Miezi mitatu nikiwa Jiji la Mbeya. CHADEMA na Sugu wasahau ubunge

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
Ndugu Zanguni leo ndio nimehitimisha majukumu yangu ya mradi unaohusisha mambo ya Jamii kupitia shirika lisilo la kiserikali la WORLD VISION. Pamoja na mengine nimekuwa nikikaa kwenye vijiwe, kukutana na wakazi wa Mbeya mjini na viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini na waumini wao.

Kwa kweli kwa sasa CHADEMA hawana umoja wala muunganiko wa kisiasa mfano hadi sasa kuna mgogoro mkubwa wa mwenyekiti wa CHADEMA wa jimbo la Mbeya mjini na mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya kamanda China wa China ambao hawaivi hata kidogo ambapo mwenyekiti ametangaza kumuondoa Mwenyekiti wa jimbo.

Kuhusu SUGU amepoteza mvuto katika jiji la Mbeya ambapo wakazi wengi wa mbeya (wanyakyusa) hawana muda naye tena ambapo wamefurahishwa na kumpata Binti yao Spika wa Bunge Hivo wamesema hawana muda na mpinzani tena.
 
Wewe CCM weka tume huru ya uchaguzi ndiyo uandike huu ujinga wako hapa
 
Sugu aliposhinda tume ilikuwa huru?Mkishinda hatusikii hoja ya tume huru mkigaragazwa tume haikuwa huru.
 
Jambo moja umesahau ama umefanya makusudi ni ukweli kuwa Mbeya mjini wakazi wake sio Wanyakyusa, lile ni eneo la Wasafa na Wanyakyusa wamefanya kukarinishwa tu. Huko Tukuyu na Kyela ndiko kwa Wanyakyusa. Kuhusu mgogoro hilo ni jambo la muda tu. Je ulifanikiwa kupima imani ya wananchi wa Mbeya kwa CDM?
 
Umeandika ujinga mtupu, waambie maccm wenzako waweke mazingingira rafiki kidogo tu ya uchaguzi angalau kama hawamu ya nne uone mziki wake.
 
Ndio maana Sugu kaamua kurudi kwenye mziki,hili lipo wazi
 
Aisee,Mbeya hali kumbe ni mbaya sana kwa muwekezaji Joseph Mbili a.k.a Sugu.Duh!
 
Reactions: Tui
World Vision zamani walikuwa wanaajiri watu smart sana au wewe ni muosha vyombo?
 
hiyo takataka ambayo imeshindwa kushawishi ikiwa naibu spika angalau Mbeya ipate barabara dual carriageway,huyo kibibi akisimama hata na diwani wangu hapa Iyela hawezi kupata kura elfu kumi.
 
Hongera mwananchi wa juu, ila Sasa ninaombi Moja kwako na kwenu, uwanja wa siasa uwe huru, na je utafiti wako uliweza kubaini siasa zisizo na usawa, na je uliweza kubaini kama huo mgogoro SI wa kutengenezwa kama ule wa COVID-19 na je utafiti wako ni huru na hauna mrengo unaoegemea, yangu ni hayo tu ndugu raia matawi🤔.
 
Mpumbavu sana wewe
 
ndicho walichokutuma ukafanye hao WV?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…