Michuzi Blog, hii ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Michuzi Blog, hii ni sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jibabaz, May 20, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. j

  jibabaz Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natanguliza shukrani kwa bro Michuzi DC wa naniii pale kwa huduma yake nzuri anayoitoa kwa jamii kuwasilisha "niuzi" kwetu sote.

  Swali langu linakuja hapa, Ni kwamba kuna tangazo pale juu kabisa mara baada ya kuingia kwenye website ya michuzi after tangazo la Ndovu. Hili ni Tangazo la Chuo kimoja hapo London(London School of Commerce), UK kinasema kinadoa MBA kwa bei poa. Sasa swali langu ni hio lugha iliotumiwa na hio shule kwenye spelling ya "course" ambayo wao wameweka "cource" (i presume wanataka kuwa na maana ya course") Nimeangalia definition yake nimekosa.
  Gonga cource definition | Dictionary.com

  Sasa kama chuo kinasema ni shule inayotoa degree inayotambulika duniani jee hii ni sawa?
  Isije ikawa ndio shule zetu za mitaani za kina Dr Nchimbi. Naomba kuwasilisha..

  Source ya hilo tangazo:
  MICHUZI
   
 2. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
 3. j

  jibabaz Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani kumbe Dr Shayo ndo ana Phd ya hapa?? Kaazi kweli kweli..mmhhhh
   
 4. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Huo ni mfano wa kutosha kuwa chuo hicho hakifai kusoma,huwezi kuwa na chuo kina intake sita kwa mwaka na digrii unapata within two years.ukitizama website ya chuo unajua kuna something ..... kwenye hicho chuo.fanyeni utafiti kabla ya kulipa au kujisali na vi college kama hivi.hata ukitaka kwenda vyuo vikuu pata ushauri wa vyanzo mbalimbali kama www,timesonline.co.uk au tizama universities ranking etc.
  chuo kama kiko serius kisingepita kwa michuzi blog kinakwepa kodi ya kujitangaza. unajua gazeti kama la ulaya gharama za matangazo ni kubwa hivyo wanavamia kwa michuzi.

  Michuzi anatakiwa awe makini kwenye matangazo kwani anaowapoteza ni watanzania wenzake.

  huko mbele tutakuwa na wasomi wenye MBA ambazo hazina misingi mizuri kama hizi za vyuo hivi.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Jamani hicho chuo sikijui wala ubora wake sifahamu. Ninacho taka kusema tu ni kuwa degree za miaka miwili zipo msiseme hazipo. Kama ubora ndiyo tatizo sawa ila hiyo ya degree za miaka miwili siyo tatizo.

  Kuna degree za aina mbili:
  1.Bachelors's degree = 4 years

  2.Associate's degree = 2 years

  Associate's degree ina hadhi ya chini ukilinganisha na Bachelor's na wengi wanaopenda kujiendeleza kama akichukua Associate's degree akimaliza anaweza kwenda kuchukua a Bachelor's degree.

  Wengi wanao chukua Associate's degree ni wale ambao grades zao au shule walizo kua wakisoma wazi ridhishi kusomea Bachelor's. Au unakuta mtu kamaliza form four so badala ya lwenda A level anachukua Associates degree miaka miwili then ana chukua zake Bachelor's degree.

