Mijadala ya Dini ijikite kuelimisha waamini wa Dini husika, Vitumike vitabu vya Dini husika kukazia maarifa ya Dini husika ndani ya Mafundisho husika.

bhachoneghe

Member
Feb 9, 2017
54
36
Mafundisho ya Dini yenye uwalakini.
Kuna Mafundisho ya Dini yamekua na mapungufu.

Muislam hufundishwa na kuelimishwa kupitia Quran, Imani ili ijitetee yenyewe hauhitaji kufundisha mapungufu ya Ukristo
(Ku ingilia Mafundisho ya Ukristo na misingi ya Iman yake) nikuonesha Imani husika inayo fundishwa haijakamilika ili ikamilike lazima ipitie mabegan Kwa Ukristo.


Ukristo hufundishwa na kuelimishwa Imani ya Ukristo Kwa kutumia Bible, ukitumia Quran kufundishia Ukristo Kwa njia chanya au hasi Bado inaonesha Iman husika haija jikamilisha.

Dini iliyo sahihi Nijambo la Imani ya mfuasi bila kushurutisha mwingine aamini unacho amini,Ukianza kulazimisha Imani Yako ionekane sahihi Kwa kukosoa Imani nyingine nidalili za uvunjifu wa Amani.

Misingi ya Iman zao ipo tofauti (Ukristo upo kwenye msingi wa Yesu kama ndo kielelezo Cha utimilifu wa Imani kupitia Mafundisho yake. Wanaamini ni mwana wa MUNGU , Na anaitwa YESU nasio jina lingine, Njia alivyo patikana, njia yake ya kuondoka ulimwenguni , Na wajibu wake akirudi Ukristo una mtazamo wake na Uislam una mtazamo wake.

Kila mtu afundishe na kuamini yake (Tafsiri ya Nguruwe na ngamia kwenye agano la kale kwenye Bible wote wanyama ni Haramu, kupitia agano jipya wanaliwa na baadhi ya wengi wakristo lakini Kwa Uislam Bado ni Najisi).

Selikari iingilie Kuweka mipaka ya kuingilia Iman za wengine (falagha za Imani). Ili tuwe na tafsiri ya mipaka ya Iman kwenye Jamii, mfano mtoto anamilikiwa na Imani au wazazi? Au Haki ziangalie Imani au Muundo wa undugu damu.
 
Kwa upande wa biblia huko hakuna shida watu wanafundishwa filosofia/falsafa za maisha hapa duniani. Mambo ya kufanya kazi na malezi ya familia/ndoa na mengineyo yanayojenga utu na kuthamini wengine hata kama hawaamini ukristo. Kuna suala la upendo na amani miongoni mwa jamii hufundishwa, kuna uadilifu na usafi. Biblia haina mkururo mgumu kuelewa mafundisho yake yako wazi
 
Jumapili moja hivi karibuni kuna muumini mmoja alikuwa anatoa shukrani kanisani kama ilivyo kawaida kushukuru jambo unaloona ni Mungu amekutendea. Jamaa alikuja na ndugu zake wengi ambao ni waislam wakashiriki ibada ya kikristo mwanzo hadi mwisho na walikaribishwa kwa amani na upendo wakapewa nafasi ya kujitambulisha majina yao na wapi wanatoka. Cha ajabu nilichoshangaa waliweza kufurahia ibada ya sifa na kuabudu kana kwamba ni wenyeji. Mwisho wa ibada walioondoka kwa amani na upendo huku wakiwa kwenye mavazi ya dini yao na hakuna aliyewashurutisha waokoke wampoke Yesu Kristo awe Bwana na Muokozi wa maisha yao. Je huko msikitini mkristo anaweza akaingia na kuswali kisha akatoka baada ya ibada bila kubughudhiwa? Mafundisho ya biblia hayana ubaguzi yanataka toba na unyoofu wa moyo na upendo kwa wote
 
Back
Top Bottom