Demokrasia ya unapoishi (Local Democracy) huanzia mtaani, kijijini mjini, wilayani hadi mijini kufikia Demokrasia kamili

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Pamoja na mambo mengine yote siasa ni majadiliano, au mgogoro wa hoja baina ya watu, vyama katika kutafuta kutwa madaraka au mamlaka.

Mtazamo wa mwanafilosofia aitwae Aristotle kuhusu siasa anamfananisha mwanasiasa na fundi kwamba mwanasiasa ni mtu alie na elimu wezeshi (practical knowledge) na fundi ambae ana hila (craft) katika mfumo wa elimu tija.

Hivyo ukienda kinyume utaona kuwa mwanasiasa aweza kutunga sheria kandamizi na kufatuta namna ya kuiidhinisha kiaina (justification) kwa hila kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi au kwa malengo fulani.

Hapa nafikiri unaesoma utakuwa umenileewa au siyo?

Maana kuna masuala kama tozo zilizopitishwa hivi karibuni kuna watu wamefika hadi katika runinga kuhakikisha "the message is sent and delivered without nock-back".

Leo tuangalie neno demokrasia na chanzo chake.

Mimi binafsi nimeishi nje ya nchi kwa muda mrefu kabla ya kurejea Tanzania, hiyo kauli huwa siifichi kwani inasaidia kuweka ajenda yangu sawa kwamba naiongelea masuala ambayo ni "genuine".

Kuna masuala nimegundua yatachukua miongo kadhaa ili kuweza kushika nafasi ndani ya mioyo ya watanzania wenzangu.

Moja ya masuala hayo ni uelewa wa neno demokrasia na wapi ianze.

Hii yaitwa demokrasia ya eneo unapoishi au "Local Democracy".

Neno demokrasia ya unapoishi au "Local Democracy" ni ile demokrasia ambayo hupatikana katika eneo ambalo mtu anaishi iwe mtaani, kijijini, mjini hadi kwenye manispaa na jiji lote.

Sasa katika eneo unaloishi yaani mtaani kwa wenzetu wazungu huhakikisha kuna njia ya wenda kwa miguu, njia hiyo ni safi na haina wadudu, takataka na kimazingira yaridhisha.

Kisha huhakikisha kila mtaa una jina, barabara ni ya lami na haina mashimo isipokuwa kama barabara hiyo ni private yaani ni njia binafsi, huduma zote kama maji, simu na internet zipo katika njia hizo na zote zaweza kuingizwa katika nyumba endapo mwananchi nahitaji huduma hiyo.

Endapo mambo haya yana kasoro basi wananchi kupitia demokrasia ya mtaa watahakikisha taarifa zinafika kwenye ofisi ya manispaa au wilayani na tatizo hilo litashughulikiwa kwa uaharaka na ufanisi.

Demokrasia ya eneo unaloishi inazuia mtu kujenga hovyo nje ya nyumba yake kuzidi viwango vilivyowekwa na sheria ya mipangop miji. Kwa mfano wataka kujenga uzio kuzunguka nyumba yako ni lazima uzio huo usizid mita 4 au 6 kwenda juu isipokuwa kama tokea zamani ilikuwa hivyo kabla ya sheria haijapitishwa.

Pia mtu akitaka kujenga chumba cha ziada au "extension" ni lazima aombe kibali na watu wa mipango miji waje kuhakikisha wajenja uzuri na huzidishi mita 4. Ukizidisha mita 4 majirani mtaani wataandika barua kwa "Local Democracy" kulalamika watasikilizwa na utaambiwa ufanye marekebisho.

Nguvu na uwajibikaji wa vyombo vyote vilivyopewa madaraka na majukumu katika eneo husika ni sehemu ya demokrasia hii ambayo (isipokuwa kwa sababu maalum) inaweza kuwashirikisha madiwani, maofisa wa kata, watendaji wa serikali za mitaa hadi kwa wabunge.

Kwa mfano, mtu binafsi ataka kujenga hoteli, au kufanya "developments" zingine kama nyumba za kupangisha ni lazima aweke tangazo, apeleke barua ya proposal yenye kuambatana na michoro na local democracy watapewa "copy" kwa ajili ya kupitia kuona kama kuna makosa yoyote (scrutinisation) na asili ya eneo "Heritage" yalindwa bila kuingiliwa.

