Miezi mi3 kwa ATCL kujiendesha ni uendawazimu wa Mwakyembe

Njowepo mimi nafikiri hawa dawa ni kuwapa deadline wakishindwa ku-deliver within the time frame or limit you get them fired nashangaa huyu jamaa analalamika hiyo miezi 3 that's the kind of people we have, 35 years and the airline hasn't done shit..

Tatizo langu sio miezi mitatu, hata mmoja ungetosha kama tatizo ni dogo. Kwa msomi kama Mwakyembe angekuwa mtu sahihi kuokoa shirika angetoa tamko sahihi. Wewe mtoto wako ameanguka ndani ya shimo futi ishirini unaenda na kamba futi mbili kumtoa si uendawazimu huo?? Una kitambaa cha kutosha kushona chu.pi halafu uanenda kwa fundi unamwambia akushoinee kanzu si uendawazimu huo? Nyie wenyewe mliona mwaka jana hawaja jamaa na serikali yao walipitisha bajeti ya trilioni 13.5 mkawasifia kila kona lakini wameishia kutekeleza trilioni 8 tu. Kama wakunyumba anataka kuokoa shirika alinunulie ndege zake walau hata mbili then atoe deadline.
 
Last edited by a moderator:
Mikakati ya 4.9 bilioni kuokoa shirika la ndege linalohitaji bilioni 300. What is juhudi by the way? Viongozi wa aina ya Mwakyembe wenye kulalamika bila kutoa suluhisho mnatakiwa kuanza kuwakataa kama mnataka nchi iendelee.
Bil 300 ni zilezile figer za kifisadi zinazotokana na upembuzi yakinifu wa kifisadi! Kumbe ulitaka waziri afanye nini sasa kama sio hizo hatua alizoanza kuchukua? Hebu tuambie wewe ungefanyaje?
 
Kwanza angetafuta hela za kupunguza wafanyakazi na kuwalipa mafao, maana hukurupuki tu na kupunguza wafanyakazi. Pili serikali ilipe baadhi ya madeni ya shirika hadi lifikie kiwango cha kukopesheka na tatu walipatie mtaji wa angalau ndege mbili mpya za size ya Boeing 737. Baada ya hapo atafute CEO kwa competitive recruitment na sio kwa style ya kuokotana, baada ya hapo nitasema ndaga fijo malafyale wewe ni jembe. Lakini kwa anayoyafanya saizi anajiaibisha tu na kuonekana vuvuzela kama Nape na ataondoka 2015 shirika liko vile vile. Maana hata akakae mwenyewe kuwa CEO kwa matatizo ya sasa ya ATCL atachemka tu.
 
Hapo umenena ila naamini jamaa analengo zuri na hizo hatua alizoanza nazo. Tumuunge mkono na kumshauri tusione matatizo tu na kuishia kulalamika!
 
Watanzania tunaongea sana................ lakini vitendo mmmmmhhhh............ Miaka ya 1970 Air Tanzania Corporation ilianzishwa sambamba na Kenya Airways.

Hivi ninapoandika, Kenya Airways anasafirisha abiria dunia nzima, ATCL ina ndege moja ya kukodi.

Huko nyuma, tulikuwa na kiwanda kimoja tu cha matairi ya magari almost East Africa yote. Kiwanda hicho kiliitwa General Tyre na kilikuwa pale Arusha. Lakini Kenya ikaona utendaji wa kiwanda hiki ni wa hovyo. Wao wakaanzisha kiwanda chao kama sikosei kiliitwa FIRESTONE. Kiwanda chetu cha Arusha kimekufa na sasa kiwanda cha Wa-Kenya ambacho kiliitwa Firestone kikabadili jina na kuitwa YANA. Hiki ni kiwanda kinachoongoza kwa kutoa matairi bora kwa sasa Afica Mashariki- Tanzania boooooooo........

Siku za nyuma tulikuwa na National Bank of Commerce. Bank ilikuwa nzuri na haikuwa na shida ya yoyote ya kutisha. Kenya nao walikuwa na Kenya Commerial Bank. Hivi niapoandika, National Bank of Commerce imeuzwa kwa Makaburu na sii mali ya Taifa tena kwa maana ya asilimia 100%, lakini Kenya Commercial Bank imekua na mpaka ninapoandika imefungua matawi kibao mpaka Mlimani City, Buguruni nk

Tusifanye kazi, tupige kelele sana na nafikiri tutafanikiwa kwa maneno. Ukiangalia utendaji kazi wetu umejaa a lot of uncertainities. Tunaongea uongo bila hofu, Ukabila kwa siri unachukua hatamu, udini nao usiombe

BADO KIDOGO wasomi kutoka nchi za Africa mashariki ndio watakaotawala ki-ajira na hata ki-biashara, lakini sisi Wa-Tanzania kwishilia mbali. Tumekosa maadili tangu msomi, mtu wa dini mpaka yule ambaye hajaenda shule.
 
