Mawasiliano ya michezo yamekuwa daraja muhimu kati ya watu wa China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111448029889.jpg
Kileta bahati cha Michezo ya Kimataifa ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ya Majira ya Joto ya Chengdu “Rong Bao” kimepata jina la Kiswahili la “Jasiri”, ambalo linaonesha matarajio ya watu wa Kenya kwa wanariadha wa nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika michezo hiyo, na pia kuelezea urafiki kati ya watu wa Afrika na China, ambayo wako mbali kwa maelfu ya kilomita.

Jumla ya nchi 24 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, zimetuma ujumbe kushiriki kwenye michezo hiyo, na Kenya iliandaa michuano maalumu iliyofanyika kwa kipindi cha miezi 6, ili kuchagua wanariadha hodari zaidi kutoka kwenye vyuo vikuu vyote nchini humo.

Katika miaka ya hivi karibuni, michezo imezidi kuwa sehemu muhimu ya mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Afrika, na pia imekuwa daraja muhimu kati ya watu wa pande hizo mbili.

Mawasiliano ya michezo kati ya China mpya na Afrika yalianza miaka ya 1950. Mnamo mwaka 1957, timu ya wachezaji wa Pingpong ya China ilitembelea Misri, na kuwa timu ya kwanza ya michezo ya China mpya iliyotembelea barani Afrika. Baadaye hatua kwa hatua, michezo imekuwa daraja la mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika.

Ujenzi wa majumba na viwanja vya michezo ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa michezo kati ya China na Afrika. Majumba na viwanja vya michezo vilivyojengwa na kampuni za China vinapatikana katika bara zima la Afrika. Kiwanja cha Michezo cha Brazzaville nchini Jamhuri ya Watu wa Kongo kilichojengwa na kampuni ya China ni kiwanja cha pili kwa ukubwa barani Afrika. Takwimu zinaonesha kuwa hivi sasa, kampuni za China zinajenga zaidi ya majumba na viwanja vikubwa 80 vya michezo barani Afrika, ambavyo vina uwezo wa kuchukua watu milioni 3. Majumba na viwanja hivyo vya kisasa vinachangia maendeleo ya michezo barani Afrika.

Kutokana na maendeleo endelevu ya China na kuongezeka kwa mawasiliano ya michezo kati ya China na Afrika, katika miaka ya hivi karibuni, China pia imetuma wataalam wengi wa hali ya juu wa michezo katika nchi za Afrika ili kuzisaidia kuboresha kiwango cha mashindano ya mpira wa meza, mpira wa wavu na michezo mingine. Hatua hiyo si kama tu imechangia maendeleo ya michezo ya Afrika, bali pia imehimiza zaidi urafiki na maelewano kati ya watu wa Afrika na China.

Mawasiliano ya michezo ni kama mtitiriko wa taratibu wa maji, kutokana na mvuto wake maalum, yamekuwa njia muhimu ya mawasiliano ya kiutamaduni kati ya watu wa China na Afrika, na kujenga daraja la kuelewana la kuvuka bara kati ya watu hao.
 
Back
Top Bottom