Demokrasia hii yataka watendaji wote wawe na ofisi kuanzia diwani hadi mbunge wa eneo na awe na siku maalum za kukutana na wananchi walomchagua kutatua matatizo mbalimbali.

Pia mbali na sheria zilizopo demokrasia ya eneo inazitaka manispaa kuhakikisha mwananchi anajulishwa kwa barua mabadiliko yoyote ya kodi ya maendeleo, mchanganuo wa kodi ulivyo unaoonyesha fedha zinavyogawiwa kwa polisi, zimamoto, huduma za mahispitali na huduma za jamii.

Demokrasia hii yahakikisha huduma zote muhimu zipo katika eneo husika hospitali, vituo vya mabasi, vituo vya polisi, masoko, na huduma zingine kama za starehe ni lazima ziwe mbali na makazi ya watu.

Huduma kama masoko, maduka, kumbi za starehe, na magulio ni lazima ziwe mbali na makazi ya watu. Masoko makuu ni lazima yajengwe kisasa na yasije kushika moto au kufanyiwa hujuma kama soko letu la kariakoo ambalo ni moja ya alama ya za utaifa wetu.

Kila wilaya au manispaa ni lazima iwe na soko lake, mpangilio na mji na hakuna wachuuzi barabarani bila kuwa na kibanda maalum na walipia kodi, huduma za maeneo maalum ya kupumzikia na vyoo vya umma vyenye mvuto.

"Local Democracy" yaleta uwezo wa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na uhuru wa majadiliano katika eneo husika kuweza kufanya shughuli zao kwa uhuru kama kutaarifu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa, uhalifu, uchumi, biashara, na masuala mengine mengi.

Haya ni mambo ambayo wenzetu waliyaanza miaka zaidi ya 200 ilopita maana waweka picha zao kuonyesha miji yao ilivyokuwa mwaka 1750 au 1800 na ulivyo sasa.

Camo'n guys ngoja tuanze, Tanzania tuna baadhi ya mambo niliyoeleza lakini si katika ujazo unotakiwa. Tunao baadhi ya viongozi wenye maono ambao wanaweza kutufikisha katika viwango vya kimataifa katika kuijenga nchi yetu.

Hapa Dodoma bado naona ujenzi wa baadhi ya miundombinu unasuasua na hata ofisi za mabalozi zinakwenda taratibu.

Mbona mwarabu (Saudi Arabia) au Myahudi wamejenga jangwani?

Gaddaffi aliijenga Libya jangwani na Libya ikawa nusu Ulaya kabla ya kuvurugwa? Sisi twashindwa ni?

Hivo kama baadhi ya viongozi wanavyodai kuwa tunaweza kugeuza miji na manispaa zetu kuwa Toronto au Dubai lakini watambue kuwa miji hiyo haikujengwa kisiasa bali kwa nia ya dhati na kwajili ya kizazi kijacho, au viongozi wetu hawajali vijazi vijavyo na wanatengenezea vizazi vyao pekee?

Hapa naweza kuungana na mwanafalsafa mwingine Niccolo Machiavelli ambae kuhusu siasa aliamini kuwa ili jamii iweze kuwa imara na yenye usalama ni lazima rushwa na ufisadi iwe ndio mbiu.

Machiavelli anaeleza katika kitabu cha Prince kwamba, umma wa watu na sekta binafsi au wafanyabiashara ni vitu ambavyo ni lazima kutenganisha. Hivyo kama ufidasi unapigwa kwa kiwango cha kutisha basi jamii haiwezi kung'amua kirahisi maana ni siri kati ya watawala na watawaliwa.

Jambo la msingi ni kwa viongozi wetu kuhakikisha wanawawezesha wananchi katika kuimarisha "local democracy" wananchi waelewe haki zao za msingi katika maeneo yao wanoishi.

Wananchi wajiulize je, diwani anawajibika, mbunge anawajibika? je, barabaraba ni za lami? hazina mashimo, kila nyumba ina umeme, huduma za hospitali zipo karibu nao? huduma za polisi, zimamoto, usafiri wa uhakika upo hadi karibu na mwanachi?

