Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,515
- 6,489
Kwanza angetafuta hela za kupunguza wafanyakazi na kuwalipa mafao, maana hukurupuki tu na kupunguza wafanyakazi. Pili serikali ilipe baadhi ya madeni ya shirika hadi lifikie kiwango cha kukopesheka na tatu walipatie mtaji wa angalau ndege mbili mpya za size ya Boeing 737. Baada ya hapo atafute CEO kwa competitive recruitment na sio kwa style ya kuokotana, baada ya hapo nitasema ndaga fijo malafyale wewe ni jembe. Lakini kwa anayoyafanya saizi anajiaibisha tu na kuonekana vuvuzela kama Nape na ataondoka 2015 shirika liko vile vile. Maana hata akakae mwenyewe kuwa CEO kwa matatizo ya sasa ya ATCL atachemka tu.
Hapo red; ona sasa shirika linatengeneza medeni ya hovyo bila serikali kujua halafu wakishindwa kulipa wanaleta hazina serikalini ilipe, hii haikubaliki lazima serikali iwe inajua na kuridhia huo ukopaji wa madeni.