Mtoa maada inabidi sasa utuambie ni mda gani unafaa karne,mlongo etc
Na pia ndani ya huo mda utuambie nini kifanyike and try to be SMART on your strategies and plans!
 
Kitendo cha waziri wa miundombinu Mh Mwakyembe kutoa miezi mitatu kwa shirika la ndege kuanza kujiendesha ni uendawazimu. Ni sawa na mwanaume ambaye hajaacha hela ya chakula nyumbani halafu anamwambia mkewe akirudi jioni akute wali kuku na Heinneken mbili za baridi...

Shirika lina ndege moja tu inayoruka, tena ya kukodi, shirika lina madeni kibao hadi Mwakyembe anawashauri kukwepa kwa kupitisha fedha za bima akaunti ya CHC, shirika lina wafanyakazi lukuki ambao halina fedha za kuwalipa mafao waende zao. Kwa msomi kama Mwakyembe angebuni namna ya kuliwezesha shirika kumiliki ndege, tena zinazoendana na soko la sasa sio zile dash 8 zao, ndio atoe muda angalau mwaka mmoja. Nina mashaka sana watu wa namna hii kuwa ndio washauri wa rais. Kwenye biashara akili nyingi, usimamizi halafu nguvu kidogo na siasa pembeni.

Ili shirika lijiendeshe linahitaji ndege ngapi? kwani shirika haliwezi kujiendesha likiwa na madeni? Haupo scientifical
 
watanzania tunafikiri shirika liweze kujiendesha linahitaji hela tu? nadhani ni zaidi ya fedha ndio maana ametoa hiyo miezi mitatu wajipange kuzaliwa upya
 
Watanzania tunaongea sana................ lakini vitendo mmmmmhhhh............ Miaka ya 1970 Air Tanzania Corporation ilianzishwa sambamba na Kenya Airways.

Hivi ninapoandika, Kenya Airways anasafirisha abiria dunia nzima, ATCL ina ndege moja ya kukodi.

Huko nyuma, tulikuwa na kiwanda kimoja tu cha matairi ya magari almost East Africa yote. Kiwanda hicho kiliitwa General Tyre na kilikuwa pale Arusha. Lakini Kenya ikaona utendaji wa kiwanda hiki ni wa hovyo. Wao wakaanzisha kiwanda chao kama sikosei kiliitwa FIRESTONE. Kiwanda chetu cha Arusha kimekufa na sasa kiwanda cha Wa-Kenya ambacho kiliitwa Firestone kikabadili jina na kuitwa YANA. Hiki ni kiwanda kinachoongoza kwa kutoa matairi bora kwa sasa Afica Mashariki- Tanzania boooooooo........

Siku za nyuma tulikuwa na National Bank of Commerce. Bank ilikuwa nzuri na haikuwa na shida ya yoyote ya kutisha. Kenya nao walikuwa na Kenya Commerial Bank. Hivi niapoandika, National Bank of Commerce imeuzwa kwa Makaburu na sii mali ya Taifa tena kwa maana ya asilimia 100%, lakini Kenya Commercial Bank imekua na mpaka ninapoandika imefungua matawi kibao mpaka Mlimani City, Buguruni nk

Tusifanye kazi, tupige kelele sana na nafikiri tutafanikiwa kwa maneno. Ukiangalia utendaji kazi wetu umejaa a lot of uncertainities. Tunaongea uongo bila hofu, Ukabila kwa siri unachukua hatamu, udini nao usiombe

BADO KIDOGO wasomi kutoka nchi za Africa mashariki ndio watakaotawala ki-ajira na hata ki-biashara, lakini sisi Wa-Tanzania kwishilia mbali. Tumekosa maadili tangu msomi, mtu wa dini mpaka yule ambaye hajaenda shule.
 
jana nilisema na leo narudia waziri mwakyembe kuwekwa wizara hii ni '' gateway'' yake......watu wako strategic bana....hawezi kuifikisha salama hii wizara hata kidogo.....ngoja plan ikamilike
 
Watanzania tunaongea sana................ lakini vitendo mmmmmhhhh............ Miaka ya 1970 Air Tanzania Corporation ilianzishwa sambamba na Kenya Airways.

