Miezi mi3 kwa ATCL kujiendesha ni uendawazimu wa Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miezi mi3 kwa ATCL kujiendesha ni uendawazimu wa Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ulukolokwitanga, Jun 8, 2012.

 1. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kitendo cha waziri wa miundombinu Mh Mwakyembe kutoa miezi mitatu kwa shirika la ndege kuanza kujiendesha ni uendawazimu. Ni sawa na mwanaume ambaye hajaacha hela ya chakula nyumbani halafu anamwambia mkewe akirudi jioni akute wali kuku na Heinneken mbili za baridi...

  Shirika lina ndege moja tu inayoruka, tena ya kukodi, shirika lina madeni kibao hadi Mwakyembe anawashauri kukwepa kwa kupitisha fedha za bima akaunti ya CHC, shirika lina wafanyakazi lukuki ambao halina fedha za kuwalipa mafao waende zao. Kwa msomi kama Mwakyembe angebuni namna ya kuliwezesha shirika kumiliki ndege, tena zinazoendana na soko la sasa sio zile dash 8 zao, ndio atoe muda angalau mwaka mmoja. Nina mashaka sana watu wa namna hii kuwa ndio washauri wa rais. Kwenye biashara akili nyingi, usimamizi halafu nguvu kidogo na siasa pembeni.
   
 2. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,646
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hii ndio aina ya viongozi tulio nao,anatoa matamko kisiasa zaidi lakini linapokuja swala la utekelezaji ni ziro kabisa matokeo yake atashusha lawama kibao baadaye na kuanza kutafuta mchawi.ATCL inatakiwa ipewe Boeing au Airbus brand new mbili (2) na Bambadier mbili (2) kwa route fupi, wachanganye na ile iliyoko garage ziwe tano (5) ,kisha wachanganye na za kukodi hapo,wapate management iliyosimama na working capital ya kutosha sasa ndio wapewe muda wa kusimama wenyewe sio hizi bla bla za bongo politician.

   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Tatizo watanzania wengi wakisikia waziri ametoa miezi mitatu shirika lianze kujiendesha wanasema huyu ndio waziri tunayemtaka, ila hajatoa mbinu lijiendeshe vipi?
  Amenza na mteremko ATC, tungoje akienda kwenye reli atasemaje maana kule biashara ya usafirishaji ni shindani na biashara ya malori ya wakubwa zake... Sijui atawapa miezi mingapi treni zishamiri
   
 4. d

  dandabo JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  kweli watanzania tunashida kubwa kimkichwa. Jamaa anajitahidi kufanya mabadiliko sisi tumebaki kupika majungu na vikwazo vya kila namna. Umesoma mikakati yake ya kufikia hilo lengo la kujiendesha na kuiona hovyo hadi utoe hukumu na kumuita mwendawazimu?
   
 5. C

  Chesty JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,335
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Kwenye Reli anaogopa hata kusogelea, maana wenye malori wanaoifinance CCM pamoja na viongozi wataenda kwa Kikwete au Pinda na hamtamsikia tena. Hiyo ndio CCM bana.

  Dawa yao hawa ipo 2015. Ondoa lichama mfu hili linaturudisha nyuma sie.
   
 6. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hilo ndilo tatizo la kuchanganya SIASA na BIASHARA....... Kwa mtindo huuu hakuna lolote hapo.... ni blaablaa blaa..
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kwa nini unalalamika kuhusu miezi mitatu wakati hata wiki haijapita! Wajipange na kama haiwezekani kwa miezi hiyo, wanaweza kuomba huruma ya kuongezewa muda. Watanzania tumechoka kuweka fedha zetu kwenye kasiki linalavuja!
   
 8. C

  Chesty JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,335
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Mwakyembe hawezi kuleta mabadiliko yoyote ndani ya mfumo wa kifisadi wa CCM, mbona unashindwa kuelewa kitu kidogo hicho? Alikuwa miundombinu nini alichokifanya.

  Mwakyembe anatrack record ya kuwa kigeugeu sana, fuatilia sakata la kuugua kwake na dhamira yake ya kusema ukweli wote baadae akabadilika ghafla baada ya kuahidiwa ulaji ili kumpoza.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona umeandika tu kwa jazba ili mradi tu..

  1. Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilion 4.9 kwa ajili ya maintanance na operations lakini hakuna tangible gains zozote zile.

