Mikao hii yote ya maombi ni halali na ina heshima sawa mbele za Mungu. Sio lazima upige magoti au usujudu katika kuomba

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,371
Unaweza

1: KUOMBA UMESIMAMA NA KUNYOOSHA MIKONO JUU.

2: Kuomba umelala kitandani kama hujiwezi kama mfalme Hezekia.

3: Kulala chini kifudifudi au kulala kama Yesu gethsemane.

4: Kuomba umeketi kama daudi.

5: Kuomba ukiwa katikati ya watu umesimama kama Nehemia, walio na wewe wasijue kama unaomba.

6: Kuomba umepiga magoti

7: Kuomba umesujudu

8: Kuomba umeinamisha kichwa kimeingia katikati ya magoti ukiwa umesujudu kana nabii Eliya.

Omba ukiwa chooni, Barabarani, unaendesha gari, kitandani, ofisini, jela, safarini,

Kimsingi kila utakapokuwepo panakidhi viwango vya wewe kumuomba Mungu. Hakuna style au mkao wa maombi ambao ni mtakatifu kuliko mwingine. Mungu anaangalia mkao wa moyo wako.

Hata kama utaomba umepiga msamba ikiwa moyo wako ni wa jiwe na tukutu usionyenyekea utakuwa huombi bali unafanya joging.
 
Kuna wale wa matendo ya mwilini wana kitabu cha kuwaongoza kimwili wajikunjeje, wainame vipi wanaposali sala zao. Wamekariri hivyo
Watu wanakariri. Na hii inawazuilia fursa zao nyingi za kuongea na Baba yao wa mbinguni.
 
nazani lazima kuna taratibu zimewekwa

Kama kuwa safi ili usiwe najisi na uweze kuingia malangoni mwake

Na dhabihu tuna toa iliyosafi na kupendeza Mungu na kwa taratibu zilizo wekwa

Wengine walikatazwa kuomba kwa kupiga kelele na wengine ni kinyume chake

Maandiko nazani yametoa fursa hizi kwa taratibu maalum kama vile waislam kula nguruwe pale inapo bidi japo ni haram na machikizo kwao

Una weza kuomba ukiwa una chepuka kitandani lakini sizani kama tumefundishwa kuchepuka

Kila jambo lina taratibu zake, ni kama Ibada ya Jpili, jmosi Au ijumaa kusalia kwenye madhabahu ni nzuri zaidi japo ukatazwi kusalia sehemu nyingine tofauti

Wakusanyikapo.... basi na yeye yupo!

Tuendelee kumcha Mungu bila kuchoka, nakubariana na wewe kusali hakuna style lakini kuna taratibu kujinyenyekeza zaidi na sio kujikweza nk...
 
binafsi sijawahi kumuogopa Mungu.namheshimu sana,najua mipango yake kwangu haihitaji sekunde kutimia wala dkk,nacheka sana mtu anapoamua kujikita kwenye sheria katika kumjua na kumuabudu Mungu.akidhani anafanya mapenzi yake,kumbe mapenzi ya aliyeziandika sheria hizo.

unaamua kuamini sala yako imepokelewa sababu ulisali huku unalia ama umesujudu.

unaamini umehesabiwa haki sababu umehudhuria ibada zote 5 au unakesha kanisani

Mungu sio mahakama anayefurahishwa na asiyevunja sheria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom