Miaka sitini na tatu unaoa ili iweje?

Miaka sitini na tatu unaoa ili iweje?

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Hivi kama uefiwa ni umefika hiyo miaka kama 55-65 unatoa sababu gani za msingi kuoa tena? Mimii huwa siridhishwi kuona mtu wa umri huu akioa zaidi najiuliza huyu mzee mhuni ama ni wajibu anatimiza?.

Karibuni tujadili
 
Ana sababu zake za msingi zilizo msukuma kuna.
 
Labda anataka mtu wa kumfulia nguo na kumdekia nyumba yake.
 
ana haja za mwili kama wengine ...sasa kuliko kufanya uhuni anaona bora aoe atulie na huyo mmoja...

mi mwenyewe 36 nikiamua naweza kuuchuna tu bila hiyo mambo ndio nashangaa hapo ngozi ishajikunja unakuwa na haja gani za mwili kama si kuchekesha
 
Bado uhitaji wa tendo unakuwa mkubwa sana kwake, kwa hiyo anaona ni bora ajitwalie kabisa wa kumalizia naye maisha.
 
Hapa mkuu umepotea kidogo,

Kama akioa kichanga kweli ni nongwa, lakini kama kaoa mzee mwenzake kuna ubaya gani? Nashauri, mjane au mgane si vizuri kuruka ruka kama afya inaruhusu. La pili, Wagane wengi huwa ngumu sana kuishi baada ya mamsapu kutangulia mbele ya haki, hivyo upweke huwa ni ugonjwa mkubwa kwao, lakini akimpata mwenzake si vibaya.

La tatu, kwani kuishi duniani mwisho miaka mingapi? Maana niko na mdogo wangu Mgabe pale Zimbabwe kagonga 93, na alifiwa miaka mingi iliyopita, sasa kama angefuata falsafa yako, angeishije?
 
Nipo pamoja na wewe
 
haya ni mawazo ya mtu anayefikiri ndoa ni tendo la ndoa tu. Katika maisha ya ndoa kuna mengi mno, ingia kwanza katika ndoa then utajuwa.
 
Hapa mkuu umepotea kidogo,

Kama akioa kichanga kweli ni nongwa, lakini kama kaoa mzee mwenzake kuna ubaya gani? Nashauri, mjane au mgane si vizuri kuruka ruka kama afya inaruhusu. La pili, Wagane wengi huwa ngumu sana kuishi baada ya mamsapu kutangulia mbele ya haki, hivyo upweke huwa ni ugonjwa mkubwa kwao, lakini akimpata mwenzake si vibaya.

La tatu, kwani kuishi duniani mwisho miaka mingapi? Maana niko na mdogo wangu Mgabe pale Zimbabwe kagonga 93, na alifiwa miaka mingi iliyopita, sasa kama angefuata falsafa yako, angeishije?
nimecheka sana mdogo wako nanii
 
Majibu umeshayapata tayari. Ndoa ni tendo kwa vijana lakini umri ukisogea sana mtu anahitaji companionship.

Awe na mtu wa kukumbatia akilala,

awe na mtu wa kuongea naye chumbani,

awe na mtu hata wa kumweleza matatizo ya afya yake,

awe na mtu wa kuita mamsap, mpaka hapo upooo?
 
nimecheka sana mdogo wako nanii

Afadhali wewe umecheka na kujiongezea uhai kwa leo, huyu jamaa anataka kuleta hadithi za vijiweni. Kwani hawezi kuwa mdogo wangu huyu nanii!!!!!! Unajua mimi nina umri gani?

Yule ni mdogo wangu wa pili !!!!!!!
 
Mke Au mume katika ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa.
 
Huu ni wivu wa kihovyo.

Kama wewe katibu kata wako kishachoka na kuzeeka kwa hiyo unataka na wa wenzio wachoke na kuzeeka!!!

Wenzako wanakula lishe saaafi kwa hivyo na afya zao ziko sawa. Wewe shindia chips na lalia chips tu.
 
Back
Top Bottom