Je ana undugu wowote na yule Mwanyika ambaye ni mwakilishi wa Barrick pale Tanzania?
 
Jana tumeshuhudia msiba mkubwa katika mikataba yetu ya madini ,mgodi wa buhemba umefungwa baada ya dhahabu yote kuchimbwa ndani ya miaka minne[ref taarifa ya habari ITV jana tar 22].
hii inaonyesha namana gani soon hata migodi mingine itamaliza kuchimba dhahabu na watanzania tuta achiwa mashimo.sasa hembu angalie3ni hili[kumbukeni jamaa wanapewa tax relief ya five years .ikiisha nao wamemaliza kila kitu
Hapa ndipo watanzania tutalia na kusaga meno. Nasikia hata yale madini ya uranium kule kusini yamekuwa yanaliwa kidogo kidogo bila hata sisi wenyewe kujua kama tunayo. Cobalt nayo karibu imekwisha wakati watanzania wweing hawajui kuwa tuna kitu kinaitwa cobalt pale kwetu.
 
Huyo sio mtandao, kwa hiyo anajua kuwa at anytime anaweza kubadiishiwa kibao!
Kuwa na raisi wa magurupu namna hii nalo ni tatizo kubwa sana. Yaani sasa hivi anaangalia maslahi ya wale waliomchangia kwenye kampeini (k.m. Gere wa Texas) na wale waliompigia debe (mtandao).

Tutafika kweli?
 
Kichuguu,


3.10% and/or 29% kickbacks = mia kwa mia

Imagine kick back ya 29% kwenye contract ya 50mil USD. Hizi hela hawa jamaa wanazipeleka wapi. Mbona sioni watu wakimiliki Jets au Yatch au hata nisikie ni wafanyabishara wakubwa baada ya kustaafu au wana Shares kwenye makampuni yanayoeleweka duniani...!!!!????
 
Kuna hii kubwa ya Mseveni...
Chini ya mwongozo wa marehemu Nyerere, Uganda walivumbua mafuta mika 10 au 15 iliyopita. Uganda walikuwa hawana hata msomi mmoja ktk maswala ya mafuta. Nyerere akamshauri M7 ayaache mafuta huko chini akawasomeshe kwanza vijana wake. M7 kayaacha akawapeleka vijana kibao nje kusomea kila fani ya mafuta. Hivi sasa wamerudi na Uganda inaongoza Afrika kwa wasomi wa mafuta na wameanza kuweka mikataba ya mafuta hayo na kampuni za nje. Ushauri mkubwa M7 anaupata toka kwa wasomi wake na imekuwa tishio kubwa kwa makampuni ya kigeni kuwa waafrika wameamka. Haaa haaa haaa! wangejua kuwa ni Uganda tu walioweza kufanikiwa hivyo kwa sababu Tanzania tulikuwa na wasomi wa madini kabla ya utandawazi (STAMICO). Leo hii wametupwa wengi wao ndio wapimaji madini mitaani hawana hata kazi. Hawa vijana sijui niwaite wazee tena, wana uwezo wa kulitazama jiwe la madini bila chombo maalum na kukupa bei ya grade yake. Bado tunasisitiza eti elimu elimu hali hatufahamu tufanye nayo kitu gani!
Mikataba inapangwa na wanasiasa, mawakili na wasomi wote toka nje. Tutaacha kuliwa?
Mkapa alikosea toka day one tulipoanza kukabidhi mali zetu kwa wageni na hakuna mbinu ya kupambana nao. Dhahabu ilikuwa dollar 250 kabla ya kuwapa hawa majambazi, leo hii ni dollar 600, bado hatuondoki na kitu. Unaweza hata kusema bora hata tungeweza kuuza kwa hizo dollar 250 sisi wenyewe na uchimbaji wa jembe!...
 
Waziri anasema Wizara yangu imeona umuhimu wa kuupitia upya mkataba huo, kipengele kwa kipengele, kazi ambayo ilianza na inaendelea,” alisema. Shughuli hiyo inafanywa na wataalamu kutoka Wizara za Fedha; Miundombinu; Mipango, Uchumi na Uwezeshaji; na Ofisi za wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Nina mashaka na jinsi serikali inavyoendesha shughuli zake. Yaani badara ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na kufanya utafiti kuhusu mkataba fulani, serikali inasaini kwanza kisha ndio wanafanya utafiti na kukusanya maoni - Bongo Science???? Serikali za nchi nyingine hufurahia kutoa huduma bora kwa watu wake, yetu inafurahia ikiona wananchi wanalialia???
 