Ila jambo la msingi ni hili la demokrasia ya eneo unapoishi, na tukianza na hili neno litasambaa na kila mwananchi atakuwa na sauti ya kuhoji kwa nia ya kuleta chachu ya maendeleo.

Pia itasaidia kutengeneza ajenda kwa nchi nzima kuwa na dira inayoeleweka ambayo itatufikisha nchi ya maziwa na asali.

Hapa bado hatujazungumzia masuala kama wananchi kudai kura za maoni na hatimae kubadilisha vipengele kwenye katiba.

Wala hatuzungumzii kudai tume huru ya uchaguzi maana mambo haya mawili yanafanana lakini yanaanzia kwenye ngazi ya chini.

Wananchi wanapaswa kuwapa "pressure" wabunge wao majimboni kuwa wanataka mabadiliko katika katiba na hii itachangiwa zaidi na kumpa kura mbunge wa upinzani.

Idadi ya wabunge wa upinzani ikianza kuongezeka bungeni itatishia ustawi wa chama kinachotawala kwa kuona kuwa kinakosa nguvu ya ushawishi.

Wabunge wa upinzani wakizidi theluthi mbili ya wabunge wote bungeni wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kuwa baadhi ya vipengele vya katiba ni lazima vibadilishwe.

Baadhi ya vipengele hivyo ni namna ya kuipata tume huru ya uchaguzi, teuzi za raisi (khasa nafasi nyeti ziidhinishwe na bunge), Mameya na wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi na si madiwani. wakurugenzi wa maendeleo wasiteuliwe na raisi bali maeneo husika kwa kushindanishwa kulingana na uwezo wao.

Bila mkakati huu namba moja wa kupata wabunge wengi wa upinzani hakuna kitu na huu ndo ukweli.

Mikakati mingine hufuata baada ya hapo ila "local democracy" ndio iwe habari za mjini.

"Local democracy" yaleta afya ya akili na afya ya maono.
 
Richard bandiko refu sana na liko kishuleshule zaidi. Ni rahisi, demokrasia yetu ilikuwa inazidi kukua, na chama kilichoko madarakani kilikuwa kinazidi kupata pressure. Lakini ifahamike ccm ni chama kilichoanza kuchoka, hii ndio ilipokea yule rais aliyeaga dunia kutumia madaraka yake vibaya kuchafua demokrasia yetu.

Alichokifanya ni kuzuia ushindani wa kisiasa dhidi ya chama chake ikiwemo kunajisi chaguzi zetu, matokeo yake tumepata viongozi walioko madarakani kisheria lakini wasio na uhalali wa umma.

Wanafanya kuiridhisha serikali, na sio kuwakilisha wananchi. Matokeo yake ajenda zinazofanyiwa kazi ni za viongozi na sio za wananchi.
 
Richard bandiko refu sana na liko kishuleshule zaidi. Ni rahisi, demokrasia yetu ilikuwa inazidi kukua, na chama kilichoko madarakani kilikuwa kinazidi kupata pressure. Lakini ifahamike ccm ni chama kilichoanza kuchoka, hii ndio ilipokea yule rais aliyeaga dunia kutumia madaraka yake vibaya kuchafua demokrasia yetu. Alichokifanya ni kuzuia ushindani wa kisiasa dhidi ya chama chake ikiwemo kunajisi chaguzi zetu, matokeo yake tumepata viongozi walioko madarakani kisheria lakini wasio na uhalali wa umma. Wanafanya kuiridhisha serikali, na sio kuwakilisha wananchi. Matokeo yake ajenda zinazofanyiwa kazi ni za viongozi na sio za wananchi.
Umenene vyema sn mkuu
 
Richard bandiko refu sana na liko kishuleshule zaidi. Ni rahisi, demokrasia yetu ilikuwa inazidi kukua, na chama kilichoko madarakani kilikuwa kinazidi kupata pressure. Lakini ifahamike ccm ni chama kilichoanza kuchoka, hii ndio ilipokea yule rais aliyeaga dunia kutumia madaraka yake vibaya kuchafua demokrasia yetu. Alichokifanya ni kuzuia ushindani wa kisiasa dhidi ya chama chake ikiwemo kunajisi chaguzi zetu, matokeo yake tumepata viongozi walioko madarakani kisheria lakini wasio na uhalali wa umma. Wanafanya kuiridhisha serikali, na sio kuwakilisha wananchi. Matokeo yake ajenda zinazofanyiwa kazi ni za viongozi na sio za wananchi.
Kwa weye waona hii imekaa kishuleshule lakini kwa mwananchi mpiga kura na hohehahe ni elimu tosha.

