Miche toka Morogoro

Miche toka Morogoro

Wickama

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2009
Posts
1,568
Reaction score
1,350
Wakuu, niliagiza miche ya miembe toka Morogoro. Kwa kweli quality yake ilinitia mashaka. Shambani ni kama 70% ili-fail. Rafiki yangu akanishawishi niagize toka Nairobi.

Kwa kusita nikaagiza. Hii ilikuja mizuri sana kwa bei sawia. Hadi leo 90% ipo shambani. Nauliza Kuna yeyote humu amepatwa na madhila kama haya? Kwenye picha nilizoambatanisha unadhani ni ipi ya Mji kasoro bahari?😅
20250516_090731.jpg
20250413_111054.jpg
 
Kwenye udongo usiouelewa otesha michungwa au milimao ...

Mimi nili agiza kutoka SUA, ambayo ni mipera,michungwa, milimao na miembe

Miche kama 700 hivi

Ila imepona kama 200, nilichogundua Miche pekee kwa eneo usilolifahamu ni Bora uoteshe michungwa na milimao inakubali bila hitilafu yeyote
 
Kununua miche SUA haimaanishi ni 100% umepata miche bora, umakini unahitajika.
 
Safi sana nyie ndio mnaipa dunia hewa safi sana🙏
 
Hiyo ya Nai hukufanya mabadiliko yoyote ya uandaaji mashimo ya kupandia.

BTW: Nilijua kuna ukiritiba kwenye uagizaji mbegu na miche kutoka nje!!
 
Morogoro kuna wahuni wengi wanaouza Miche kwa jina la SUA. Sio miche yote utakayoambiwa imetoka SUA kweli itakuwa imetoka chuoni. Ukiagiza hakikisha uliyemuagiza anafika chuoni, katika idara husika, utapata miche yenye ubora.
 
Kwenye udongo usiouelewa otesha michungwa au milimao ...

Mimi nili agiza kutoka SUA, ambayo ni mipera,michungwa, milimao na miembe

Miche kama 700 hivi

Ila imepona kama 200, nilichogundua Miche pekee kwa eneo usilolifahamu ni Bora uoteshe michungwa na milimao inakubali bila
100%
 
Wakuu, niliagiza miche ya miembe toka Morogoro. Kwa kweli quality yake ilinitia mashaka. Shambani ni kama 70% ili-fail. Rafiki yangu akanishawishi niagize toka Nairobi.

Kwa kusita nikaagiza. Hii ilikuja mizuri sana kwa bei sawia. Hadi leo 90% ipo shambani. Nauliza Kuna yeyote humu amepatwa na madhila kama haya? Kwenye picha nilizoambatanisha unadhani ni ipi ya Mji kasoro bahari?😅
View attachment 3420831View attachment 3420832
Ramli chonganishi hiyo😂😂😂
 
hujaeleza kwanini ili-fail mkuu
 
hujaeleza kwanini ili-fail mkuu
Zamani nilipofundishwa ku-transplant shambani miche iliyofanyiwa budding au grafting niliambiwa subiri hadi shina la mche husika liwe angalau na unene wa kalamu ya pencil. Hili somo nililisahau.
Miche mingi niliyopokea toka kasoro bahari haikuwa na unene huu. Ilikuwa myembamba zaidi. Pia ilikuwa na viriba vidogo. Nahisi haya mawili ndio yaliiua tulipoihamishia shambani. Ya Nairobi ilikuwa minene na viriba vilikuwa vikubwa. Haijafa.
 
sawa mkuu
 
Mi nadhani Moro kuna demand kubwa ya miche toka Bongo nzima (brand ni SUA) kiasi kwamba mazingatio ya ubora inakuwa mtihani
naam mkuu, namna ya kufanya regulations imeshakua changamoto, lakini pia ni nidhamu ya kazi mbovu tu kuna muda unapokea miche ukiiangalia tu unajiuliza maswali kama itaweza kutoboa --- lakini tunasonga
 
Wakuu, niliagiza miche ya miembe toka Morogoro. Kwa kweli quality yake ilinitia mashaka. Shambani ni kama 70% ili-fail. Rafiki yangu akanishawishi niagize toka Nairobi.

Kwa kusita nikaagiza. Hii ilikuja mizuri sana kwa bei sawia. Hadi leo 90% ipo shambani. Nauliza Kuna yeyote humu amepatwa na madhila kama haya? Kwenye picha nilizoambatanisha unadhani ni ipi ya Mji kasoro bahari?😅
View attachment 3420831View attachment 3420832
SUA kama SUA hawazalishi miche pale ni wahuni wanao tumia jina la SUA na nashangaa sana SUA kukaa kimya
 
Back
Top Bottom