Lowassa jitume kabisa!

Huko Nyamongo tunasikia naibu waziri wa madini wa wakati huo(Masha) alitoa vibali kwa barrick ili wawanyangánye wanach ardhi!!

Barrick walishindwa kukubaliana na wanachi juu ya malipo ya ardhi yao. baada ya kuona hivyo hao barrick waliwasiliana na Wizara husika na hapo ndipo huyo waziri alipotoa vbali direct tokea wizarani. Hayo yalisemwa jana nilisia bbc idhaa ya Kiswahili. Alipohojiwa mkuu wa wilaya ya tarime ..Kolimba alikiri kuwa ni kweli! naibu waziri alitoa vibali!! huo ni uchuro wa hali ya juu wa Masha!

Madini lazima yawe na maslahi kwa wananchi-Lowassa

Na Mwandishi Maalumu, Calgary, Kanada

SEKTA ya madini nchini itakuwa ya maana tu kwa wananchi iwapo itajali maslahi ya kitaifa hususan katika uchangiaji wake kwenye maendeleo ya uchumi, imeelezwa.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, katika hotuba yake kwenye mkutano juu ya Maliasili na Maendeleo ya Kiuchumi Afrika na Mchango wa Kanada katika karne ya 21 uliofanyika hapa.

Akifafanua, Bw. Lowassa alisema hata tathmini ya mikataba inayofanywa nchini kuhusiana na sekta hiyo, ina lengo la kuhakikisha upatikanaji mzuri wa madini, lakini pia utoaji huduma bora kutoka katika kampuni zinazochimba.

"Tunataka kampuni za madini kuajiri Wazalendo wengi katika shughuli zao. Tunataka kampuni za madini kuwa na uwazi katika ununuzi wa bidhaa na huduma zao na kuwaomba kuisaidia Serikali katika kuwawezesha wachimbaji wadogo," alisema Waziri Mkuu.

Alisema haitoshi kulalamikia uwezo mdogo walionao wachimbaji Wazalendo, badala yake ipo haja ya kutambua maeneo yenye udhaifu na kuanzisha mipango ya pamoja ili kupambana na matatizo yaliyopo.

Alisisitiza kuwa upitiwaji upya wa mikataba ya uchimbaji madini haufanywi na upande mmoja tu, yaani Serikali, bali ni mchakato unaohusisha pande zote ikiwa ni pamoja na wenye kampuni zilizoingia mikataba.

"Ni kutokana na mtazamo huo, Serikali imeanzisha majadiliano na kampuni za uchimbaji madini kwa nia ya kufanyia marekebisho Mikataba ya Uchimbaji Madini (MDA) ili kuweka mazingira yenye uwiano sawa baina ya Serikali na kampuni husika...ninatia moyo kwamba kampuni mbili za Barrick Gold Tanzania na Resolute Mining (T) Limited, tayari zimeitikia mwito huo," alisema na kuongeza kuwa mazungumzo na kampuni zingine kama vile Anglo Gold Mining yanaendelea vizuri.

Alisisitiza kuwa kwa sasa sekta binafsi haina budi kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji kwenye maliasili, lakini nchi za kiafrika bado zinahitaji kujifunza kutoka majimbo ya Kanada jinsi ya kunufaika na uwekezaji huo.

Alisema kubadilishana uzoefu ni muhimu katika kujenga uwezo katika vyombo vya usimamizi na sheria, kupitia kubadilishana utaalamu na elimu, ambapo Tanzania inatarajia kuona Mamlaka ya Mapato (TRA) ikijifunza kutoka kwa wenzake wa Kanada jinsi ya kusimamia na kukagua kampuni za madini.

"Kuhusiana na wataalamu wa madini na nishati, Kanada ina vyuo vikuu vizuri kabisa duniani...kuwapatia Watanzania nafasi ya kujiongezea maarifa katika sekta hizo litakuwa ni jambo la maana sana," alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mipango mingi ya kutumia raslimali yake katika kuzalisha umeme, ambapo hivi sasa uzalishaji umeme nchini unategemea sana nguvu za maji, ukisaidiana na gesi na katika kipindi kifupi na cha kati, uzalishaji wa ziada utatokana na makaa ya mawe.

Hata hivyo, alisema nguvu ya maji ndicho chanzo nafuu zaidi cha uzalishaji umeme na ndiyo sababu vyanzo kama Rumakali, Ruhudji na Sitigler Gorge, vitapanuliwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yaliyopo.
 