Ndo maana nimetoa hii kwa angazi ya chini kabisa mwananchi kuelewa namna anavyoweza kuanza mchakato chini kabisa.

Ni kjama vile jamii yajihitaji kutafakari na kujijenga upya.

Yaani kama vile mtu yupo Kwa Mpalange asoma huu uzi na ana bando la kutosha.
 
Kwa weye waona hii imekaa kishuleshule lakini kwa mwananchi mpiga kura na hohehahe ni elimu tosha.

Ndo maana nimetoa hii kwa angazi ya chini kabisa mwananchi kuelewa namna anavyoweza kuanza mchakato chini kabisa.

Ni kjama vile jamii yajihitaji kutafakari na kujijenga upya.

Yaani kama vile mtu yupo Kwa Mpalange asoma huu uzi na ana bando la kutosha.

Wananchi wa nchi hii tunawajua, hiki ulicholeta hapa ni nadharia zisizo na uhalisia wowote.
 
Wananchi wa nchi hii tunawajua, hiki ulicholeta hapa ni nadharia zisizo na uhalisia wowote.
Kwani weye si mwananchi?

Kwanini useme "wananchi wa nchi hii tunawajua"?

Wasema hivyo kama nani?
 
Acha porojo za kishuleshule bro.
Wewe nakuelewa waangalia njia moja tu huna njia zingine.

Kwa kiingereza twasema, "You are not as smart at you want to portray yourself".

Kwa kuwa tayari una "perception" yako kichwani na imeimarika basi huwezi kufikira njia yoyote mbadala.
 
Wewe nakuelewa waangalia njia moja tu huna njia zingine.

Kwa kiingereza twasema, "You are not as smart at you want to portray yourself".

Kwa kuwa tayari una "perception" yako kichwani na imeimarika basi huwezi kufikira njia yoyote mbadala.
Seems you think you are smart than you are! Anyway I respect your school ideas.
 
Watu wakipiga kelele za Katiba Mpya huwa hamuwaelewi, hampendi kusikia, lakini kimsingi ili yote uliyoandika hapa yatekelezeke, basi lazima Katiba Mpya iwepo.

Nasema hivyo nikiegemea uliposema "viongozi wanawawezesha wananchi katika kuimarisha local democracy" bahati mbaya kwasasa hii local democracy kwa viongozi wetu haina maana kwao, huo muda wa kuwaelimisha wananchi watautoa wapi kama wana uhakika wa kupewa ushindi bila jasho (kura feki).

Hapa taka usitake, lazima yatengenezwe mazingira yatakayomfanya huyo kiongozi "wakuwawezesha wananchi" ajione ana jukumu/wajibu wa kufanya hivyo, isiwe kama anafanya kwa kupenda/kujisikia kama ilivyo sasa.

Hayo mazingira ndio yatatengenezwa kwa uwepo wa Katiba Mpya itakayoainisha wajibu na mipaka ya kila kiongozi katika kutimiza majukumu yake, hii Katiba tuliyonayo na tume ya uchaguzi vinawafanya viongozi walioko madarakani wawe wazembe sababu wana uhakika wa ushindi.

Viongozi kutotambua majukumu yao kwa sababu za kulindana ndiko kunasababisha huko Dodoma ujenzi wa miundombinu kwenda taratibu, hawabanwi na sheria, lakini mbele kidogo ukakosea kwa kutoa mfano wa Libya ambayo demokrasia yake haifanani na ya kwetu, kule ilikuwa ni amri ya mtu mmoja ndio sheria.
 
Back
Top Bottom