Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

Sehemu inayokuja naona no iliandikwa vibaya msiwe na wasi wasi tunaendelea hivyo hivyo
 
SEHEMU YA 94

Fareed aliumia moyoni mwake, hakujua sababu iliyomfanya Mungu kumpitisha katika maisha aliyokuwa akipitia kipindi hicho. Alidhamiria kubadilisha maisha yake, alidhamiria kumuabudu Mungu katika roho na kweli lakini pale alipokubaliana na moyo wake kwamba alitakiwa kubadilika, tayari tatizo likawa limetokea.

Alilia, alihuzunika, moyo wake ulichoma mno. Alimwamini Padri Luke kwa kuona kwamba angemuombea msamaha kwa Mungu ili maisha yake mapya yaanze rasmi lakini kitu cha ajabu kabisa, mwanaume huyo akaamua kumbaka.

Hakutaka kuendelea kubaki pale alipotupwa, akaondoka na kurudi hotelini, huko akakaa na kulia sana, akahuzunika mno na mwisho wa siku kupanga kurudi nchini Tanzania, alitaka kuanza upya kabisa, kama mtu aliyezaliwa kwa mara ya pili.

Alirudi nchini kimya kimya, hakutaka kumtaarifu Asteria kama alikuwa amerudi, alifanya hivyo kwa sababu alitaka kuyabadilisha maisha yake, aiondoe tamaa iliyokuwa mwilini mwake, asimtamani tena mwanaume ashinde vishawishi vyote na kuwa mtu mpya.

Akamtafuta daktari aliyekuwa akiwahudumia sana wanaume tata, huyo aliitwa Emmanuel Kihampa, daktari maarufu aliyekuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alipofika huko, akamfuata katika ofisi yake na kuanza kuzungumza naye.

Hakutakiwa kumficha kitu chochote kile, alitakiwa kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mwilini mwake, alimwambia tabia yake hiyo ambayo ilianza tangu utotoni, alimwambia juu ya tamaa kali aliyokuwa nayo.

Daktari huyo akampa vidonge vya kumeza lakini pia alitakiwa kuchomwa sindano nyumba kwa ajili ya kuua vijidudu ambavyo vilikuwa vikimuingiza katika matamanio makubwa. Hilo halikuwa tatizo, alidhamiria kubadilika, alidhamiria kuyabadilisha maisha yake, hivyo akachomwa sindano hiyo.

Haikutosha, akaambiwa kwamba ilikuwa ni lazima auweke mwili wake kimazoezi, alitakiwa kufanya mazoezi ya kila aina kuhakikisha anakuwa sawa.

Akaanza kukimbia mitaani, akawa anajiunga na vijana wengine kufanya mazoezi huku ikifika usiku, alitumia muda wake mwingi kusoma vitabu, yote hiyo ilikuwa ni harakati za kuachana na tabia chafu alizokuwa nazo kwamba asingeweza kufikiria ngono kama kipindi cha nyuma.
 
SEHEMU YA 95

Ilikuwa kazi kubwa, alipambana nayo, ilimtesa, ilimnyima raha kwani wakati mwingine alikuwa akishtuka kutoka usingizini, mwili ulikuwa ukimsumbua na kutandani, alikuwa na matamanio makubwa ya kuwa na mwanaume kipindi hicho, alivyokuwa akiiona hali hiyo, haraka sana alichukua mazoezi humohumo, kuruka kamba na kupiga pushapu kisa kulala.

Hayo yalikuwa ni maisha yake, hakuacha kwenda hospitalini, kila alipokwenda, alichomwa sindano nyumba kwa ajili ya kuua vijidudu vilivyokuwa vikimpa hamu ya kufanya mapenzi na mwanaume, ilimsaidia japokuwa ilionekana kuwa vigumu kumalizana na matatizo aliyokuwa nayo.

Kila siku alikuwa akienda katika sehemu ya mazoezi, gym kwa ajili ya kuchukua mazoezi mbalimbali hata kunyanyua vyuma. Alikuwa na muonekano wa kike, alikuwa na sauti iliyofanana na mwanamke lakini baada ya kuanza kufanya mazoezi, kunyanyua sana vyuma hatimaye mwili wake ukaanza kubadilika.

Akaanza kujazia, kifua chake kikaanza kuwa kipana, muonekano wa kike ukapotea, akaanza kuwa na six packs tumboni, mabadiliko hayo yote yalitokea ndani ya miezi sita, akaonekana kuwa mwanaume kamili, aliyeendelea kupata tiba kila siku na kufanya mazoezi ya nguvu.

Hakuwasahau watu waliomtenda, aliwachukia mno na hakutaka kabisa kuona watu hao wakiendelea kuishi. Alimkumbuka Keith, mwanaume mwenye roho mbaya ambaye alidhamiria kumuua baharini lakini kwa bahati nzuri sana akanusurika baada ya kuokolewa na mvuvi mmoja.

Hakuishia hapo, alimkumbuka bilionea Belleck ambaye alijifanya kumpenda, alimtumia alivyotaka na mwisho wa siku kutaka kumuua kwa kumtoa madawa ya kulevya yaliyokuwa tumboni, tena pasipo kujali kama alimsaidia kusafirisha madawa hayo au la.

Na mtu wa mwisho kabisa aliyemkumbuka alikuwa Padri Luke Mathew ambaye alimfuata kwa ajili ya kutubu dhambi zake lakini mwisho wa siku mwanaume huyo akambaka.

Alikumbuka kila kitu, hakutaka kuona watu hao wakiendelea kuishi kwa raha na wakati walishirikiana kumuumiza moyoni mwake, walishirikiana hata kuuumiza moyo wake.
 
Back
Top Bottom