Miezi mi3 kwa ATCL kujiendesha ni uendawazimu wa Mwakyembe

Kwanza angetafuta hela za kupunguza wafanyakazi na kuwalipa mafao, maana hukurupuki tu na kupunguza wafanyakazi. Pili serikali ilipe baadhi ya madeni ya shirika hadi lifikie kiwango cha kukopesheka na tatu walipatie mtaji wa angalau ndege mbili mpya za size ya Boeing 737. Baada ya hapo atafute CEO kwa competitive recruitment na sio kwa style ya kuokotana, baada ya hapo nitasema ndaga fijo malafyale wewe ni jembe. Lakini kwa anayoyafanya saizi anajiaibisha tu na kuonekana vuvuzela kama Nape na ataondoka 2015 shirika liko vile vile. Maana hata akakae mwenyewe kuwa CEO kwa matatizo ya sasa ya ATCL atachemka tu.

Hapo red; ona sasa shirika linatengeneza medeni ya hovyo bila serikali kujua halafu wakishindwa kulipa wanaleta hazina serikalini ilipe, hii haikubaliki lazima serikali iwe inajua na kuridhia huo ukopaji wa madeni.
 
Hiyo miezi mitatu nilivyo muelewa mimi ni kwa ajili ya 'restructuring' ambayo ina maana pana sana. Kwa anae elewa atakubaliana na Mwakyembe.

Heri wewe mzee wa safari, umezpiga mpaka akili imebaki... Hatutaki anayejaribu, hatutaki anayekoromea, hatutaki anayetupa matumaini, hatutaki anayetupa siasa, hatutaki asiyetupa
 
Hiyo miezi mitatu nilivyo muelewa mimi ni kwa ajili ya 'restructuring' ambayo ina maana pana sana. Kwa anae elewa atakubaliana na Mwakyembe.

Heri wewe mzee wa safari, umezpiga mpaka akili imebaki... Hatutaki anayejaribu, hatutaki anayekoromea, hatutaki anayetupa matumaini, hatutaki anayetupa siasa, hatutaki asiyetupa Matumaini, hatutaki anayetupa data...hatutaki hatutaki, hatutaki kuelewa chochote, hatutaki!
 
Watanzania tunaongea sana................ lakini vitendo mmmmmhhhh............ Miaka ya 1970 Air Tanzania Corporation ilianzishwa sambamba na Kenya Airways.

Hivi ninapoandika, Kenya Airways anasafirisha abiria dunia nzima, ATCL ina ndege moja ya kukodi.

Huko nyuma, tulikuwa na kiwanda kimoja tu cha matairi ya magari almost East Africa yote. Kiwanda hicho kiliitwa General Tyre na kilikuwa pale Arusha. Lakini Kenya ikaona utendaji wa kiwanda hiki ni wa hovyo. Wao wakaanzisha kiwanda chao kama sikosei kiliitwa FIRESTONE. Kiwanda chetu cha Arusha kimekufa na sasa kiwanda cha Wa-Kenya ambacho kiliitwa Firestone kikabadili jina na kuitwa YANA. Hiki ni kiwanda kinachoongoza kwa kutoa matairi bora kwa sasa Afica Mashariki- Tanzania boooooooo........

Siku za nyuma tulikuwa na National Bank of Commerce. Bank ilikuwa nzuri na haikuwa na shida ya yoyote ya kutisha. Kenya nao walikuwa na Kenya Commerial Bank. Hivi niapoandika, National Bank of Commerce imeuzwa kwa Makaburu na sii mali ya Taifa tena kwa maana ya asilimia 100%, lakini Kenya Commercial Bank imekua na mpaka ninapoandika imefungua matawi kibao mpaka Mlimani City, Buguruni nk

Tusifanye kazi, tupige kelele sana na nafikiri tutafanikiwa kwa maneno. Ukiangalia utendaji kazi wetu umejaa a lot of uncertainities. Tunaongea uongo bila hofu, Ukabila kwa siri unachukua hatamu, udini nao usiombe

BADO KIDOGO wasomi kutoka nchi za Africa mashariki ndio watakaotawala ki-ajira na hata ki-biashara, lakini sisi Wa-Tanzania kwishilia mbali. Tumekosa maadili tangu msomi, mtu wa dini mpaka yule ambaye hajaenda shule.

Nimekubali ulichosema ni ukweli mtupu na hilo tatizo sidhani kama kuna haja ya mtu au chama kitatuondolea kwani ni vigumu sana. Tunachotakiwa tubadilike kila mmoja kwa dhamiri yake ya ndani, vinginevyo hakuna shule ya kutubadilisha.
 
Back
Top Bottom