  Ni hicho tu nilicho taka kusema kuhusu degree za miaka miwili.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Moja ya vyuo hivyo mifano yake hai ipo hapa hapa Dar,kuna baadhi ya vyuo vya Hoteli na uhazini vipo Parking ya Avalon na mitaa ya Mansfield,Nkrumah na vitongoji vya K'koo,Sinza,K'nyama... Sijui ila ni bomu la muda litalipuka siku moja...
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,384
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu, Suala ubora wa chuo na credibility yake ni jambo moja, na michuzi kupokea tangazo ni jambo jingine. Kwenye tangazo, sio jukumu la mpokeaji kufanya vetting ya chuo, hilo ni jukumu la mtumiaji huduma hiyo. Ni kawaida kukuta matangazo ya hivi vyuo feki na non accredited kwenye magazeti na vyombo vya habari vya home na sio jukumu la chombo husika kuulizwa.
  Hivyo ni sawa kwa michuzi kupokea tangazo lolote.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hivi vyuo sidhani viko zaidi ya kufanya biashara.Wenye kusoma huko wanasafari ndefu ya kuelimika/kupata taaluma stahiki.BUYER BEWARE!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni makosa kusema Michuzi hahusiki kwa tangazo..Kupokea tu matangazo bila kujua undani wake na kuyabandika bila kujiridhisha ni dalili ya u-robot.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,384
  Trophy Points: 280
  WoS amesema vizuri 'buyer be ware' kosa la Michuzi lipi?. Hivi kweli ni jukumu la mtangazaji kufanya vetting?. Kuna sheria ya liability kwenye matangazo mipaka ya sheria hii inaishia kwenye vyakula na madawa, mtu akithirika ndipo mpaka aliyetangaza atawajibika ndio maana huwezi kuona matangazo ya madawa ama mahospitali.Kwa tangazo la chuo, hakuna liability yoyote kwa media inayotangaza hata kama hicho chuo ni non existance, fake ama un accredited.Kwenye hili la matangazo, nasimama na Michuzi sio kwamba he is doing the right thing, bali he is making his good clean money huku akiisaidia jamii kuihabarisha, kulikoni wengine wetu mimi nikiwemo, tunajisikitikia na umasikini wetu tukishindwa kufanya yatupasayo kufanya, tuishia kuwalaumu wengine wafanyao vitu vyao.Naomba kudeclare conflict of interest. Mimi ni fan mkubwa wa globu ya jamii.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Yaani unarejea tena kuuliza kosa la Michuzi ni lipi? No wonder nchi yetu kila kitu kinaenda shaghalabaghala kwa sababu ya watu kama wewe mnaoukubali u-robot. Robot hatumii akili kuchuja kitu kinachokuja mbele yake, yeye anapokea tu instructions na kuzitekeleza ..thats why..

  Sitaki kujikita kwenye maelezo mareeefu kuhusu sheria, na nafanya hivyo makusudi kabisa kwa sababu sheria zenyewe nazo si absolute and most of them are debatable.Tukianza kila kosa lazima liwekwe kwenye sheria ndio lihesabike kuwa kosa itakuwa kufanya ufarisayo, na kuzunguka kwenye circle badala ya kutoka kwenye circle. Nnachosema kama kweli mtu anaamua kuhost blogu inayoinadi ni ya jamii ni vyema aliridhishe na akifanyacho kweli kuwa ni kitu cha kuinufaisha jamii. Kusema tu ana-make 'decent' money is very low, kwa sababu kuna some folks wataingia mkenge kwa matangazo ya hiohio blogu ya 'jamii'
   
 12. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Ntamwambia Invisible asikubali kuitwa Robot,,,,, hii imekaa vibaya
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh..sasa itabidi tuanzishe twisheni ya kutumia akili hapa jamvini..lol
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,384
  Trophy Points: 280
  Sio kila kitu unahitaji kutumia akili, mambo mengine kweli ni kirobt robot na hata watu wenye mtindio, nao pia wana uwezo wa kuchuja mema na mabaya kwa jamii kutegemeana na mtindio wao umeathiri idara gani.
  Kwa chuo kutokuwa accredited mbona sio kosa, ndio maana kimesajiliwa. Mbona hayo matangazo kila siku yako magazetini mpaka TBC ambayo ni ya taifa na sijasikia yakilalamikiwa?.
  Hivi kumbe akifanya fulani ndipo inageuka issue!.
  Hebu mwacheni Michuzi atengeneze huku akihabarisha na kuelimisha.
  Bado nasimama na 'globu ya jamii' sisemi kuwa is the right thing to do, but its not wrong anyway.
   
 15. A

  AbbyBonge Member

  #15
  May 21, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani Michuzi hapaswi kulaumiwa ila Chuo ndio kinaonyesha udhaifu, maana kampuni au tasisi inapotoa tangazo, inapaswa kufuatilia kwa karibu ili kuona kama tangazo linatolewa katika ubora na wakati uliokusudiwa, ili malipo yao yaende kihalali.
  Sasa kama wameshindwa kuona hiyo typing error hapo natilia mashaka hata documents zao kama hata zinasomeka.
  Lakini pia inawezekana inachangiwa na ile tabia ya kuamini kuwa kazi hii ni ya fulani. Watumishi wa chuo wanapaswa kushirikiana katika kulinda hadhi ya ofisi yao, maana sitaki kuamini kama hakuna mtu au mtumishi wa chuo husika hajawahi kuona kosa hili maana hili tangazo nadhani halitokei kwa Michuzi tu bali sehemu nyingine.
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Vyuo vingi vimeanzishwa siku hizi lakini yet wanataaluma hafifu.
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Mkuu, chuo kilicho serious kisingepita kwa Michuzi?!I don' think whether you're right!!! Hapo lazima ujue kwamba walilenga kumtangazia nani!!! Kama target yao at that time ilikuwa East African students, TZ in particular, unazani ingekuwa rational kwao kutangaza kupitia media za Ulaya?! Umetoa good advice kwamba applicants, before doing so, watafute more information about the advertised college, and this's never Michuzi's business!!
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Mkuu, chuo kilicho serious kisingepita kwa Michuzi?!I don' think whether you're right!!! Hapo lazima ujue kwamba walilenga kumtangazia nani!!! Kama target yao at that time ilikuwa East African students, TZ in particular, unazani ingekuwa rational kwao kutangaza kupitia media za Ulaya?! Umetoa good advice kwamba applicants, before doing so, watafute more information about the advertised college, and this's never Michuzi's business!!
   
 19. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  TATIZO SIYO HIVYO VYUO.

  Tatizo ni Mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia hivyo vyuo au Wizara husika ambayo inatakiwa kubuni sera itakayokidhi mahitaji ya soko.

  Mfano, Wizara ya Afya imefuta kozi za cheti kwa waganga,wafamasia na wauguzi then wakati huo huo wizara inasema haivitambui vyuo vilivyopo mitaani vinavyotoa mafunzo hayo,that is absurd!!!!!??????
  Wakati huo huo unasema vyuo hivyo visajiliwe kwa sheria ya VETA, wahitimu wakimaliza masomo yao unasema huwatambui?????!!!!!! nchi hii ni ya ajabu sana.

  Then mamlaka husika zinaagiza wahitimu wa diploma ndiyo wakauze maduka ya dawa baridi yanayouza Tsh.6,000 kwa siku, wakati wahitimu hao wanauwezo wa kupata kazi nzuri tu kwenye mahospitali ya private na serikali.Hao wa cheti ndiyo wangeweza kuadminister hayo maduka.

  Wajawazito bado wanajifungua kwa msaada wa Wakunga wa jadi huko vijijini hakuna wataalamu wa Afya, wakati RMAs walikuwepo kwa ajili hiyo, leo Wizara imesimamisha "uzalishaji" wa hawa Wahitimu , hata wale waliopo makazini wamepewa muda maalumu wa kujiendeleza kabla ya "maafa" hayajawakuta.

  Ndiyo maana watu wanapeleka watu kwenye hivyo vyuo vinavyoonekana "havina sifa"
  Watapeleka wapi watoto wao au wadogo zao , hawawezi kuwaacha washinde wakipiga soga.

  HILO LIPO KWNYE SEKTA ZOTE SIYO AFYA TU.

  Badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma.Tulianza vizuri , First Phase Administration ya Mwalimu iliweka misingi leo tumebomoa.

  Matokeo yake leo tunalaumiana, HOOH FULANI DEGREE YAKE FEKI ,HOO FULANI HANA PHD......PUUUUH

  MIAFRIKA BWANA..........
   
 20. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vyuo hivyo si vina Mamlaka zilizo juu yake zenye kutakiwa kuregulate na kuhakikisha vinaperform 2 the required standards?

  By the way,Asalaam aleikum Sheikh.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...