  2. Shirika lina ndege moja na wafanyakazi 200 wanaolipwa mishahara, kwangu mimi it does not make sense

  3. Serikali inadaiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 69 kutokana na mikataba ya kijinga ya ATCL

  4. Je, huyu Chizi wakati anaenda kukodi hii ndege aliishirikisha Wizara? Alimshirikisha AG(Attorney General)? Je alifuata sheria za tenda wakati anaenda kukodisha hiyo ndege (Boeing 737-500 kutoka kwa Aero Vista)?
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Usidhani watu wote wanafanana, Huyu wa uzi huu akili yake imefikia hapo. Wapo watu wanaoweza kufanya mambo yakaitwa miujiza. Sokoine alikua akisema kitu kinakuwa. Naona sasa bongo zimelala. Mwacheni Mwakyembe ajaribu kufanya mazuri kwa kadri ya uwezo wake. Tusijilinganishe nae.
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona sokoine aliweza. Ila mwisho duhh. Magufuli anaogopa mpaka kiti, lakini anaweza. watua wanatofautiana, hawafanani na wewe.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,450
  Likes Received: 5,838
  Trophy Points: 280
  Hiyo miezi mitatu nilivyo muelewa mimi ni kwa ajili ya 'restructuring' ambayo ina maana pana sana. Kwa anae elewa atakubaliana na Mwakyembe.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sisi wa uku sector binafsi tumezoea deadlines ila serikalini wanataka wapewe karne kusolve issues!
  Kiustaarabu kama umepewa deadline na mda umefika haujatekeleza uliyoambiwa lazima uanishe kilichokukwamisha then mnakaa meza moja na mtoa deadline tuone the way forward!
  Sasa hawa wanaosema 3 months hazitoshi umejuaje wakati mda wenyewe haujapita?
  Na hiki ndicho kinachotukwamisha watz ktk kazi!
   
 14. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hapa ugumu ni nini? sikuna wakati hapa jamvini uliwahi kuwekwa uzi wa kumsifia Rais Paul Kagame wa Rwanda, mnajua siri yake yule jamaa, huwa anawapa mawaziri wake kitu kinachoitwa KPI pamoja na muda, robo ya mwaka ikiisha tu wanatakiwa kuleta mafanikio na kushindwa kwao, hapa mimi naomba nitofautiane kabisa na wengine, MWakyembe yupo sahihi kabisa, issue ya kuwa na wafanyakazi 200 while una ndege 1 tena ya kukodi wa kulaumiwa sio waziri, hiyo ni issue ya CEO wa shirika husika. Kama shirika halina pesa kweli, mbona hizo uniform za batiki wameweza kununua kwa USD 49000/=

  Guys, let us open our eyes, uwezi wanao sana tu, mi naona miezi 3 inatosha kabisa kwa wao kujipanga, Mwakyembe is right!
   
 15. d

  dandabo JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Duh! Kwahiyo unamshauri aendeleze uozo alioukuta kwa kisingizio cha system mbovu!
   
 16. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mikakati ya 4.9 bilioni kuokoa shirika la ndege linalohitaji bilioni 300. What is juhudi by the way? Viongozi wa aina ya Mwakyembe wenye kulalamika bila kutoa suluhisho mnatakiwa kuanza kuwakataa kama mnataka nchi iendelee.
   
 17. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka hata JK kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa alianza na mikwara ya ziara za kushtukia kwenye wodi muhimbili na kwingineko! Lakini zilimshinda badala yake akahamia wizara ya mambo ya nje kwakusafiri na kuzunguka dunia.
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Njowepo mimi nafikiri hawa dawa ni kuwapa deadline wakishindwa ku-deliver within the time frame or limit you get them fired nashangaa huyu jamaa analalamika hiyo miezi 3 that's the kind of people we have, 35 years and the airline hasn't done shit..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Braza kuna kitu kinaitwa SMART unapotoa deadline ya kufanya kitu. Haukurupuki tu. Wanasiasa wetu tuwafundishe kuanza kutoa matamko yenye akili na sio kuatract public opinions
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  Sometimes we Tanzanians have to learn the hard way...tusipende ubweteubwete kama JK alivyodhani kuongoza taifa ni kama vile anavyoongoza familia zake.
  Bunge la bajeti muda si mrefu litafanyika na itakuwa ndani ya hiyo miezi mitatu. Mgawanyo wa fedha umeshafanyika na Miundombinu ni kati ya wizara zenye kipaumbele.
   
Loading...