Hivi ninapoandika, Kenya Airways anasafirisha abiria dunia nzima, ATCL ina ndege moja ya kukodi.

Huko nyuma, tulikuwa na kiwanda kimoja tu cha matairi ya magari almost East Africa yote. Kiwanda hicho kiliitwa General Tyre na kilikuwa pale Arusha. Lakini Kenya ikaona utendaji wa kiwanda hiki ni wa hovyo. Wao wakaanzisha kiwanda chao kama sikosei kiliitwa FIRESTONE. Kiwanda chetu cha Arusha kimekufa na sasa kiwanda cha Wa-Kenya ambacho kiliitwa Firestone kikabadili jina na kuitwa YANA. Hiki ni kiwanda kinachoongoza kwa kutoa matairi bora kwa sasa Afica Mashariki- Tanzania boooooooo........

Siku za nyuma tulikuwa na National Bank of Commerce. Bank ilikuwa nzuri na haikuwa na shida ya yoyote ya kutisha. Kenya nao walikuwa na Kenya Commerial Bank. Hivi niapoandika, National Bank of Commerce imeuzwa kwa Makaburu na sii mali ya Taifa tena kwa maana ya asilimia 100%, lakini Kenya Commercial Bank imekua na mpaka ninapoandika imefungua matawi kibao mpaka Mlimani City, Buguruni nk

Tusifanye kazi, tupige kelele sana na nafikiri tutafanikiwa kwa maneno. Ukiangalia utendaji kazi wetu umejaa a lot of uncertainities. Tunaongea uongo bila hofu, Ukabila kwa siri unachukua hatamu, udini nao usiombe

BADO KIDOGO wasomi kutoka nchi za Africa mashariki ndio watakaotawala ki-ajira na hata ki-biashara, lakini sisi Wa-Tanzania kwishilia mbali. Tumekosa maadili tangu msomi, mtu wa dini mpaka yule ambaye hajaenda shule.

....mkuu nashukuru kwa taarifa hizi!unajua bongo tumezidi kuongea sn!hivi kenya wanatuzidi nn jamani?...khaaaaa!
 
Kitendo cha waziri wa miundombinu Mh Mwakyembe kutoa miezi mitatu kwa shirika la ndege kuanza kujiendesha ni uendawazimu. Ni sawa na mwanaume ambaye hajaacha hela ya chakula nyumbani halafu anamwambia mkewe akirudi jioni akute wali kuku na Heinneken mbili za baridi...

Shirika lina ndege moja tu inayoruka, tena ya kukodi, shirika lina madeni kibao hadi Mwakyembe anawashauri kukwepa kwa kupitisha fedha za bima akaunti ya CHC, shirika lina wafanyakazi lukuki ambao halina fedha za kuwalipa mafao waende zao. Kwa msomi kama Mwakyembe angebuni namna ya kuliwezesha shirika kumiliki ndege, tena zinazoendana na soko la sasa sio zile dash 8 zao, ndio atoe muda angalau mwaka mmoja. Nina mashaka sana watu wa namna hii kuwa ndio washauri wa rais. Kwenye biashara akili nyingi, usimamizi halafu nguvu kidogo na siasa pembeni.

Ulukulo;
Kama neema ingekushukia leo, ukaitwa na Mkuu wa Nchi na ukaulizwa nani asimamie wizara hii, ungemtaja nani baada ya kumwona Mwakyembe mwendawazimu? Onyesha mikakati yako 10 ya makusudi ambayo ungeweza ku2mia zaidi ya ile aliyoanza nayo huyu, baada ya Nundu kuvurunda. Unafikiri ni rahisi kusimamisha jengo siku moja hata kama una pesa ya kupata kila kifaa kwa dakika?
 
Mikakati ya 4.9 bilioni kuokoa shirika la ndege linalohitaji bilioni 300. What is juhudi by the way? Viongozi wa aina ya Mwakyembe wenye kulalamika bila kutoa suluhisho mnatakiwa kuanza kuwakataa kama mnataka nchi iendelee.

Ukisikia mtu bichwa kuuubwa lakini ndani yake ubongo wa mbu hawezi kuwa sio wewe! sasa wewe ulitaka kyembe afanye nini? au wewe ndo walewale ambao mkipewa ruzuku na serikali kipaumbele ni kushona uniform za shilingi milioni nne na laki kadhaa kwa kila mmoja! hiyo ndo akili ya ubongo mmbu kama wewe!
 
Joseph Stallin aliwapa Wahandisi wa Russia miezi mitatu kuwa wameujenga mji wa Volgograd.

