Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 73

Hakushtukiwa na mtu yeyote yule, akatoka na kwenda sehemu ya watu waliokuja kuwasubiri watu wengine, hapo akamuona kijana mmoja akiwa amesimama huku akiwa na bango dogo lililoandikwa jina lake ambapo akamfuata na kujitambulisha kwamba yeye ndiye alikuwa Fareed.

“Are you Fareed?” (wewe ndiye Fareed?) aliuliza jamaa huyo huku akishangaa.
“Yes!” (ndiyo)
“How? Are you a boy or girl?” (Kivipi? Wewe ni mvulana au msichana?)
“Hey! You are wasting my time. Take me where Am suppose to be,” (Hey! Unanipotezea muda.

Nipeleke ninapotakiwa kuwa) alisema Fareed huku akionekana kuanza kukasirika.
Mwanaume huyo hakuongea kitu chochote lakini alionekana kuwa na maswali mengi kichwani mwake. Alikuwa akijiuliza kuhusu mtu aliyekwenda kumpokea, ilikuwa awe na jina la kiume na wakati alikuwa na muonekano wa kike?

Alivalia gauni refu, kichwani alikuwa na wigi, alipaka wanja na lipstic, sasa ilikuwaje awe mwanaume?
Hakutaka kujiuliza maswali zaidi bali ni kukaa kimya na kuendelea kuendesha gari kuelekea katika sehemu ambayo alitakiwa kumpeleka mgeni huyo. Akiwa hapo njiani akamtumia meseji Belleck kwamba mgeni aliyetakiwa kufika, tayari alikuwa ndani ya gari

*** Belleck aliwaanda vijana wake kwa ajili ya kazi ya kuyatoa madawa ya kulevya kutoka tumboni mwa Fareed. Yalikuwa ni madawa yenye thamani kubwa ambayo yangemuingizia kiasi kikubwa cha fedha.

Kete za madawa hayo zilikuwa tumboni mwa Fareed, kwa kawaida alitakiwa kwenda kujisaidia ili kutoa kete hizo lakini Bellck hakutaka kuona hilo likifanyika na badala yake alihitaji mtu huyo apasuliwe tumbo na kutolewa madawa hayo.

Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, waliwahi kufanya kazi kama hiyo kipindi cha nyuma kwa watu wengi, kuua, kwa vijana hao lilionekana kuwa jambo dogo sana ambalo lilikuwa ni kama kumuua sisimizi kwa kumkanyaga.

Walijiandaa nyumbani, walimtuma mwenzao kwenda kumpokea Fareed uwanja wa ndege ili atakapofika basi kazi ya kumpasua tumbo ianze mara moja.
 
SEHEMU YA 74

Belleck alivyotumiwa meseji kuambiwa kwamba mtu huyo aliwasili na alikuwa ndani ya gari, naye akawapigia simu vijana wake na kuwaambia kwamba mtu waliyeta kumpasua tumbo na kumtoa madawa hayo alikuwa garini akielekea hapo nyumbani.

“Hakikisheni mnamuua na kutoa huo mzigo. Ni wa gharama sana, kama ukipotea nitapata sana hasara,” alisema Belleck kwenye simu.
“Hakuna shida mkuu! Wapo njiani wanakuja.”
“Basi haina shida. Kazi njema.”
“Nawe pia.”
****

Hawakuchukua muda mrefu wakafika ndani ya jumba hilo la kifahari. Moyo wa Fareed ulikuwa ukitetemeka, hakuamini kama kweli alikuwa amenusurika katika mdomo wa kifo kwa bilionea Keith lakini mwisho wa siku alikuwa kwenye mdomo wa kifo kwa bilionea mwingine.

Aliumia na wakati mwingine alikuwa akijutia kazi yake ya kujiuza aliyokuwa akiifanya kwa moyo mmoja. Aliwachukia Wazungu, hakutaka uswahiba nao tena, kila alipoifikiria safari ya maisha yake mpaka kunasa kwa watu hao, moyo wake uliumia kupita kawaida.

Gari likasimama katika eneo la kupaki magari na wanaume wawili waliokuwa na bastola kutokea mahali hapo. Wakaufungua mlango na kumshusha Fareed kinguvu kisha kuanza kumpeleka ndani.

Walimshangaa mwanaume huyo, muonekano wake ukawatia hofu kwa kuhisi kwamba huyo hakuwa mwanaume kama walivyoambiwa, walihisi kwamba alikuwa mwanamke kutokana na muonekano wake wa kike aliokuwa nao.

Wakamchukua na kumpeleka katika chumba kimoja kilichokuwa na meza kubwa pamoja na vifaa vya kumfanyia mtu upasuaji. Fareed alipoviona vifaa hivyo na chumba hicho, moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama siku hiyo na yeye alibebeshwa madawa ya kulevya kama walivyokuwa wakifanyishwa watu wengine.

“Call Dr. Watson,” (mpigie simu daktari Watson) alisema mwanaume mmoja.
Bonny Watson alikuwa daktari kutoka katika Hospitali ya St. Napoleon iliyokuwa hapohapo Marseille nchini Ufaransa.

Daktari huyu ndiye aliyekuwa akitumiwa sana na Bilionea Belleck kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji watu wote waliokuwa wakimeza kete za madawa ya kulevya nchini Ufaransa.
 
Hivi na haya mahadithi sijui story hamnaga kazi zakufanya?
 
Back
Top Bottom