Michezo inaleta uhai kwa maendeleo ya vijijini China na Kenya

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111454741074.jpg


Michezo ya 19 ya Asia ilifunguliwa tarehe 23 mjini Hangzhou, China. Katika miaka 15 iliyopita, toka Michezo ya Olimpiki ya Beijing, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing hadi Michezo ya Asia ya Hangzhou inayoendelea sasa, China imekuwa mwenyeji wa michezo kadhaa muhimu ya kimataifa, ambayo sio tu imeifanya dunia kuiona China kwa mapana yake, bali pia imewahamasisha wachina wengi wa kawaida kushiriki katika michezo, jambo ambalo ni muhimu hasa katika mikoa ya kati na magharibi ambayo inakabiliwa na kazi nzito ya maendeleo ya vijijini.

Katika msimu huu wa joto, katika kaunti ya Rongjiang, mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, mechi ya soka ya mashinani inayojulikana kama "ligi ya soka ya vijiji" ilipata umaarufu bila kutarajiwa. Nyota wa michezo kutoka ndani na nje ya nchi, akiwemo mchezaji maarufu wa Uingereza Michael Owen, walituma salamu zao.

"Ligi ya soka ya vijiji" ni mashindano yaliyoandaliwa na wanakijiji wenyewe. Kwa mfano, katika kaunti ya Rongjiang, timu zinapocheza, karibu kijiji kizima, vijana kwa wazee, wanajitokeza kwa wingi na kushangilia wakivaa mavazi ya kikabila, na hii imeenea na kuwagusa watu wengi kupitia mtandao wa internet.

Wakati wa mashindano ya wikiendi, watalii wengi walimiminika Rongjiang, na mahitaji yao na chakula, nyumba, usafiri, na utalii yalichangia kipato kwa sehemu hiyo ndogo.

Kulingana na takwimu, katika kipindi cha "ligi ya soka ya vijiji", mauzo ya bidhaa za kilimo za kaunti ya Rongjiang ndani na nje ya mtandao wa internet yalizidi yuan milioni 400, karibu dola milioni 55, ikiwa ni ongezeko la karibu 60% kuliko mwaka jana kipindi kama hicho.

Ikiwa moja ya kaunti za mwisho nchini China kuondolewa kwenye umaskini na moja ya kaunti za China kupokea uungaji mkono wa kitaifa kwa ajili ya kustawisha vijiji, kaunti ya Rongjiang imetumia fursa ya "ligi la soka la vijiji" ili kujistawisha kwa njia ya kipekee.

Kwa bahati, katika mji mdogo wa Iten nchini Kenya, maelfu ya maili kutoka Rongjiang, michezo pia imebadilisha sura ya huko. Hapo awali Iten ulikuwa mji wa kilimo ulio nyuma kimaendeleo, lakini katika miaka 15 iliyopita, uchumi wa Iten umeboreka sana.

Wanariadha maarufu kutoka kote duniani, wakiwemo timu ya kitaifa ya China ya Marathon, wamepata mafunzo katika mji huo, na kwa pamoja na wanavijiji wa huko wanaopenda kukimbia, wametengeneza Iten kama "kijiji cha mbio za masafa marefu".

Mabingwa wengi wa dunia waliopata mafunzo hapa wamerejea Iten na kuwekeza katika hoteli mpya na shule za mafunzo, na kusababisha kushamiri kwa biashara na utalii. Wanakijiji hawalazimiki tena kusafiri umbali mrefu kutafuta maisha, na wamepata kazi nzuri katika mji wao mdogo.

Kwa sasa, serikali ya Kenya imejitolea kugeuza miji midogo kama Iten kuwa vivutio vya michezo na utalii, kukaribisha wanariadha na watalii kutembelea huko, kuvutia uwekezaji, na kubadilisha barabara nyingi za udongo kuwa njia za kukimbia.

Kutoka Rongjiang nchini China hadi Iten, Kenya, ingawa kuna umbali wa maelfu ya maili, maeneo hayo yote yanatafuta maendeleo kupitia michezo. Katika siku zijazo, iwe "ligi ya soko ya vijiji", mbio za masafa marefu, au michezo mingine, michezo inapaswa kutumika kama nguvu mpya za kiuchumi ili kuleta matumaini na fursa mpya kwa maendeleo ya maeneo ya vijijini China na nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom