Miji suitable kwa City Trams (treni ndogo za mjini)

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,508
19,320
Laiti kama siku moja tutajilipua, tukajenga miundombinu ya trams, ambayo inaweza kuwa humuhumu kwenye barabara zetu za jini, usafiri utakuwa rahisi zaidi. napendekeza maeneo haya yazingatiwe, hata hiyo pesa ya bilioni 300 anatoa kwa ajili ya darala la jangwani, inaweza kutosha.

1. Dodoma iwepo tram toka chamwino ipite katikati ya mji hadi msalato.

2. DSM iwepo tram toka posta hadi kibaha, posta hadi gongo la mboto, posta hadi karidi na bagamoyo.

3. mwanza, toka airport hadi misungwi

4. arusha miundombinu na milima sio rafiki.

5. iringa, toka nduli hadi mwangata

7. mbeya toka nsalaga hadi sokomatola

8. morogoro ni tambarare, wachague tu popote.

9. Tanga tambarare hadi raha, itafaa sana.

10. kigamboni toka pale ferry hadi anakoishi yeriko nyerere

hizo ni kwa kuanzia tu. tram zinatumia umeme, south africa walishawahi uwa nazo tangu zamani sana sijui kama watakuwa walizibomoa, ila kwa nchi za ulaya, hakuna nchi isiyo na trams, wengine zile za zamani kabisa bado zinatumika. Algeria na Morocco na misri trams wanazo tena kama za ulaya.

Fw9nCq_WwAEYquu.jpeg
 
sema sasa, shida mabodaboda yalivyo na bange, itabidi polisi wakae na fimbo za kuchapia mgongoni. bila kusahau bajaji.
 
Mwendokasi iwekwe trams Tu...baasi...
mwendokasi iende njia fupi hizo kama vile ubungo buguruni, hizo za mkato, ila njia kuu zote waweke trams. kazi ingekuwa kubadilisha vichwa tu mabehewa hata hapa wangeweza kutengeneza, kama wanatengeneza mabodi ya mabasi yanaenda hadi mkoani, ukipata kichwa utashindwa kutoa tenda hapahapa bongo kweli?
 
Hizi tram ni tofauti na treni?
ni tren hizo hizo ila hazitembei kwenye mataluma yaliyoko juu kama hizo reli za SGR, wanakuwa kama wanachimba kidogo tu humohumo barabarani na ile reli wanaizika kwenye lami, mifereji tu inaonekana ndio inapita. na utofauti wake haibebi mizigo mizito kama makontena, ni watu tu, ila kwa juu kuna connector ya umeme inapotembea inakuwa inagusa na kupata moto wa kuendelea. kama ilivyo kwenye picha. tungesema ni trendi ndogondogo za mjini.
 
Wajapan wakipewa tenda...fasta tu
 
Wajapan wakipewa tenda...fasta tu
wajapan, korea kusini, brazil, wafaransa au wajerumani. hawa wote wapo vizuri mno.na hiyo kiti kwao ipo kwao hata kabla hatujapata uhuru huku bongolala. na kwa waliotembelea nchi hizo, usafiri huo ndio unasaidia sana watu wa kipato cha kawaida, na hata wenye kipato kikubwa wengine wanaacha gari home wanapanda hayo kwenda kazini.
 
Kama madereva wameshindwa kuheshimu njia za mwendokasi kwenye Tram kila siku mtakuwa mnazika.Mtu atambiwa kuna sheria za ku overtake tram,wataanza kuleta siasa zao sijui ni gari la serikali,sijui ni jaji,bodaboda nae ataendeleza ujuaji wake..Haya zileteni tuanzishe na biashara ya masanduku ya kuzikia.
 
ni tren hizo hizo ila hazitembei kwenye mataluma yaliyoko juu kama hizo reli za SGR, wanakuwa kama wanachimba kidogo tu humohumo barabarani na ile reli wanaizika kwenye lami, mifereji tu inaonekana ndio inapita. na utofauti wake haibebi mizigo mizito kama makontena, ni watu tu, ila kwa juu kuna connector ya umeme inapotembea inakuwa inagusa na kupata moto wa kuendelea. kama ilivyo kwenye picha. tungesema ni trendi ndogondogo za mjini.
Sasa we mangi umeme unao wa kusukuma hayo matrams? SGR kila siku wanasema wataanza kutoa huduma kesho toka 2017 mpaka leo kesho kesho kumbe shida umeme hautoshi
 
Kama madereva wameshindwa kuheshimu njia za mwendokasi kwenye Tram kila siku mtakuwa mnazika.Mtu atambiwa kuna sheria za ku overtake tram,wataanza kuleta siasa zao sijui ni gari la serikali,sijui ni jaji,bodaboda nae ataendeleza ujuaji wake..Haya zileteni tuanzishe na biashara ya masanduku ya kuzikia.
uzembe wa madereva hauwezi kutufanye tusifanye maendeleo. hilo ni suala la kujipanga tu kufanya watu watii sheria. nenda rwanda ona kama kuna mambo kama hayo, kama rwanda wameforce watu wawe wastaarabu, sisi tunashindwa nini?
 
Sasa we mangi umeme unao wa kusukuma hayo matrams? SGR kila siku wanasema wataanza kutoa huduma kesho toka 2017 mpaka leo kesho kesho kumbe shida umeme hautoshi
umeme tunajenga nyerere dam, umeme pia tunaweza kujenga wa gas, na hata hizo tram zingine vichwa vyao huwa vinakuwa vinachaji na kuproduce umeme. unawezakuta unatumia umeme kidogo tu.
 
uzembe wa madereva hauwezi kutufanye tusifanye maendeleo. hilo ni suala la kujipanga tu kufanya watu watii sheria. nenda rwanda ona kama kuna mambo kama hayo, kama rwanda wameforce watu wawe wastaarabu, sisi tunashindwa nini?
Maana yake madereva wote waliopo barabarani itabidi warudi shule kujifunza kuendesha kwenye barabara pamoja na train. Kupata driving licence ya EU kuendesha kwenye njia za Trams pamoja na kwenye freeways/Expressways ndio test ambazo mtu anaweza kurudia mara nyingi
 
wala sio hivyo. haikimbiii kwa spidi ya treni, inatembea mwendo sawa tu na wa wa magari, ina honi pia, na mara nyingi wao wanakuwa upande wao hasa pembeni ya barabara. kama unaweza kuendesha gari yako ukapishana na basi la shabiby au new force hapohapo city centre, utashindwaje kuendesha pamoja na trams? na mbona ulaya wanaendesha tu kawaida tu yaani. nenda hata youtube uone zinatembeaje.
 
Youtube kufanya nini wakati ni muda mfupi nimetelemka kwenye Tram?
 
nilidhani huzijui. kama umetelemka kwenye tram, unashindwaje kuelewa kwamba sio kitu kigumu kutembea humuhumu barabarani? au nini kilikuwa kigumu kwako? kuna traffic ligh,kuna michoro na kila kitu barabarani na inatembea mwendo wa kawaida tu kwasababu inaco-exist na raia wengi mtaani, ugumu utatoka wapi sasa hapo.
 
Back
Top Bottom