Kumbuka huu mji ulibomolewa wote na kubaki jengo moja tu limesimama ilipokuwa mashine ya kusaga ngano.

Amini usiamini, leo hii angelikuja MBABE na kusema Tanzania iwe TAJIRI na Nchi SAFI huku mashirika yote ya Serikali yakileta Faida na Daraja la Kigamboni, Reli, ATCL, General Tires etc yakifanya kazi kwa fadi, LINGELIWEZEKANA.

Warusi kweli kwa miezi mitatu, waliujenga mji wa VOLGOGRAD.

dsc04962ss.jpg
 
Ukisikia mtu bichwa kuuubwa lakini ndani yake ubongo wa mbu hawezi kuwa sio wewe! sasa wewe ulitaka kyembe afanye nini? au wewe ndo walewale ambao mkipewa ruzuku na serikali kipaumbele ni kushona uniform za shilingi milioni nne na laki kadhaa kwa kila mmoja! hiyo ndo akili ya ubongo mmbu kama wewe!
Linapokuja suala rushwa ndani ya serikali ya CCM hakuna wa kunyoshea kidole mwenzie. Huyu huyu Mwakyembe aliwahi kuitwa takukuru akahojiwe kwa ufisadi wa kupokea posho mara mbili kwa kikao kimoja akakataa, wakataka kumkamata kwa nguvu akaokolewa na swaiba yake spika Sitta. Kupambana na rushwa inahitaji dhamira, Mwakyembe na wana CCM wenzie hawana, kila mtu anawaza apige dili gani. Hata huko huenda kamuweka binamu yake Lusajo wapige dili baada ya Chizi kuwazuia kupiga dili la uagizaji wa hii ndege ya sasa kwa kukataa kuongeza cha juu.
 
kweli watanzania tunashida kubwa kimkichwa. Jamaa anajitahidi kufanya mabadiliko sisi tumebaki kupika majungu na vikwazo vya kila namna. Umesoma mikakati yake ya kufikia hilo lengo la kujiendesha na kuiona hovyo hadi utoe hukumu na kumuita mwendawazimu?

I like that Dandabo
 
Kitendo cha waziri wa miundombinu Mh Mwakyembe kutoa miezi mitatu kwa shirika la ndege kuanza kujiendesha ni uendawazimu. Ni sawa na mwanaume ambaye hajaacha hela ya chakula nyumbani halafu anamwambia mkewe akirudi jioni akute wali kuku na Heinneken mbili za baridi...

Shirika lina ndege moja tu inayoruka, tena ya kukodi, shirika lina madeni kibao hadi Mwakyembe anawashauri kukwepa kwa kupitisha fedha za bima akaunti ya CHC, shirika lina wafanyakazi lukuki ambao halina fedha za kuwalipa mafao waende zao. Kwa msomi kama Mwakyembe angebuni namna ya kuliwezesha shirika kumiliki ndege, tena zinazoendana na soko la sasa sio zile dash 8 zao, ndio atoe muda angalau mwaka mmoja. Nina mashaka sana watu wa namna hii kuwa ndio washauri wa rais. Kwenye biashara akili nyingi, usimamizi halafu nguvu kidogo na siasa pembeni.

Wakati Nyerere anaanza kudai uhuru kuna watu walisema kama wewe , Walimuona Nyerere kama mtoto ambaye asingeweza kuwatoa wakoloni kwa sababu kuna watu mashuhuri zaidi kama akina Mkwawa, kinjekitile, Songea Mbano n.k walijaribu wakashidwa hivyo huyu mtoto mdogo kama yeye asingeweza. Nyerere hakukata tamaa na aliendelea na mwisho akaweza. Kila kitu kinawezekana kwa kuthubutu, Mwakyembe amethubutu kutamka kitu amabacho wengi wameshidwa. Mwacheni kwanza muone mikakati yake ndo muoji kama ataweza au atashindwa. Kukata tamaa na kuona kuwa atuwezi ndo ugonjwa mkubwa tulionao watanzania including mtoa mada hapo juu. Tuache kucritsize wakati hatujui mikakati aliyonayo waziri. Let us think positive always.
 