TUNASUBIRI

'Maneno matupu hayavunji mfupa' siye huyu EL aliyewaambia wabunge wafyate mkia kule Dodoma? Hatuhitaji porojo, tunamsubiri akirudi atupe majibu tuliyomuuliza?
 
NIna pendekezo:

Serikali isitishe majadiliano ya mikataba mipya ya nishati na madini mara moja. Hii itaipa serikali nafasi ya kupumua kidogo ili kuone ni mikakati gani ichukuliwe katika mikataba hiyo mipya.

Pili, serikali isitishe mara moja mikataba ya uchimbaji wa madini unaoendelea hivi sasa na iwe tayari kuingia hasara inayotokana na mikataba hiyo. Ikishafanya hivyo, ianze at zero kunegotiate mikataba mipya badala ya kuomba kila kampuni itufikirie. Haitoshi kusema "tunataka mikataba iwanufaishe watanzania". Ni lazima tuweke utaratibu mpya kabisa wa kodi na mapato yanayotokana na madini.

Katika mikataba ijayo mambo yafuatayo lazima yazingatiwe:

a. Kila kampuni inayochimba madini ichangie katika jamii iliyopo ujenzi wa barabara, hospitali, na shule. Aidha kwa kujenga yenyewe au kwa kuanzisha mfuko wa ustawi wa jamii. Haina maana kuwa na kampuni inayotengeneza mabilioni ya shilingi halafu pembeni yake kuna shule isiyo na vyoo!!!!

b. Uanzishwe mfuko maalum wa fedha za Mfuko wa Maendeleo kutoka katika Mapato ya Madini utakaotumika kuendeleza maeneo mengine ya Tanzania ambayo hayana madini. Mfuko huo utachangiwa proportionally na mapato ya kila kampuni mara nne kwa mwaka adjusted for inflation and other economic pressures. Hivyo, mfuko huo ambao utakuwa na wajumbe toka serikalini, NGO, makampuni na muwakilishi wa mabalozi. Mapato yake yatangazwe hadharani na mara mbili kwa mwaka ielezwe mapato na matumizi yake. Kwenye mfuko huo asiwemo Mbunge yoyote!!!

c. Makampuni ambayo hayataki kuingia mikataba mipya na serikali wako huru kuondoka na serikali mara moja itangaze hasara itakayopata na kukaribisha kampuni mpya ambayo iko tayari kuingia hilo deni na kuchukua nafasi ya kampuni iliyoondoka. Ama sivyo, acheni madini yetu yakae hapo hadi wenyewe tutakapokuwa na uwezo wa kuyaendeleza!!!!!!
 
I'm sick, sick tired of all these rhetoric talk of our top leaders. Talk, talk, talk and more talk. That's ALL they can do. They should be entered in the Guinness book of records, starting with JK.
 
Ni usanii mtupu. Mnaosubiri fundamental changes katika hii mikataba endeleeni kusubiri. Mikataba inaandikwa na Barrick inabarikiwa na serikali.
 
Compare this to any of TZs mining companies board:

attachment.php


Debswana - Board of Directors

wazawa tupu; i don't mind hata kama ni wa serikali...

sasa tazama

attachment.php

attachment.php

attachment.php



TanzaniteOne - The largest and most advanced miner of the rare tanzanite gemstone

Wanamuweka mbongo mmoja ambaye watam'control
 

Attachments

  • Botswana.jpg
    Botswana.jpg
    67.2 KB · Views: 119
  • Tanzanite1.jpg
    Tanzanite1.jpg
    87.6 KB · Views: 113
  • Tanzanite2.jpg
    Tanzanite2.jpg
    96.6 KB · Views: 108
  • Tanzanite3.jpg
    Tanzanite3.jpg
    99.7 KB · Views: 105
Nchi kama botswana ina watu wasiozidi 2 million wanakuwa na uzalendo wa namna hiyo sisi Bongo kazi ya viongozi ni kuiba.

JK kama anaogopa hatuwezi kumchagua next term tunahitaji kiongozi mwenye courage.
 
Kijasti,
Na huyo Mtanzania mmoja kishakunjwa mfukoni siku nyingi.
 
Wewe Kijasti-utaniliza!

Wacha: Si mpaka tuweze ndugu yangu. Wadanganyika hapo walipo wanapiga makofi kwa sana tu!
 
Back
Top Bottom