SEHEMU YA 67
Muda huo ulikuwa zamu ya Mzee Sadiq, alilala na Fareed usiku kucha, haikuishia siku hiyo, huo ulikuwa muda wake wa kuwa na mwanaume tata huyo. Maisha ya Fareed yaliendelea kubadilika, alikaribia kuwa milionea kwa sababu tu alijiuza kwa wanaume matajiri ambao walikuwa tayari kutoa kiasi chochote cha fedha mpaka kufanikisha kile walichokuwa wakikihitaji.
Siku ziliendelea kukatika, waliendelea kuwa pamoja. Japokuwa maisha yalikuwa mazuri, alipata kila kitu alichokuwa akikihitaji lakini hakuacha kuwasiliana na wanaume wengine, wote hao alitaka kulala naye na mwanaume ambaye alikuwa na hamu naye kwa kipindi hicho alikuwa Belleck.
Aliendelea kuwasiliana na mwanaume huyo, hakutaka kuonana naye kwa muda huo, alitaka kumuweka kiporo, alale naye katika siku za mwisho za kutaka kuondoka nchini humo.
Kwa kuwa mwanaume huyo alimuhitaji sana, alijitahidi kumtumia kiasi kikubwa cha fedha, kila shida ambayo Fareed alikuwa akiililia, alitumiwa fedha na mwanaume huyo ingawa hawakuwa wameonana.
Baada ya kukaa na Mzee Sadiq kwa siku kadhaa hatimaye akaamua kuondoka nyumbani kwa mzee huyo na kwenda kuonana na Belleck ambaye alionekana kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.
Macho yake yalipotua kwa mwanaume huyo, moyo wake ulimlegea, alikuwa mwanaume mwenye sura nzuri, ya kitoto ambapo mwili wake ulikuwa umejazia kidogo. Alipomuona tu, moyo wake ukatokea kumpenda, alikuwa ana mvuto wa ajabu, zaidi ya wanaume wote ambao aliwahi kukutana nao.
Belleck alivalia suti iliyotengenezwa na Kampuni ya Pollo, alivalia saa nzuri, ya thamani iliyotengenezwa na Kampuni ya Solex, kwa kifupi, muonekano wake ulikuwa ni wa kitajiri.
“Fareed…” aliita Belleck huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Nimekuja kukuona mpenzi!” alisema Fareed.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuonana na mwanauume huyo, kilichofuata baada ya hapo ni kula maisha kwa kutembea sehemu mbalimbali. Fareed alijisikia amani moyoni, hakuuacha kumshukuru Mungu kwa kumuumba mwanaume.