Kitendo cha waziri wa miundombinu Mh Mwakyembe kutoa miezi mitatu kwa shirika la ndege kuanza kujiendesha ni uendawazimu. Ni sawa na mwanaume ambaye hajaacha hela ya chakula nyumbani halafu anamwambia mkewe akirudi jioni akute wali kuku na Heinneken mbili za baridi...Shirika lina ndege moja tu inayoruka, tena ya kukodi, shirika lina madeni kibao hadi Mwakyembe anawashauri kukwepa kwa kupitisha fedha za bima akaunti ya CHC, shirika lina wafanyakazi lukuki ambao halina fedha za kuwalipa mafao waende zao. Kwa msomi kama Mwakyembe angebuni namna ya kuliwezesha shirika kumiliki ndege, tena zinazoendana na soko la sasa sio zile dash 8 zao, ndio atoe muda angalau mwaka mmoja. Nina mashaka sana watu wa namna hii kuwa ndio washauri wa rais. Kwenye biashara akili nyingi, usimamizi halafu nguvu kidogo na siasa pembeni.
Sidhani kama ni kweli kuwa Mwakiembe ametoa miezi mitatu, huenda amenukuliwa vibaya , ila kama ametoa hiyo miezi mitatu basi hicho ni kichekesho kwa mwaka 2012
 
Hii ndio aina ya viongozi tulio nao,anatoa matamko kisiasa zaidi lakini linapokuja swala la utekelezaji ni ziro kabisa matokeo yake atashusha lawama kibao baadaye na kuanza kutafuta mchawi.ATCL inatakiwa ipewe Boeing au Airbus brand new mbili (2) na Bambadier mbili (2) kwa route fupi, wachanganye na ile iliyoko garage ziwe tano (5) ,kisha wachanganye na za kukodi hapo,wapate management iliyosimama na working capital ya kutosha sasa ndio wapewe muda wa kusimama wenyewe sio hizi bla bla za bongo politician.

MWAKYEMBE BADO TATIZO NI KUBWA WIZARA YAKO KUWA MAKINI NA KATIBU MKUU WAKO.

Kwanza naendelea kusisitiza kuwa MR CHIZI hauhisiki na kuiingizia hasara billion 69 serikali ambazo ni pesa za kitanzania, kwa kuingia mkataba na ndege ya AB320 ijulikanayo kama AIRBUS ambayo ndege hii aliingia mkataba Mr MATAKA mwaka 2008. sasa Mr chizi hapo anahusika vipi??? Wakati Mr chizi ameteuliwa mwaka 2011 mwezi 8.

Na je nani alimuajiri MR CHIZI ? mbona hawajibishwi?? Katibu mkuu anahusika kumuajiri MR CHIZI, Mr MATAKA yeye aliteuliwa na RAIS je rais hakufuata masharti ya kumteua mr mataka ambaye baadae ameiingizia hasara serikali sh billion 69 Tzsh mwaka 2008 kwa kuingia mkataba na AB320 ambayo sasa imekuwa kesi ya CHIZI?? Usisahau kuwa mataka aliwahi kufukuzwa kazi PPF ndio akaajiriwa ATCL je ni vigezo vipi vilitumika kwa MATAKA kumrudisha kazini kama unasema MR CHIZI alisha staafu??

Kama suala ni kuwa serikali haikushirikishwa kwenye ukodishaji wa B737-500 ambayo MR CHIZI ndio ameisimamia mpaka kuja kwake hapa ni kwanini WAZIRI alikuwa anajibu maswali kuhusu ATCL bungeni na kutueleza sisi wananchi juu ya mipango ya ATCL ya kuleta ndege itakayotoa huduma??

Kama haitoshi serikali ktk BUNGE la bajeti la mwaka 2011/2012 iliidhinisha billion 21 ili ATCL ijiendeshe yenyewe kwa kuwa imekuwa mzigo kwa serikali, na serikali iliongeza kuwa haitoingilia shirika hilo.Je ATCL kuleta ndege imekuwa kosa wakati serikali ilisha sema hamtoingilia kwa kuwa mliishaidhinisha billion 21 ili ijitegeme??

Kama walisha kuwa mzigo kwenu kwanini msinge waletea ndege ili wao wajiendeshe wenyewe? Mpaka mmesubiri wameleta ndege then mnawatuhumu??? MWAKYEMBE kuna mengi kuwa makini.

Kama haitoshi serikali iliidhinisha pesa hizo bil.21 kwenye bunge la bajrt 2011/2012 pesa hizo hazikutolewa kwa muda muafaka na zimetoka juzi nazo ni bil,4.9 pekee, je watajiendeshaje??

Kama kosa ni kutotangaza tenda ya UNIFORM za atcl ktk mfumo wa serikali mbona serikali ilisha jitoa kuingilia shirika hilo??? Sijaona tatizo la MR. CHIZI hapo. Kaa chini na ATCL vizuri utagundua mengi ya katibu wako.

Asante.
 
Back
Top Bottom