Miaka Niliposoma Vitabu 1000 na Zaidi

Miaka Niliposoma Vitabu 1000 na Zaidi

nimeshiba...nikisoma nitasinzia...ngojea nikiamka usiku wa manane nitaipitia tena.
 
Unadhani pale ambayo hauna uhakika.
"pale ambapo huna(sio hauna) uhakika"

Unaweza kutumia neno "Nadhani";
1. Kama unatoa maoni kutoa nafasi wengine watoe maoni yao pia... You give a room for others to air their opinion..!
2. Kama huna uhakika na mada husika, hii ni kuweka nafasi ya kukosolewa.

''Nadhani anaihamasisha jamii"...hapa naongelea nafsi nyingine, kwa hiyo siruhusiwi kuhitimisha kwa kusema "Anaihamasisha jamii"

Tafadhali nikosoe ''pedagogist"
 
Nilipenda kusoma utotoni.Lkn kutokana na kukimbizana na maisha nimepoteza hobby .
 
Ukitaka kumficha mwafrika kitu chochote weka ujumbe kwenye kitabu. Waafrika ni wavivu sana wa kusoma na kufanya tafiti ndio maana ata thesis nyingi za wasomi wetu huko nyumbani yanajirudia au ni marudio.
 
nimejitahidi mara nyingi kuwa msomaji wa vitabu,kila nikianza nasoma vizuri muda unafika najikuta nakata tamaa ya kuendelea kusoma vitabu,nafikiri maisha ya Watanzania yamejengwa kwenye kutafuta fedha na kuhangaika na maisha,ndiyo msingi haswa tulikojengwa ndiyo maana Tanzania inashindwa kutoa wataalamu wa kushindana kimataifa,Rose Migiro angekuwa amejengwa kwenye msingi wa usomaji vitabu kama Thabo Mbeki bado angekuwa ameshikilia nafasi yake ya Deputy UN Secretary,ni aibu mno kwa taifa letu kuwa na kiongozi kama Kikwete anayeshindwa kuteua mawaziri wenye uwezo wa kuongoza kwa sababu ya kutokusoma vitabu,mageuzi hayawezi kuja japo yanatamaniwa na watanzania walio wengi kwa kuwa hatuna maarifa ya kuyaleta hayo mageuzi,uwezo wetu ni mdogo sana kiasi kwamba tunadharauliwa kimataifa,japo Mwanakijiji umeeleza historia yako kwa kifupi imenifurahisha sana hasa ulipotaja kuwa umetoka Tanga,tulifikiri Tanga wanatoka watu wasiopenda maendeleo katika Elimu,nimependa wazo lako
 
"pale ambapo huna(sio hauna) uhakika"

Unaweza kutumia neno "Nadhani";
1. Kama unatoa maoni kutoa nafasi wengine watoe maoni yao pia... You give a room for others to air their opinion..!
2. Kama huna uhakika na mada husika, hii ni kuweka nafasi ya kukosolewa.

''Nadhani anaihamasisha jamii"...hapa naongelea nafsi nyingine, kwa hiyo siruhusiwi kuhitimisha kwa kusema "Anaihamasisha jamii"

Tafadhali nikosoe ''pedagogist"

Ulikuwa hauna uhakika kama anajisifu ndiyo maana ukasema unadhani. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango, rudi nyuma ujikumbushe, unaonesha ni mfupi wa kumbukumbu.
 
Ulikuwa hauna uhakika kama anajisifu ndiyo maana ukasema unadhani. Wacha kuhohoroja na kubwabwaja bila mpango, rudi nyuma ujikumbushe, unaonesha ni mfupi wa kumbukumbu.
Oh poor you..!
pedagogist my foot..!
 
Nilikuwa na utamaduni wa kujisomea miaka ya tisini mpaka 2010, natamani sana nianze tena mkuu Mwanakijiji.Hivyo vitabu nilivisoma miaka hiyo ila tatizo miaka hii mambo yanabana nikirudi kazini saa 11 jioni nakuwa hoi nikishika novel ni usingizi tu bora hata movie naweza kuangalia.Lakini nina maktaba ya nyumbani sio muda naanza tena kusoma na nitajaribu hata kushawishi wengine wajaribu.
 
hakika hii mada imenigusa sana! kuna haja serikali ikaweka sera maalum kuhamasisha watu kusoma vitabu binafsi mi ni msomaji sana wa vitabu na kwa uhakika huwa naona mabadiliko maishani mwangu kutokana na kujisomea
 
Tabia ya kuhudhuria maktaba nilikua nayo sana hadi nlipoanza kazi nilikua narenew uanachama... Ikaishia wapi cjui..
 
Back
Top Bottom