tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,039
Kampuni ya Microsoft imezindua kipengele kipya katika programu yake ya Teams kinacholenga kurahisisha ufuatiliaji wa mahali wafanyakazi walipo, hatua ambayo imezua mjadala kuhusu faragha kazini.
Kupitia kipengele hicho, waajiri wataweza kubaini kama mfanyakazi anafanya kazi ofisini au nje ya ofisi kwa kupitia mtandao wa Wi-Fi atakaokuwa anautumia mfanyakazi huyo. Vilevile, wasimamizi wa timu wataweza kuweka anwani rasmi za ofisi ili kurahisisha ufuatiliaji wa mahudhurio na kupanga ratiba za kazi kwa urahisi.
Soma pia: Microsoft imetangaza kufunga rasmi mtandao wa Skype
Kwa mujibu wa Microsoft, lengo ni kusaidia wafanyakazi na waajiri kuelewa ratiba na maeneo ya kazi ya kila mmoja ili kuepuka mkanganyiko katika mfumo wa kazi mchanganyiko
Hata hivyo, baadhi ya wadau wameeleza wasiwasi wao, wakihofia kuwa teknolojia hiyo inaweza kutumika kama njia ya kufuatilia wafanyakazi badala ya kurahisisha mawasiliano kazini.
Microsoft imesema kipengele hicho kitazinduliwa rasmi duniani kote kufikia Disemba 2025, na kitapatikana kwa watumiaji wa Teams wanaotumia Windows na macOS
Ifahamike, 'Microsoft Teams' ni programu ya mawasiliano na ushirikiano wa kikazi, inayomruhusu mfanyakazi kuzungumza, kufanya mikutano ya video, kushirikiana mafaili, na sasa pia kufuatilia mahali wafanyakazi walipo kwa ajili ya usimamizi wa rasilimali watu